Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Wote tunafahamu kwamba Salum Jecha alifuta matokeo ya Urais ya 2015 baada ya Mgombea wa chama chake CCM aliyeitwa Mohamed Shein kuangushwa kwa kishindo na Gwiji Maalim Seif, huu ndio ukweli na ndivyo dunia inavyofahamu .
Salum Jecha alifuta uchaguzi ule kwa Maelekezo ya CCM, hii maana yake ni kwamba Jecha alishirikiana na ccm kufuta uchaguzi wote wa Urais kwa lengo la kuokoa chama chake baada ya Mgombea wao kuangukia pua, ikumbumbukwe kwamba Jecha ni Mwanaccm hai aliyeshiriki chaguzi za ubunge na Urais za chama hicho kama Mgombea.
Kabla ya tangazo la kufutwa kwa uchaguzi wa 2015 vyombo vya usalama vilisambazwa mitaani ili kukabiliana na watakaopinga , hii maana yake ni kwamba kulikuwa na ushirikiano kati ya Vyombo vya dola, CCM na Jecha, Sitaki kuamini kama Pius Msekwa alikuwa hayajui haya, kiasi cha kusema JECHA ALIFUTA UCHAGUZI PEKE YAKE, hapa amelenga kupotosha umma , hawa wazee wakiachwa kuendelea kupotosha watatuona sisi vijana wa kileo ni mabwege, nampinga vibaya sana huyu Mzee.
Ni kweli kwamba Jecha ndiye aliyetangaza kufutwa kwa uchaguzi ule kwa vile alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ule, lakini alitumwa kufanya vile na chama chake, hakuwa peke yake, Mzee Msekwa aseme ukweli ili aendelee kuheshimiwa.