Msanii Roma Mkatoliki amevuka mstari mwekundu lakini anachekewa tu!

mstari mwekundu huo umechorwa wapi?
 
Hakuna haja ya kurudisha maisha ya kishamba na ya hovyo kama ilivyokuwa wakati wa Mwendazake. RomaMkatoliki hajakosea kitu zaidi ya kutumia uhuru wake wa maoni unaotambuliwa na Katiba ya JMT.


Na kumvumilia RomaMkatoliki ndiyo ukomavu wa demokrasia. Tukubali kutokubaliana lakini lazima tuseme.
 
Peleka umagulification chato, Sasa nchi imefunguliwa ni huru na Kila mmoja yupo huru.
 
Duh! Watu wenye akili kama zako Kumbe wako bado duniani
Mind set ya mwafika itachukua miaka mingi kuwa huru

Imancipate yourself from metal slavery non but yourself can free your minf
 
Tujadili vigezo Gani vimetumika kumweka pale wizara ya tamisemi mtoto wa Mzee yule kabla hatujamjadili Rm.
 

Hivi huko "Msoga" alikokutaja Roma na mwenzake Abel ktk wimbo wao ni wapi eti?

Ni ile Msoga ya Bagamoyo - Pwani nyumbani Kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete au ni Msoga ipi?

Kama ni kule kwa Kikwete, kwani huko anaishi Jakaya Kikwete pekee yake maana kwenye wimbo Roma ameitaja Msoga tu lakini hajamtaja Jakaya Kikwete ila wewe ktk andiko lako ndo umeingiza jina la Jakaya Kikwete...

Wewe ndo unastahili kupigwa pini. Wimbo hauna tatizo lolote. Hakuna sheria yoyote iliyovunjwa. Tatizo liko kwenye kichwa na akili zako..
 
Jiongeze
 
Hakuna nchi duniani inayoweza kuvumilia ukosoaji wa matusi kwa rais wake....haipo....

Tusijidanganye na iitwayo DEMOKRASIA ya ulaya kuwa kwa kiwango hichohicho cha kwao basi imeenea kwetu na tunaweza kuibeba 100p kama wao.....

Si lazima tafsiri ya DEMOKRASIA ya nchi za magharibi iweze kutekelezwa na kila nchi duniani....hapana huu ni uongo....

DEMOKRASIA ya magharibi inaendana na maisha yao ,TAMADUNI ,hulka ,mitazamo na vingi tu ambayo binadamu hatuwezi KUFANANA hata kidogo.....

Afrika ina TAMADUNI na maadili yake ambayo MATUSI haswa kwa waliotuzidi umri na walio viongozi wetu HAYARUHUSIWI/HAYAKUBALIKI hata chembe......

Huwezi kumdhalilisha rais namna vile alivyofanya.......

#SiempreJMT[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
🤣🤣🤣Muacheni kijana wa watu.
Kaongea ukweli hadi unauma
 
January , Nape , Mafuru , Kagasheki , Bade , Mchechu , mbalawa , Kinana , Mtemvu , Kairuki na kila unayemjua wa JK karudi ulingoni , kwamba Mama na JK wana maono yanayofanana ?

Hawa uliowataja ni watu wenye akili na uelewa mkubwa wa kuendesha mambo kisasa. Kuwaacha nje ni kutotumia rasolimali watu za Nchi ipasavyo. Kwamba wamerudi ni habari njema. Nchi itaendelea kwa haraka!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Muacheni kijana wa watu.
Kaongea ukweli hadi unauma
Ukweli kumdhihaki ,kumkedi na kumweka msambweni mh.Rais SSH kwa kumwita "mwendeshwa akili"?!!!

Huyu Ibra anadharau sana...
Huyu mpare wa Tanga ni mkorofi sana....ametuumiza sana kumtukana mama yake na mama yetu sote daaaah

#SiempreJMT[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…