Msanii namba 1 Afrika kwa sasa, Diamond Platnumz ajenga nyumba ya Ibada (Msikiti)

Msanii namba 1 Afrika kwa sasa, Diamond Platnumz ajenga nyumba ya Ibada (Msikiti)

"INNA LLAHA TWAYYIBUN LA YAQBALU ILLA TWAYYIBA" INA MAANA KUWA "HAKIKA YA ALLAH(MW/MUNGU) NI MZURI HAKUBALI ILA VILIVYO VIZURI". PERIOD. ILA MLANGO WA TOBA UPO AKIACHA AYAFANYAYO NA KUMREJEA MOLA WAKE BASI ATASAMEHEWA KWANI HAKIKA YA MW/MUNGU NI MWINGI WA MSAMAHA KWA WAJA WAKE.
nikuulizee..?!
 
Mashehe watujuze msikit umejengwa kwa pesa ya haram je itaswihi watu kuswal humo
 
hivi mtoa mada kumbe uliandika msanii namba1 africa? Aisee sikuona kabisa hii pumba uliyoandika list ya wasanii bora Africa ni ndefu sana hadi umkute Diamond acha kuandika kwa mahaba
 
pesa za wimbo unasema "anifinyie kwa ndani.." ndio zinajenga msikiti?
 
Kila mtu na zama zake, ndio maana nikasema bora kwa mwaka huu. Wala sijazungumzia utajiri ila ubora wa msanii. Hao uliowataja walikuwa bora kwa wakati wao sasa hivi wamebaki kupewa heshima tu. NIMEELEWEKA
ndugu we unaishi kwenye handaki nn? unaonekana huna Idea kinachoendelea duniani
 
Huo ni msikiti au kajumba ka kunywea kahawa? Angejenga walau wenye size ya msikiti wa Mahita Moro au ule wa Ghadafi Dom tungemuelewa
daaaaah mkuu ndo uwezo wake kumkomesha we jenga mkubwa kuliko huo alafu kimya kimya wala uclete habar hapa jamvini
 
Hili ni jambo la kheri,halipaswi kabisa kubezwa.
Pamoja na madhaifu yake kama binadamu ila kwa hili nampongeza.

Ifikie mahali tuache unafiki,ni nani asiye na dhambi kati yetu?Kuvaa kwake hereni hakumzuii kujenga msikiti, ingekuwa ndio hivyo basi hata swadaka tulio wengi tusingetoa misikitini maana kama ni utimilifu ndio kigezo cha kutoa swadaka hakika hakuna aliye kamili zaidi ya Mtume Muhammad (S.A.W)

Allah akuzidishie kheri Nasib,uzidi kujenga misikiti mingine mingi watu wapate kufanya ibada na kumcha Mola wetu.
Mumche Mola huku kiburudika na nataka kulewa lewa nataka kulewa lewa
 
Huo msikiti haufai kufanyiwa ibada ya swala
wakati mwingine bora kunyamaza tu haswa kwa mambo ucyo na elimu nayo maana ukiongea ndo watu hutambua we ni mmtu wa namna gani
 
Sidhani kama inaruhusiwa katika hiyo dini, labda kama atasali yeye na kundi lake la WCB
 
hivi mtoa mada kumbe uliandika msanii namba1 africa? Aisee sikuona kabisa hii pumba uliyoandika list ya wasanii bora Africa ni ndefu sana hadi umkute Diamond acha kuandika kwa mahaba
Kwa sasa.
 
Back
Top Bottom