Msanii Vitalis Maembe anadaiwa kukamatwa kwa tuhuma za “kuimba nyimbo za kuitukana Serikali”

Msanii Vitalis Maembe anadaiwa kukamatwa kwa tuhuma za “kuimba nyimbo za kuitukana Serikali”

TAARIFA![emoji3544]

NIMEPOKEA SIMU SASA HIVI KUWA MWANAMUZIKI NA MWANAHARAKATI, KAKA YETU VITALI MAEMBE (Namba yake⁩) AMEKAMATWA NA POLISI JUMANNE JIONI WIKI HII

WALIMUITA KITUO CHA POLISI BAGAMOYO DUNDA AKARIPOTI.

ALIPOENDA JIONI HII NA KUFIKA PALE WAKAMUWEKA NDANI..

WATU WALIOKARIBU WAKAENDA KUFUATILIA WAKAAMBIWA KUWA IMEAGIZWA TOKA JUU AKAMATWE KWA KUWA AMETUKANA SERIKALI KWENYE NYIMBO ZAKE.

SASA WAMEMCHUKUA KWA GARI YA POLISI NA INASEMEKANA WAMEENDA NAYE KIBAHA.

KAMA JUKWAA NAAMINI TUNAWEZA KUFANYA JAMBO. PAAZENI SAUTI ZENU.

Asante
Maagizo kutoka juu...hahahaha...Free Sabaya
 
Kwa Maembe kuna namna mtu kajichanganya kumkamata huyu mzee wa guitar
 
Majuzi nilikua nafuatilia intavyuu ya XXL na mtendaji mkuu wa wizara ya michezo. Bibafsi nilishangaa mdodoswaji ndio anaamua ajibu kipi na aache kipi bila kubanwa. Viva maembe
 
Binafsi niko very comfortable na mama kuliko nchi ilipokuwa mikononi mwa shetani malaika wa kuzimu.

Issue ya Mbowe Director ni malaika wa kuzimu huyu mama hajainjinia hii kitu ingawa kuna taarifa walimdanganya kwa malengo yao.

Huwezi kufanya comparison kati ya mama na yule malaika wa kuzimu, mama she's far better.
Hyo ni kweli, Mbowe alifunwa na mwendakuzimu, nenda mahakamani kathibitishe huo uongo aliodanganywa mama.
 
Maza alishasema yeye na yule dhalim aliyeko jehanam ni kitu kimoja
 
Kwamba anakuja kutuambia
Sufuria imetoboka.
Nyama zimevuja,,, mchuzi ndio umebakia
.

Hehehe changa la macho
 
VITALI MAEMBE HAS BEEN DETAINED AT KIBAHA POLICE STATION

Today November 02, 2021 Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) received information that a seasoned human rights artist in Tanzania Vitali Maembe has been arrested and detained at Bagamoyo Police station, coast region on unrevealed allegations.

Human Rights advocates under THRDC's instructions went at the Police station and were informed that he has been transferred to Kibaha Police Station for further investigation. THRDC will keep you posted on more details about his arrest.

Issued by
Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)
November 02, 2021
Bagamoyo, Coast region

============ UPDATE=========
Mpaka uzi huu unapandishwa hewani, bado haijajulikana anashikiliwa kituo gani hapo Kibaha.



Juhudi zimefanyika kufahamu alipo lakini hajafikishwa kituo kikuu cha Kibaha. Shiirika la THRDC wanafuatilia kwa kina suala hili ili kutoa msaada wa kisheria

Najaribu kupandisha wimbo uliopelekea kukamatwa kwake
20211103_094350.jpg
 
Wimbo.. KAIZARI by VITALI MAEMBE

Baadhi ya mistari.

Hatukulima Nafaka tu, tulipanda pia miti,
Kama urithi Wetu tunaoiachia Dunia.
Hatukufuga Nyuki tu, Tulifuga Hadi Kuku.
supu tukaifaidi Asubhi na Usiku.

Tuwe makini na watawala, Maana hao tuliowapa dhamana ya Usalama Wetu wanatafuta urafiki Kwa Kaizari.
Watawala wa siku hizi, Wanatuuzia Vitanda na kutunyima Usingizi.

Umeingia moto umeunguza misitu,
Umeingia utitiri Umefanya Ukatili,
Umemaliza Makoo, Haukuacha
Majogoo..

Kaizari tumempa Yake na yetu
Anaipora......
Kaizari Kachukua yake na yetu
Anaichukua....

Kufumba na kufumbua Akabaki mmoja Kuku, Basi nasi tukaamua Tumpike Tuuze supu.
Tukainjika Sufuria, Vipande tukavikatia,
Mmoja tukamwachia Supu anaichochea
Pembeni tukasogea Supu tunaisubiria.

Mara kaja analia ati limetoboka Sufuria,
Nyama zimevuja, mchuzi umebakia .... CHANGA LA MACHO.

Kaizari tumempa Yake na yetu
Anaipora......
Kaizari Kachukua yake na yetu
Anaichukua....

Kodi, Nauli, Ada,Bili,Rushwa,Misosi,Tiba,Faini,Tozo,
Tozo,Tozo,Tozo.

Naona TOZO Ndo zimwakera Sana maana Jamaa Tozo kairudia Sana.
 
Back
Top Bottom