Msekwa kudai kwamba Salum Jecha alifuta uchaguzi wa 2015 peke yake ni Uongo

Nawapongeza wanaccm waliokutunukia sifuri yenye masikio kwenye kura za maoni
 
Kwanini kwa wakati huo walinyamaza?
Kwanini waongee muda huu?
Huu ndio unafiki wenu.
Hamna msaada katika taifa hili.
Hamzibi ufa mapema.
Mtaligharimu taifa baadae kwani watu wakiendelea kuvumilia maumivu kuna siku watalipuka ghafla.
Majibu mazuri sana haya. Eti hakutumwa na mtu!!?? Kwanini walikaa kimya baada ya Jecha kutangaza kufuta matokeo kama hawakuafiki au kama hoja haikutoka kwao?
 

..Jecha alitangaza peke yake / mwenyewe.

..lakini kuufuta uchaguzi alishirikiana na mamlaka nyingine.

..Mzee Msekwa ni muongo, na watangazaji walizubaa kumshika ktk uongo huo.
 
CHADEMA imeongelewa wapi kwenye mada?

Mbona hamna amani mkisikia CHADEMA?
Utapasuka kichwa tu Mkuu kwa hawa Mataga..! Binafsi nilishajiridhisha pasipo na shaka kabisa,tena kwa vitendo...CCM haina uwezo wa kukabiliana na CHADEMA kisiasa kwenye uchaguzi wowote ule na hata siasa za majukwaani,kama kuna uwanja sawia,bila mbinu za ziada(Chafu).CCM si lolote kwa CHADEMA.JK anafahamu mno,hata JPM( R.I.P).
Usifikiri kesi za kizushi kama hii,ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake,zinazuka tu!? Ni CCM wanapambana kabisa kutafuta manusura...
 
Mimi nilichokiona 2015 yalikuwa ni mapinduzi ya kijeshi yaliyomweka shein madarakani ila jumuiya ya kimataifa na AU na EAC wakanyamaza sijui kwanini.
Hayo hayo yalimuweka JPM( R.IP) madarakani,kwa Tanzania bara pia..TB Joshua( R.I.P),akawahi mapema kuteta na EL,kutuliza hali ya hewa.
 
Ukweli mtupu !
 
Halafu sasa kuna watu wanataka tuamini kwamba alifanya yeye kama Jecha na hakukua na msukumo?

Cc Pascal Mayalla
Mkuu Ng'wale , tunapozungumzia tukio, the realists watazungumzia kile tuu kilichoonekana, Jecha kafuta uchaguzi. Just that, the deep thinkers na the wishful thinkers wao ndio wataanza kuchimba chimba, the motivés behind, the underlying factors, the causative agents, the collaborators, etc.
Msekwa is very very right, aliyefuta uchaguzi ni Jecha pekee yake, iwe alitumwa, alishinikizwa, au ni yeye tuu mwenyewe alimua kuokoa jahazi, all that is invisible, kitu visible ni kimoja tuu, Jecha pekee yake.
P
 
..Jecha alitangaza peke yake / mwenyewe.

..lakini kuufuta uchaguzi alishirikiana na mamlaka nyingine.

..Mzee Msekwa ni muongo, na watangazaji walizubaa kumshika ktk uongo huo.
Hakuna uthibitisho wa hilo, japo tangazo lile lilikuwa batili, Jecha hakuwa na mamlaka ile, lakini baada ya kutangaza kuufuta, wote wakamkubalia na uchaguzi kufutika kweli.

Binti over 18, akibakwa na akanyamaza na kuendelea kuishi na mbakaji na akawa anabakwa repeatedly, tena na tena na tena, atahesabika ame consent.

Jecha alipotangaza kufuta uchaguzi, hakuna yeyote aliyepinga, hivyo kuhesabiwa wote wameridhia...

Hili jambo hata mimi nililizungumzia sana humu
Mwisho, heshima kitu cha bure, Msekwa aheshimiwe asiitwe muongo !.
P
P
 

..hapana.

..CUF walipinga na ndio maana hawakushiriki uchaguzi wa marudio.

..Mzee Msekwa ni muongo kwa sababu anadai Jecha alikuwa peke yake, kwamba hakupata ushirikiano wa mamlaka nyingine kufuta uchaguzi kwa ubatili.

..Hapa hatuna mfano wa Binti aliyebakwa akanyamaza. Tuna mfano wa Binti aliyebakwa, akalalamika, na watu wazima wakakataa kumsaidia.
 

Umesahau kwamba Msekwa mwenyewe ni kada mkongwe wa CCM and its predecessors? Kesi ya ngedere unampelekea nyani kuiamua?
 
Mkuu JokaKuu , there you are, na hili ndilo kosa kubwa la upinzani wa Tanzania!.

Uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, hivyo kukitokea dosari zozote, kuna utaratibu wake wa kulalamika ikiwemo kujaza fomu za malalaliko SEL 04.

