Shikwambi
Shinda kwa Mbinu ( Shikwambi)
Ile ya 2020 ni cha mtoto, 2025 mtapigwa Shikwambi ambayo haijawahi kutokea na hii Itakuwa Massive landslide Victory kwa Rais Samia
Mama atashinda kabla hata ya tarehe ya uchaguzi, Ndani ya miezi kadhaa Mama ameshashawishi wahisani wengi na hata biashara za matajiri zina anza kuamka
Tuliwaeleza mwaka 2020 matumizi ya Shikwambi mkatukana hapa JF, Yaliyotokea kwenye uchaguzi mliyaona
2025 hata neno Chadema huta lisikia hapa Tanzania
Mimi mwenyewe najitokeza Front line lazima Mama ashinde.
Huoni ujenzi umeanza tena mitaani kwa kasi ya ajabu na watu sasa wanakula starehe sana
Nipo Dar hapa kwa muda toka Dodoma Hakika sasa watu wanakarabati sehemu zao za starehe kwa kasi sana na hayo ndio yanaonyesha pesa inazunguka kwa kasi sana
Tegemea matumizi ya Shikwambi zaidi 2025
Hakuna wa kukutetea maishani mwako, Jibebe na ujitetee mwenyewe, Kila mtu ana matatizo yake na ana familia yake inayomtegemea, Wewe nani tukuruhusu ukate mirija ya watu ya shibe na chakula kisa uchaguzi
Uchaguzi ni neno tu linalotumika kuonyesha kuna Demokrasia sio Tanzania tu hata baadhi ya nchi ulaya na Asia hakuna uchaguzi wa Demokrasia hata marekani wenyewe aina ya uchaguzi wao wa majimbo ni wa kidikiteta sana, Kuna majimbo yamepewa electro vote nyingi sana Marekani na mengine electro vote kiduchu sana,
Kama unategemea ushindi wa spoon feeding sahau mkuu, Utapigwa Shikwambi na hata hutaamini kama kweli akina Mama sasa wanaweza 2025 na neno Chadema hutalisikia bali litabaki kwenye kumbukumbu za kitabu cha gnesisi kuwa kilikuwa chama cha siasa Tanzania kilichojifia chenyewe kabla ya uchaguzi 2025