Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi

Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi

Wewe upo nchi nyingine sio Tz ninayoijua, niliyozaliwa na kukulia, kama Masaki unapaita kijijini kweli? au ni mhamiaji nini hauvijui vijiji vya Tanzania jinsi vilivyo.
Kwanini kusiwe kijijini ikiwa babu na bibi yake wanakaa hapo ni ruksa kutambulika kama kijijini kwao hilo halina ubishi kijijini sio lazima iwe mbwinde shehe wangu we kubaliana nae yupo sawa
 
Kwanini kusiwe kijijini ikiwa babu na bibi yake wanakaa hapo ni ruksa kutambulika kama kijijini kwao hilo halina ubishi kijijini sio lazima iwe mbwinde shehe wangu we kubaliana nae yupo sawa

Bado nasisitiza labda atakuwa ni ukoo uliohamia Tz na wakapata citizenship by registration maana hata wenye asili ya hapa Mzizima waliokuwa wanaishi pale maeneo ya Kariakoo walisogea vijiji vya ndani kuanzia na pwani
 
teh teh teh
Mkuu wagonjwa wote hubembelezwa ili wawahi kupona aisee.

Hali aliyofikia ni mbaya sana, ukimpeleka puta anaweza kufa yule.
Mjinga tu yule kuna mambo kibao ya maana kudiscuss humu mkuu ray c kitu gani bwana si anajifanya nyoka?watu tunapigika na maisha yeye anachezea anatafuta kiki2 mbuzi huyo
 
Bado nasisitiza labda atakuwa ni ukoo uliohamia Tz na wakapata citizenship by registration maana hata wenye asili ya hapa Mzizima waliokuwa wanaishi pale maeneo ya Kariakoo walisogea vijiji vya ndani kuanzia na pwani

Mkuu kuna Kijiji kinaitwa Masaki.
Ukifika Chanika ulizia magari yanayoenda Masaki. Au anzia Buguruni
 
Ni rahisi kuongea yanayomsibu huyo binti kwa kuwa kati yetu hakuna aliyewahi kuwa kwenye hali kama aliyonayo huyo binti.....ni kipindi kimoja kigumu sana kwenye maisha ya mwanadamu......kumbukeni ni mpambano kati ya uhai na kifo..........

Kila mmoja wetu humu ndani ana uraibu wake ambao kwa namna moja au nyingine ameshindwana nao na akaamua kuendelea.....wengine ni ngono na wengine pombe bila ya kusahau wengine ni kwenye mambo ya ajabu ambayo hayafai hata kuandika humu..... Bahati mbaya kwa dada yetu ni kuangukia kwenye uraibu ambao ni kama taa kwenye giza.....

Nina uhakika kuwa huyu binti anajaribu kwa kadri ya uwezo wake kujiweka mbali na hivyo kuliko mtu mwengine yoyote isipokuwa tu matamanio yake yanashindwa na jitihada zake juu ya jambo hilo zito......ni jambo zito kuliko hata watu wanavyolichukulia kiwepesi kwa kuwa nilishawashuhudia jamaa zangu wa karibu wakipitia hali kama hiyo na wengine kujimaliza hasira na stress za mpambano huo.....

Kama alivyosema ndugu yetu hapo juu ni kumuombea tu pamoja na jitihada zake ili aweze kuishinda vita hii ngumu iliyo mbele yake........ni jambo lenye kuhuzunisha kwa binti kama huyo ambaye alikuwa anafahamika kwa umahiri wake wa kutoa burudani kwa mtindo wake maarufu wa kiuno bila ya mfupa....lakini leo hii anadhalilika......kwa kweli ni jambo lenye kuhuzunisha kama sio kufedhehesha kwa kila mwenye roho ya kiubinadamu ndani yake.......

TUMUOMBEEE NA SIO KUMLAANI NA KUMLAUMU.......
 
Hivi kuna teja yeyote aliyefikia hatua kama ya Ray C amewahi kuacha unga akiwa hai?

Nchi ambazo kupata Methadone ni kazi kuliko kupata Cocaine siyo rahisi kuwaokoa waliofikia hatua ya Ray C.
 
Nadhani huelewi maana halisi ya 'addiction'. Mtu ambaye yupo addicted hayo mawazo kama yako inakuwa magumu kuyapata. Anaweza akawa ana nia lakini nia pekee itafeli. Hawa watu wanahitaji msaada ili watoke kwenye mtego wa addiction. Wanahitaji uangalizi wa hali ya juu, mwenyewe hawezi.
Na njia kuu ya kuwasaidia watu kama Ray C na mateja wengine ni kupambana na wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya pamoja na wasambazaji wao.
I think hio ni long term, ila mpango wa muda mfupi ni upi?
 
Bado nasisitiza labda atakuwa ni ukoo uliohamia Tz na wakapata citizenship by registration maana hata wenye asili ya hapa Mzizima waliokuwa wanaishi pale maeneo ya Kariakoo walisogea vijiji vya ndani kuanzia na pwani
Ila mana nyengine ya kijijini ni kwa babu na bibi kwa hiyo kama wapo hapo masaki kuna tatizo kwake yeye kusema anakaa kijijini muelewe tu yupo sawa ila mimi babu yupo shinyanga
 
wanamtandao?? kwamba tunakula naye unga? nisisaidie wanaolala njaa nisaidie mwenye hela ya unga? wacha pesa imuue.
 
Back
Top Bottom