Msanii Q Jay aingia kwenye madawa ya kulevya

Msanii Q Jay aingia kwenye madawa ya kulevya

mleta mada huyo dogo si nilisikia ni mlokole wa kutupwa?... nakumbuka kati ya mwaka 2015 au 2016 nilimsikia akihojiwa na dullah wa east africa radio, alikiri kwamba yeye kwa sasa ni mlokole na hatakuja tena kuimba bongofleva.

baadae nikaja kusikia story mtaani kuwa aliingia kwenye ulokole kwa shinikizo la wakwe zake. yaani alipata mke halafu wazazi wa mke wakatoa sharti lazima aokoke ndio aweze kumuoa mtoto wao.

inawezekana pia kaingia kwenye matumizi ya madawa kutokana na stress za ndoa baada kugundua ndoa imempotezea mda wake.

hivi mallow kapotelea wapi?... nasikia na yeye aliacha mziki kwa masharti kama hayo ya q jay.
Yeah nakumbuka mahojiano yake dullah ch 5,,alikataa kuimba nyimbo zake za zamani kisa ulikole wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Q Jay nilikutana naye Bukoba mwaka jana mwezi wa 12, niliongea naye kidogo akaniambia anaishi BK kwa sasa na huwa anatumbuiza kwenye mahotel. Alinipa mualiko ila sikuweza kwenda, sikuwahi kuonana naye tena baada ya hapo. Ila kimuonekano alikuwa poa tu, labda kama hali yake ilibadilika baada ya hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nini kuokoka bana,kwani Rose muhando hajaokoka?
 
So so bad. Nawapongeza Ally Kiba na Dimond hawajelewa umaarufu na wala hawajafata mikumbo ya madawa. Mungu awaepushe wawe mifano mizuri hivyo hivyo
Bado hawajashuka!
Tujipe muda ukifika washuke kimuziki ndio tutakua rangi yao halisi!
 
hii hoja yako" nilishawahi kuisikia zamani" magomeni mitaa ya sunna" vijana walikuwa waki shauriana huo ujinga
hata watoto wa kinondoni kuanzia mkwajuni mpaka kule chini hananasif wana mawazo hayo hayo, wanadai unga unawasaidia katika harakati zao za u ben10
 
hata watoto wa kinondoni kuanzia mkwajuni mpaka kule chini hananasif wana mawazo hayo hayo, wanadai unga unawasaidia katika harakati zao za u ben10
hiyo kanda yote vijana wake hawana tofauti kitabia" kuna baadhi ya vijana wengi niliocheza nao utotoni sasa hivi nimateja wengine walianza kujiongopea kama hvyo
 
hiyo kanda yote vijana wake hawana tofauti kitabia" kuna baadhi ya vijana wengi niliocheza nao utotoni sasa hivi nimateja wengine walianza kujiongopea kama hvyo
Madawa ni kuomba tu usiingie tu mambo ya kufata mkumbo haufai...
Wengine tulipokulia tumezungukwa na mapusha siku zote ktk maisha Fata akili yako tu
Kama wewe ulikuwa mwenyeji Kino enzi hzo kilikuwa na kijiwe kimoja kinaitwa Ajax mm nlikulia pale sehemu hyo kilikuwa na mateja mapusha kulikuwa na mbilinge zote fujo zote aise
Nyumba nyingi pale walikuwa wanaojihusisha na ngada ilibidi polisi toka kitengo nakumbuka walikuja kupiga kambi pale mwezi mzima lkn Pali kuwa balaa kama Mexico

Ova

hahaaa Mimi nimekulia kino brazil mzee baba " ni hatari aiseee" mtihani sana wallahi
 
Sio kweli wengi wanataka kupoza stress na kutumia kunaanza baada ya kujiingiza kwenye biashara ya kuuza akiwa na imani hatotumia ila in long run unakuta anaanza kujaribu bidhaa yake kwa kuonja mzigo kama OG
Sababu yake ni ya kweli kuna wadogo wawili nawajua ni mateja though mmoja ameshafariki walitoa sababu hiyo hiyo nilipowauliza walianzaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom