Msemaji mkuu wa serikali ametoa tamko kupitia kwenye ukurasa wa Twitter akisema, namnukuu; "Kuna upotoshaji mkubwa kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki iliyoanza katika mwaka huu wa fedha (2022/23). Serikali imepunguza kwa kiasi kikubwa tozo hizo. Wizara ya Fedha itatoa ufafanuzi kuhusu tozo hizi na namna zilivyoleta nafuu kwa wananchi. NAOMBA TUTULIE."
-------------------
Msemaji Mkuu wa Serikali: Kuna upotoshaji mkubwa kuhusu Tozo
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa kumekuwepo na upotoshaji mkubwa kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki(tozo katika miamala ya kibenki) iliyoanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/2023, ambapo ameeleza kuwa Serikali imepunguza kiasi kikubwa kwenye tozo hizo.
Ameeleza hayo leo Agosti 22, 2022 kupitia kurasa rasmi za Msemaji Mkuu wa Serikali kwenye mitandao ya kijamii, ambapo amesema kutokana na uwepo wa upotoshaji Wizara ya Fedha itatoa ufafanuzi kuhusu tozo hizo na namna zilivyoleta nafuu kwa wananchi.
"Kuna upotoshaji mkubwa kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki iliyoanza katika mwaka huu wa fedha (2022/23). Serikali imepunguza kwa kiasi kikubwa tozo hizo. Wizara ya fedha itatoa ufafanuzi kuhusu tozo na namna zilivyoleta nafuu kwa wananchi. Naomba tutulie."- amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
Kumekuwepo na mijadala kwenye mtandao ya kijamii pamoja na kwenye vyombo vingine vya habari ikiwemo magazeti kuhusu tozo mpya kwenye miamala ya huduma za kibenki, huku baadhi ya wadau wakikosoa suala hilo na kudai kuwa linaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.
Itakumbukwa Serikali kupitia Waziri wa fedha, Dkt.Mwigullu Nchemba ilitangaza kupitia Gazeti la Serikali Na 478V kuanza kwa utekelezaji wa tozo ya miamala ya fedha kupitia benki.