1. Tangazo lile la Jecha ni batili kwasababu Jecha hana mamlaka ya kujigeuza yeye ndie ZEC, hakukuwa na malalamiko yoyote ya kutokea dosari zozote zilizoripotiwa ZEC, kujustify kuufuta uchaguzi.
2. Watu wa kwanza kulalamika, rasmi, walipaswa kuwa wale wajumbe wawili wa CUF ndani ya ZEC, kuwa uamuzi ule ni wa Jecha na sio ZEC, walikaa kimya, kuonyesha ni walikubali.
3. CUF waliitisha Press Conference kulalamika na kutoa tangazo la kususia uchaguzi wa marudio. Kulalamika huko kwenye Press sio kulalamika chochote, wala lolote, ni kupiga tuu kelele kama mwanamke anayepiga kelele wakati akifanyiwa tendo la ubakaji, na baada ya tendo kukalilika, mbakaji kamaliza kujilia na kutosheka, mwanamke huyo akanyaza kimya bila kuripoti popote, na kujiswafi na kutulia. Tena mbakaji akatoa kabisa na siku, tarehe na muda atakakuja tena kumbaka, mwanamke yule hakuripoti popote, na ilipofika ile siku ya kubakwa tena, this time mwanamke huyo alimsaulia na kumchanulia mbakaji huyo, ubakaji huo ukatunga mimba, mwanamke huyo akaendelea kunyamaza na kuishi na mbakaji yule kinyumba akirimiza majukumu yote ya nyumbani ukiwemo kutoa huduma za unyumba!. Atakesabika alibakwa?.

Scénario zote za uchaguzi wa Zanzibar ikiwemo haramu ya Jecha, nimeieleza kwenye mabandiko haya zaidi ya 10 ya uchaguzi ule...







P
 
..Jecha alitangaza peke yake / mwenyewe.

..lakini kuufuta uchaguzi alishirikiana na mamlaka nyingine.

..Mzee Msekwa ni muongo, na watangazaji walizubaa kumshika ktk uongo huo.
Mkuu, nilishangaa vijana hawakumbana

Msekwa alisema eti CUF walitakiwa kwenda mahakamani. Nilimshangaa huyu mzee na kujiuliza maswali mengi sana. Hivi ni kazi ya nani kusimamia integrity ya uchaguzi kama si Serikali.

Jecha aliondolewa kwa ulinzi, makamu wake akazuiliwa kuendelea na zoezi, serikali ikampa nafasi ZBC kufuta uchaguzi, Polisi hawakuhoji bali walipiga watu. Msekwa hakuyaona yote hayo

Msekwa alidanganya suala la watu 19 Bungeni akisema barua ya Spika inajieleza
Akadanganya kuhusu katiba, kwamba haihitajiki. Mbona alitoa maoni kwa Tume ya Warioba

Haya ni madhara ya 'hongo' ya mafao ya kustaafu! inakera inaudhi sana!

Tuna mzee mmoja tu anaitwa J.S Warioba
 
Mkuu Pasco, kuna nyakati za kulaumu Wapinzani kwa udhaifu wao. Kuna nyakati za kuwaonea huruma kwa nyakati wanazopitia. Nitazungumzia mazingira ya uchaguzi

Jecha hakuondoka mwenyewe, ''aliondolewa '' na waliobaki walikuwa 'chini ya ulinzi'.
Jecha akapewa kila fursa akisindikizwa na vyombo vya dola.

Kusema kwamba kuna Fomu ya malalamiko ni kujidanganya
TL alilamika anafuatiliwa na watu akawataja. Baada ya kumiminiwa risasi, Polisi hawafuati 'lead' wanamtafuta dereva wake. Polisi hawajui kamera zilipo, wanamtafuta dereva wa TL
Hawa ndio unawapa fomu ya malalamiko ya bosi wao ! real

Mkuu, hapa ndipo nawaona ACT-Wazalendo ni matutusa sana. Huwezi kushinda uchaguzi kwa tume huru ukiwa na mfumo uliopo.

Uchaguzi wa Jecha, tume ilikuwa huru na Wapinzani.
Tume haikuharibu uchaguzi, mfumo mzima wa vyombo vya dola ndilo lilikuwa tatizo.

Ni kwa msingi huo, kuna uwezekano wa kushinda uchaguzi ukiwa na tume ya leo lakini vyombo vya dola vikiwa huru na kusimamia majukumu yao ikiwemo Mahakama.

Hapa ndipo tunahitaji Katiba mpya ili tutengeneze vyombo huru. Hatuhitaji Tume kama ACT-Wazalendo a.k.a CUF ambao hawana kumbu kumbu ya kulichowasibu

Unaposema Wapinzani waende mahakamani, umesahau ''majaji wameagizwa waangalie mweleko wa mihimili mingine na siyo sheria peke yake''

Mhimili mwingine ukisema 'umeshinda' kuna mahakama gani itakwenda kinyume.
Maagizo ya Mahakama yametolewa na Mwalimu wako tuliyekueleza kuanzia mwanzo, namba hazielezi weledi wa dunia bali wa jambo fulani tu.

JokaKuu
 
Umeandika nini hiki?Mnaona fahari kuiba kura?CCM mna ugonjwa mbaya sana wa uroho wa madaraka ila hamjitambui.
Hapo ulipoharia nani atasafisha?Unataka Watanzania wafanye nini ili CCM isituibie kura?Msije kutulilia.
 
Nilimsikia pia juzi akihojiwa na kituo cha tv, naona amebadili gia angani kuhusu wabunge covid-19. Eti taarifa haijamfikia Spika, mbaya zaidi hata hiyo stori hataki izungumzwe tena.
 
Nilimsikia pia juzi akihojiwa na kituo cha tv, naona amebadili gia angani kuhusu wabunge covid-19. Eti taarifa haijamfikia Spika, mbaya zaidi hata hiyo stori hataki izungumzwe tena.
Mzee bora angejinyamazia tu
 
Mzee bora angejinyamazia tu
Mkuu, huwezi kuwa critical kama sio msafi, utakuwa unagusia mambo juu juu tu, kuna mambo ya maana huyo mzee anataka kuyasema lkn anapokumbuka anaweza kukumbushiwa ujumbe wake wa bodi ya mamlaka Ngorongoro anashuka chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…