Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Halafu ikawaje ?nasikia mbowe kashamtayarishia tundu lisu selo ya kukaa segerea siku akirudi bongo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halafu ikawaje ?nasikia mbowe kashamtayarishia tundu lisu selo ya kukaa segerea siku akirudi bongo
Atatangulia mbowe kwanza huko gerezaniKuna dalili zote kuwa unabii wa ChidBenz umeanza kutimia.
Alimuambia Makonda badala ya kuwekeza fedha kwa wasanii, jenga magereza kwa kuwa na wewe waweza kuwa mfungwa siku moja
Mbowe mbona kishaenda mara kadhaa !Atatangulia mbowe kwanza huko gerezani
Exactly..Mungu sometime hua anatumia hata punda au mawe kusema kama watumishi viongozi wa dini wakikaa kimya
NikweliNi swala la muda tu kabla maneno hayo hatajatimia.
Wanaona raha kuweka wapinzani ndani ila hawajui kuwa kuna siku na wao wataingia humo.
Sikuwa namtilia maanani sana msanii huyu awali lakini baada ya kumsikiliza nimegundua ana akili sana tofauti na wanavyo mchukulia watu wengi.
Mwishoni mwa mahojiano yake katoa ushauri Kwa Makonda aache kujiingiza mambo mengi yasiyo maana ikiwemo wasanii Kwa kutaka wamsifie wakati wao wanataka hela tuu.
Ajikite mambo ya maana ikiwamo kuboresha hata Segerea kwani yeye au hata Magufuli kama kuna waliyotenda Kwa makosa sasa wajue wataenda kule hivyo waboreshe makazi yao.
Ujumbe murua, Ila waweza kubezwa
=======
Ni mwanamuziki wa Hip Hop Tanzania. Maarufu ‘Chidi Benz’. Kwa miaka kadhaa Chidi amekuwa alama ya waathirika wa dawa za kulevya.
Chidi ni kielelezo cha anguko la vijana maarufu wenye kutumia mihadarati. Hata hivyo, hivi karibuni alizungumza mambo ambayo kimsingi yalipaswa kujadiliwa na Bunge.
Kuna kipande cha video kimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, kikimwonesha Chidi katika mahojiano na chombo kimoja cha habari. Katika video hiyo, anamshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kujielekeza katika masuala ambayo yanahusu nafasi yake.
Chidi anasema Paul Makonda amekuwa akijielekeza kwa wasanii ili wamsifie na kuacha mambo yenye kuhusu cheo chake. Anabainisha kuwa mwisho, wasanii huhitaji wapewe pesa. Akishafeli kwa wasanii, watu watampima kwa yale atakayokuwa ameyafanya kama mkuu wa mkoa.
Akatolea mfano kushughulikia suala la wafanyabiashara wa soko la Karume, upangaji wa vitu ili watu na magari yapite vizuri, akazungumzia kuhusu hali za vituo vya polisi na magereza, kwamba Makonda anatakiwa kwenda na kuangalia wanaowekwa mahabusu na wafungwa wanaishije na wanalala vipi huko?
Chidi alisema mazingira ya magereza yanatakiwa kuboreshwa kwa sababu hali ni mbaya. Alifafanua kuwa watu hujisahau, lakini yeye ameshalala mahabusu na waliokuwa mawaziri, kwa hiyo jela anaweza kwenda yeyote, akiwemo Makonda.
Ni hoja ya bungeni
Alichokizungumza Chidi ni hoja nzito ya bungeni. Amezungumza kwa lugha rahisi yenye kueleweka kwa kila mtu. Kwamba watu hujisahau kuwa jela anaweza kwenda yeyote.
Mtaani kuna msemo kuwa wanaokwenda jela siyo wote wana hatia. Wengi tu wanabambikiwa kesi. Hii imekuwa lawama kwa mahakimu na majaji kuwa miongoni mwao hawatendi haki. Fikiria asiye na kosa, amesingiziwa kisha anakwenda kukutana na mateso saa 24 maisha yake yote.
