Msemaji Mkuu wa Serikali kuzungumza na Waandishi wa Habari jioni hii.

Msemaji Mkuu wa Serikali kuzungumza na Waandishi wa Habari jioni hii.

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Msemaji mkuu wa serikali atazungumza na waandishi wa habari jioni hii,ambapo atakuwa live au mbashara kupitia vyombo vyote vya habari hapa Nchini yaani vile vya serikali na vile vya binafsi vitarushaa matangazo hayo na mkutano huo na waandishi wa habari muda wa saa kumi na mbili jioni hii kuongea na umma wa watanzania.

Lengo la mkutano huo ni kuelezea maazimio yaliyofikiwa kati ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kasimu Majaliwa pamoja na viongozi wa jumuiya ya wafanya biashara Tanzania.

Usikose kufuatilia mkutano huu ili kuweza kujuwa nini kimeafikiwa kati ya serikali na jumuiya ya wafanyabiashara Nchini.tega sikio lako na nawa macho yako na usisubiri kuhadithiwa
Screenshot_20240627-185119_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Tutashukuru km maombi ya wafanya biashara wameyasikia na kuyafanyia kazi ila kama watasema watayafanyia kazi mgomo uko palepale.
 
Tutashukuru km maombi ya wafanya biashara wameyasikia na kuyafanyia kazi ila kama watasema watayafanyia kazi mgomo uko palepale.
Kaa kwa kutulia tega masikio yako na kuwa karibu na Tv yako kama unayo uweze kusikiliza maazimio yaliyofikiwa kati ya serikali na jumuiya ya wafanyabiashara Nchini. Tanzania utamaduni wetu ni kumaliza mambo yetu mezani kwa njia ya mazungumzo na majadiliano ya amani na maridhiano.
 
Tanzania imebadilika siku hizi ina maamuzi ya kistaarabu sio kama zamani kichapo/kipigo kifo tu.
 
Kwanini ameweka upara wake hapo. Post ya kiofisi haipaswi kuwa na picha ya mtu unless ni Rais,PM au W mkuu
 
Kwanini ameweka upara wake hapo. Post ya kiofisi haipaswi kuwa na picha ya mtu unless ni Rais,PM au W mkuu
Anataka kutudanganya yafuatayo.
1. Bandari haijauzwa.
2. KIA haijauzwa
3. NCAA haijauzwa
4. Misitu haijauzwa
5. Ardhi ya Tanganyika haijauzwa.
6. Bahari haijauzwa
7. Madini adimu hayajauzwa.
 
Kasimu Majaliwa ni useless ameunda KAMATI 156686434587654 hakuna hata moja iliyoleta majibu
 
Back
Top Bottom