Matibabu ni zaidi ya Starehe mkuu, usiseme hivyo kabisa. Kumbuka kwenye Starehe unatumia wakati huo huo unaingiza. Unapopata maradhi huingizi kitu bali unatoa tu.
Hata wewe ukiumwa kufikia mwezi 1 tu maisha yako yanabadilika.
Tumemuona hapa Prof Jay, kama sio huruma ya Mama Samia ilikuwa anarudisha jezi mapema sana, alikosa pesa za matibabu ya uhakika na watu walichanga lkn mpka pale Rais alipotoa tangazo la kumgharamikia.
Ugonjwa sio starehe ndugu yangu. Usitukane watu wala kukashifu kisa amefariki na hakuwa na hela za matibabu, hadi anapatwa na umauti unajua alitumia kiasi gani kwa matibabu achilia mbali huduma zingine muhimu?
Tuache Dharau, sisi ni Binadamu tu. Pumzi yako isikufanye kuwaona waliotangulia mbele za haki kama wazembe.