Hili linapaswa kueleweka; katika nchi huru, watu kwenda jela haitakiwi liwe jambo la kufurahia. Isipokuwa ni uamuzi wenye kuchukuliwa kwa hisia kali ili kuwanyima uhuru wale ambao wanahatarisha uhuru wa wengine. Ile adhabu ya kuwanyima uhuru ni tosha sana. Uhuru ni hitaji la msingi kwa kila binadamu. Hivyo, kwa yeyote mwenye akili timamu, anapofungwa hujutia makosa yake na kufunguka kifikra kwamba anahitaji kuwa raia mwema.
Hata hivyo, Uamuzi wa kupeleka watu jela unatakiwa kufanana na ule wa mzazi anapomwadhibu mtoto wake pendwa. Unakuta mzazi anadondosha chozi lakini hana namna, anatakiwa kufanya jambo ili mwanaye awe mtu bora.
Bunge kama chombo cha uwakilishi, kinapaswa kushughulikia kero za magereza. Watu hawawezi kulala kama wapo kwenye nyumba zao, lakini hawapaswi kulazwa kama mahindi ghalani.
Jela hukutanisha watu wa hovyo kabisa na wengine ni wazuri kuliko waliobaki mitaani. Inatakiwa wale wazuri walindwe na ikiwezekana wao ndiyo wafanye ‘maambukizi’ ya kitabia kwa wengine. Haitakiwi jela liwe eneo ambalo watu wa hovyo wanakuwa na mamlaka ya kuwadhuru wengine na hata kuwafanyia vitendo visivyo vya kibinadamu.
Kuna hili lisipuuzwe
Februari 8 mwaka huu, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi aliipinga hoja ya kuwakutanisha wafungwa na wapenzi wao kwa ajili ya tendo la ndoa, akisema kitendo hicho cha kijamii siyo cha lazima.
Wafungwa kutembelewa faragha na wenzi wao ilipitishwa kwenye nchi nyingi ili kusaidia kulinda ndoa za wafungwa na kuziwezesha familia zao kisaikolojia kuona bado wapo pamoja kipindi chote cha ufungwa hadi wanapoachiwa huru.
Inatakiwa magereza yawe na vyumba maalumu kwa wafungwa wanandoa kukutana kama nchi nyingi zinavyofanya au mfungwa kupewa likizo kwenda nyumbani kukutana na mkewe kama Urusi inavyofanya. Uamuzi wa kujenga mazingira bora gerezani unatakiwa uzingatie kuwa jela si jehanamu. Wanaokwenda kule ni utaratibu wa kikatiba kuwa wakosefu waende wakajifunze na kujutia makosa yao kukosa uhuru. Izingatiwe kuwa jela si mahali pa kukomoana, kwani anaweza kwenda yeyote.
Tuzidi kupaza sauti, huyu hayawani Makonda amefanya uovu mara 50 ya ule wa Ole Sabaya.June haitakwisha
Mbowe amekwishaingia Gerezani mara 2, kwa hiyo hakuna kipya kwa Mbowe.Atatangulia mbowe kwanza huko gerezani
😆😆😆Mbowe amekwishaingia Gerezani mara 2, kwa hiyo hakuna kipya kwa Mbowe.
Mwambie tu Makonda, ule msambwanda utamfanya aishi maisha powa Gerezani asiogope
Kumekucha !![emoji23][emoji23]
Daaah !!Mbowe amekwishaingia Gerezani mara 2, kwa hiyo hakuna kipya kwa Mbowe.
Mwambie tu Makonda, ule msambwanda utamfanya aishi maisha powa Gerezani asiogope
Halafu ikawaje ?nasikia mbowe kashamtayarishia tundu lisu selo ya kukaa segerea siku akirudi bongo
Aisee ...Ni swala la muda tu kabla maneno hayo hatajatimia.
Wanaona raha kuweka wapinzani ndani ila hawajui kuwa kuna siku na wao wataingia humo.
Aisee ...Hakika nami nimejifunza nimebadili mtazamo wangu, nilidhani ameharibika kiasi hicho wanachosema kumbe la. " ....Aboreshe kule Segerea, Watu wamebanana wanalala wengi, kule tunalala na Mawaziri, kuna mawaziri kule. Watu wanajisahau kwamba hata Magufuli akimaliza muda wake anaweza akaenda kama ana matatizo ni bora uboreshe kama unajua sio kila unachofanya ni jema" - Chid Benz
very.. TrueMungu sometime hua anatumia hata punda au mawe kusema kama watumishi viongozi wa dini wakikaa kimya