Uchaguzi 2020 Msanii T.I.D aitaka CHADEMA imlipe kwa kutumia neno "Ni Yeyee" kwenye kampeni zao

Mbona na mie nimeanza kusema "ni yeye" toka nimezaliwa na kuanza kuongea [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na mimi nilipwe
 
Mpuuzi, hapo sasa kuna ubunifu gani?
Bangi mbaya sana,mbona uchaguzie uliopita Banki ya CRDB hawakusema neno,pale Chadema na Lowasa walipo sema Ulipo tupo.
 
Kwani hili neno si kiswahili?sasa toka lini amekua akimiliki kiswahili?njaa mbaya sana
 
Ni neno la kawaida ndio kwani diamond platnumz sio jina la kawaida ya kaisali mpeni kaisali TID ndo amelifanya ilo neno kuvuma kwakipindi hiki na kwasababu yeye ni msanii imekuwa rahisi kupenya kwa watu..
 
..CDM waondoe hayo maneno.

..hakuna haja ya kuhangaishana na huyo msanii.
 
You have to patent your product, most of us know nothing about the importance of patenting our products
 
Huyu namfahamu kabla sijabalehe,nabalehe,naanza kupiga rungu,naoa,napata watoto,nazeeka sasa yeye bado tu kabaki vile vile.

Hopeless..
 
Ni neno la kawaida ndio kwani diamond platnumz sio jina la kawaida ya kaisali mpeni kaisali TID ndo amelifanya ilo neno kuvuma kwakipindi hiki na kwasababu yeye ni msanii imekuwa rahisi kupenya kwa watu..
Wewe acha hizo.Hilo Ni Yeye ni maneno mawili yakiswahili yanayotumika kwenye jamii kwa matumizi ya kawaida na hayana uhusiano wowote na jina au nembo yoyote.Na isitoshe uyo jamaa kazaliwa kakikuta kiswahili kilishakuwepo na hayo maneno sasa hapo katunga au kabuni nini.na aliyetunga hayo maneno naye asemeje.Yeye mwenyewe katumia maneno ya kiswahili mangapi kwenye nyimbo zake, je kuna yeyote aliyemsumbua.Aya yeye anajiita Top in Dar, je ilo neno Dar ni yeye ndo alilibuni au alilikuta tu kwenye jamii.Achana na neno Dar kuna nyimbo yake inaitwa Zeze, je ilo neno ni yeye ndo alilibuni au alilikuta tu, na alilitumia hilo neno kibiashara nani alikuja kumsema.Haki miliki haiko ivyo aise.
 
amesajili?
 
Hawana huruma kabisa,

Kazi za watu wanazifanya ni zao,

Chama cha kukopi tu na kupesti.

Magwanda wamekopi.

Peoples Power wamekopi.

Kila kitu wamekopi hawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…