Msanii namba 1 Afrika kwa sasa, Diamond Platnumz ajenga nyumba ya Ibada (Msikiti)

That's my girl [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Kidini hivi inaruhusiwa?
Mana mimi najua mziki ni haram na fedha anazojengea ni zao la muziki.
Kama nakosea nirejebishwe.
Wajuvi tujuzeni kama hii ni sahihi?
Misikiti mingi huku mitaani inajengwa kwa swadaka na michango mbalimbali yetu sisi waumini.
Kuna anayejua kila swadaka/mchango wa muumini chanzo chake ni khalal?
Ni wapi swadaka ya muumini imewahi kukataliwa msikitini?
Tena wengine ni 'madon' wa sembe na Masheikh wanajua fika ila swadaka zao wanazipokea.

Allah ndiye hakimu,atamhukumu kila mmoja wetu kwa kadiri ya aliyoyatenda.
Period
Kwa kweli mimi ni shabiki wa Diamond lakini kusema yeye ajenge msikiti na watu wakaswali kabisa siungi mkono. Anayo yafanya sidhani kama dini ina yaunga mkono.

Ni sawa sawa na jay z ajenge kanisa, au davido ajenge kanisa. Yaan haija kaa poa.
 
Yaani hapa umenikosha sana...... Ajabu hawaoni kuwa hizo sadaka twazitoa tena wengine tuna dhambi hatari diamond haoni ndani...

Good job Diamond
 
Huo ni msikiti au kajumba ka kunywea kahawa? Angejenga walau wenye size ya msikiti wa Mahita Moro au ule wa Ghadafi Dom tungemuelewa
We mbona mama ako aishi kwenye nyumba mbavu za mbwa, mjengee walau hata ya tope ndio uje kusengenya wana wa wenzio.
 
Huge masekela, Yousou N'dor, Salif Keita, Manu Dibangu, Oliver Mutukudzi wako bara lipi na namba gani?
 
Acha kudanganya watu Huyo diamond hayupo hata kumi bora Africa au nikupe orodha ya wasanii matajili afrika?
Kuna sehemu nimesema TAJIRI, umekula kweli mchana au njaa njaa zako umekuja kwenye bandiko langu na nenge?
 
uislamu unaruhusu music ya kidunia na hereni na tatuu
 
Yaani hapa umenikosha sana...... Ajabu hawaoni kuwa hizo sadaka twazitoa tena wengine tuna dhambi hatari diamond haoni ndani...

Good job Diamond
Binadamu utatuweza mama?Tena tukishakaa nyuma ya fake ID's wakamilifu ndio sisi, wajuaji wa kila kitu ndio sisi.
Aaaarrrgghhh
Waungwana tunampa pongezi zetu namna hii.
 
Kwa mara ya kwanza umenifurahisha kumuongelea vizuri Diamond.
 
Kwakuongezea tu ni kwamba,kuna mizani ya kupima heri(mema)na mabaya,hili ni jambo la kheri,aungwe mkono.
 
Huge masekela, Yousou N'dor, Salif Keita, Manu Dibangu, Oliver Mutukudzi wako bara lipi na namba gani?
Kila mtu na zama zake, ndio maana nikasema bora kwa mwaka huu. Wala sijazungumzia utajiri ila ubora wa msanii. Hao uliowataja walikuwa bora kwa wakati wao sasa hivi wamebaki kupewa heshima tu. NIMEELEWEKA
 
Umepata wapi mamlaka ya kumhukumu mwenzio..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…