Msemaji Mkuu wa Serikali: Rais ametoa UHURU wa KUJIELEZA lakini hajaruhusu watu walete mtafaruku na mgongano kwenye nchini

Msemaji Mkuu wa Serikali: Rais ametoa UHURU wa KUJIELEZA lakini hajaruhusu watu walete mtafaruku na mgongano kwenye nchini

Kwani katiba inasemaje kuhusu uhuru wa kujieleza?
Pia mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka bandari yetu tu.
Asante
 
Hata sisi wananchi hatujamchagua Huyo wanayedai ni rais.Na hatujamtuma kuuza Mali za Tanganyika pekee na kuacha za nyumbani kwao Zanzibar wakati bandari ni jambo la muungano.
kwahyo unatakaje we mjinga. ndoo tayar ashauza unasemaje
 
Kwasababu dhalimu alikuwa anavunja katiba kwa kuzuia uhuru wa maoni, hao mabingwa wa kujipendekeza wanadhani uhuru wa maoni ni hisani ya rais.
 
Watanganyika hatuna tatizo na muwekezaji!!

Tunachotaka kujua ni;

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hiyo namba 5 kuhusu bandari za zanzibar hazimo kwa sababu tayari wamepewa makaburu
 
Kama serikali inajua kuna watu wanapitisha bure mizigo bandarini kwa nini wasiwachukulie hatua? Excuses zingine ni za kijinga.

Hebu wajibu hoja

1. Ukomo
2. Kuruhusu bandari za bara tu na siyo za Zanzibar
3. Kuwalipia eneo pindi wakilihitaji eneo lolote hata kama ni hapo Kariakoo serikali ilipe maghorofa.
4. Faida tutakayoipata

5. Tumeuza kwa shs ngapi?
6...
Hiyo namba 2 bandari za zanzibar hazimo kwa sababu tayari wamepewa makaburu
 
Gerson Msigwa ambaye ni Msemaji Mkuu wa Serikali amesema haya...

Rais ametoa uhuru wa kujieleza, kila mmoja anaweza kujieleza lakini Mheshimiwa Rais hajaruhusu watu walete mtafaruku kwenye nchi,mgongano kwenye Nchi, Sio kwamba hatujuwi wanachokifanya, bahati mbaya sana watu wameingiza maslahi yao, wanajitahidi kupotosha, tena baadhi yao tunawafahamu, ni wajuzi wa sheria, na wanajuwa wazi wanachokisema wanakipotosha...".

Uwekezaji huu wa DP WORLD kuna watu unawagusa,kuna watu hawataki Uwekezaji huu kwa sababu udhaifu huo uliopo Bandarini kwa sasa unawapa faida, watu wanapitisha mizigo bila kulipa kodi, watu hawa ndio wanapinga Uwekezaji huu kwa sababu watadhibitiwa kuiba
Angetoa mfano japo mmoja wa uwekezaji uliowahi kufanikiwa ,huu uwe wa pili ,kama bandari ameshindwa kuusimami itakuw ni hawa elite people achaeni utan jamani
 
Msigwa na Samia wote ni wajinga wanaozidisha huo wanaouita mgongano.

Samia licha ya kuruhusu watu wakosoe lakini amegoma kuwajibu, au anapojibu anatoa majibu ya dharau, hii maana yake Samia nae hajielewi, ukiruhusu watu wakosoe, kuwa tayari kuwajibu kwa staha, lakini kinyume chake utavuna unachopanda.

Msigwa ni mpuuzi kwa kusema wanaolalamikia mkataba wa bandari waliopewa waarabu milele ni wale waliokuwa wakivuna kule bandarini, kwamba hii nchi licha ya kuwa na jeshi la polisi, TAKUKURU, na mahakama, lakini hizo idara zote ni wajinga, zilizozidiwa ujanja na wajanja waliokuwa wakiiba bandarini!.
Kuna siku alisema kwa hasira ndo jibu la mwisho kulisikia kuwa eti SERIKALI HAIFANYI BIASHARA ,Ili hali upande wa pili wa dp world state own entity, halotel ni state own entity
 
Kama serikali inajua kuna watu wanapitisha bure mizigo bandarini kwa nini wasiwachukulie hatua? Excuses zingine ni za kijinga.

Hebu wajibu hoja

1. Ukomo
2. Kuruhusu bandari za bara tu na siyo za Zanzibar
3. Kuwalipia eneo pindi wakilihitaji eneo lolote hata kama ni hapo Kariakoo serikali ilipe maghorofa.
4. Faida tutakayoipata

5. Tumeuza kwa shs ngapi?
6...
Tuna riasi asiyewajbika yeye anataka kukaa ikulu akiwa amepaka hinna na vijora kwa kodi zetu ,badala ya kuwashugulikia wezi eti anajificha kwenye kivuli cha uwekezaji
 
Gerson Msigwa ambaye ni Msemaji Mkuu wa Serikali amesema haya...

Uwekezaji huu wa DP WORLD kuna watu unawagusa,kuna watu hawataki Uwekezaji huu kwa sababu udhaifu huo uliopo Bandarini kwa sasa unawapa faida, watu wanapitisha mizigo bila kulipa kodi, watu hawa ndio wanapinga Uwekezaji huu kwa sababu watadhibitiwa kuiba
Kwahio kila anayepinga ni mwizi aliyekuwa anapata Faida ?!!!

Mbona tunapeana matusi ya rejareja - Rais ameruhusu haya ? Yaani Rais ndio anaruhusu na sio Katiba inasema hivyo ?

Hawa watu wamejisahau kwamba Boss ni Mwananchi na Cheo ni Dhamana...
 
Back
Top Bottom