Hili ni jambo la kheri,halipaswi kabisa kubezwa.
Pamoja na madhaifu yake kama binadamu ila kwa hili nampongeza.
Ifikie mahali tuache unafiki,ni nani asiye na dhambi kati yetu?Kuvaa kwake hereni hakumzuii kujenga msikiti, ingekuwa ndio hivyo basi hata swadaka tulio wengi tusingetoa misikitini maana kama ni utimilifu ndio kigezo cha kutoa swadaka hakika hakuna aliye kamili zaidi ya Mtume Muhammad (S.A.W)
Allah akuzidishie kheri Nasib,uzidi kujenga misikiti mingine mingi watu wapate kufanya ibada na kumcha Mola wetu.