Wimbo.. KAIZARI by VITALI MAEMBE
Baadhi ya mistari.
Hatukulima Nafaka tu, tulipanda pia miti,
Kama urithi Wetu tunaoiachia Dunia.
Hatukufuga Nyuki tu, Tulifuga Hadi Kuku.
supu tukaifaidi Asubhi na Usiku.
Tuwe makini na watawala, Maana hao tuliowapa dhamana ya Usalama Wetu wanatafuta urafiki Kwa Kaizari.
Watawala wa siku hizi, Wanatuuzia Vitanda na kutunyima Usingizi.
Umeingia moto umeunguza misitu,
Umeingia utitiri Umefanya Ukatili,
Umemaliza Makoo, Haukuacha
Majogoo..
Kaizari tumempa Yake na yetu
Anaipora......
Kaizari Kachukua yake na yetu
Anaichukua....
Kufumba na kufumbua Akabaki mmoja Kuku, Basi nasi tukaamua Tumpike Tuuze supu.
Tukainjika Sufuria, Vipande tukavikatia,
Mmoja tukamwachia Supu anaichochea
Pembeni tukasogea Supu tunaisubiria.
Mara kaja analia ati limetoboka Sufuria,
Nyama zimevuja, mchuzi umebakia .... CHANGA LA MACHO.
Kaizari tumempa Yake na yetu
Anaipora......
Kaizari Kachukua yake na yetu
Anaichukua....
Kodi, Nauli, Ada,Bili,Rushwa,Misosi,Tiba,Faini,Tozo,
Tozo,Tozo,Tozo.
Naona TOZO Ndo zimwakera Sana maana Jamaa Tozo kairudia Sana.