Msemaji Mkuu wa Serikali: Wachina wataiendesha reli ya TAZARA kwa miaka 30 ili kupunguza mzigo kwa serikali

Msemaji Mkuu wa Serikali: Wachina wataiendesha reli ya TAZARA kwa miaka 30 ili kupunguza mzigo kwa serikali

Narudia tena, ile propaganda mnayawapaga wananchi kuwa wapinzani wanataka kuchukua nchi ili wagawe raslimali kwa wageni huwa mnamaanisha nini?
Hakuna aliyegawa nchi, hapo Tanzania na China wote wanafaidika, wazungu wa magharibi wanapotaka tuwalambe miguu tunatumia rasilimali iliyojengwa miaka ya 70 katika kuingiza mapato serikali kuu.

Ni ubunifu unaokwenda sambamba na nyakati hizi.
 
Narudia tena peleka utoto mbali.
 
Nawaambia ule upuuzi wenu mnaowambia wananchi kuwa wapinzani wanatumika na wazungu ili wagawe raslimali za nchi. Sasa unafiki wenu huo hapo hadharani.
Wewe Hauna ulijualo katika vitu ambavyo Marekani ameumia hadi anakutumieni nyinyi mambumbu mfanye Fujo Ili nchi isitawalike ni pamoja huo mradi

Hiyo reli china anataka kuipeleka Hadi Zimbabwe na Botswana

Reli itakuwa bize na bandari yetu itakuwa bize ikihudumia mizigo ya Zambia. Zimbabwe na Botswana

Alafu Marekani anabaki kuwa kama Joka la kibisa katika hizo nchi
Na ndio maana hata Zambia pia Kuna mambumbu kama nyinyi mnatumiwa kufanya vurugu tena ni kama huku na kule pia zinasababishwa na TEC ya Zambia

Shida ni kwamba hi nchi tuliyosoma Cuba tupo wachache ila tutakufundisheni ikibidi hata viboko tutakuchapeni Ili muelewe
 
Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amewahakikishia Watanzania kuwa mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na China wa uboreshaji wa reli ya TAZARA utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania kiuchumi na kijamii.Msigwa aliyekuwa akitoa ufafanuzi kufuatia baadhi ya watumiaji wa mitandao kupotosha kwa kubeza hatua hiyo, amesema reli ya TAZARA ambayo ilijengwa kwa mkopo usio na riba kutoka China kati ya mwaka 1970 na 1975 na kisha mwaka 1976 kukabidhiwa kwa Tanzania na Zambia ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiuendeshaji hali iliyosababisha kukosa tija, kushindwa kujiendesha na kulazimu Serikali kutumia fedha zake kuiendesha.

Amefafanua kuwa kupitia mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na nchi ya China kupitia kampuni CCECC, China itawekeza kiasi cha dola za Marekani Bilioni 1.4 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 3 na Bilioni 450 ambazo zitaboresha miundombinu ya reli, kujenga vituo, kununua treni ya abiria na pia kujenga kituo kikubwa cha Kidatu Transshipment Joint ambacho kitawezesha mizigo kutoka reli ya kati ambayo ina kiwango cha MGR kuhamishiwa katika reli ya TAZARA ambayo ina kiwango Cape Gauge.

Amebainisha kuwa pamoja na uboreshaji huo, kampuni ya CCECC ambayo itaboresha reli kwa miaka mitatu na kuiendesha reli hiyo kwa miaka 30 itakuwa inatoa kwa Serikali dola za Marekani Milioni 30 kila mwaka (sawa na shilingi Bilioni 35) ikilinganishwa na sasa ambapo Serikali ya Tanzania pekee inalazimika kutoa shilingi zaidi ya Bilioni 28 ili kuchangia uendeshaji wa TAZARA.Kutokana na uwekezaji huo TAZARA inatarajiwa kuchochea uchumi wa Tanzania na Zambia kwa kiwango kikubwa kwa kuwa reli hiyo inaunganishwa na mtandao wa reli za kiwango cha Cape Gauge zenye urefu za zaidi ya kilometa 50 Barani Afrika.Baadhi ya manufaa ambayo Tanzania itanufaika ni pamoja na kurahisisha usafirishaji wa madini mbalimbali yakiwemo madini adimu yaliyopo Tanzania (rare earth elements, cobalt, granite, makaa ya mawe na chuma pamoja na mazao mbalimbali ya kilimo kwenda nchi za SADC na kwenda Bandari ya Dar es Salaam.

Msigwa ametoa wito kwa Watanzania kupuuza wanaobeza mafanikio ya kupata uwekezaji huo mkubwa ambao umefanikiwa baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukutana na Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kukubaliana nae kuwekeza katika uboreshaji wa TAZARA na pia Rais Samia alipokwenda kuhutubia Bunge la Zambia na kutoa wito kwa Serikali ya Zambia kukubali uboreshaji wa reli hiyo kufanyika.Tayari Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amezindua uboreshaji wa TAZARA nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji wa mradi huo.

Pia Soma: Kampuni ya China CCECC kukabidhiwa kuendesha Reli ya TAZARA kwa miaka 30

Yaani hawa watu wetu mimi nashindwa kuwaelewa. Yaani hawawezi kuendesha vitu vyote ispokuwa serikali tu. ......!!
 
Wewe Hauna ulijualo katika vitu ambavyo Marekani ameumia hadi anakutumieni nyinyi mambumbu mfanye Fujo Ili nchi isitawalike ni pamoja huo mradi

Hiyo reli china anataka kuipeleka Hadi Zimbabwe na Botswana

Reli itakuwa bize na bandari yetu itakuwa bize ikihudumia mizigo ya Zambia. Zimbabwe na Botswana

Alafu Marekani anabaki kuwa kama Joka la kibisa katika hizo nchi
Na ndio maana hata Zambia pia Kuna mambumbu kama nyinyi mnatumiwa kufanya vurugu tena ni kama huku na kule pia zinasababishwa na TEC ya Zambia

Shida ni kwamba hi nchi tuliyosoma Cuba tupo wachache ila tutakufundisheni ikibidi hata viboko tutakuchapeni Ili muelewe
Hao mawakala wa EU hawawezi kukuelewa, wanakariri maisha siku zote wakidhani kesho itakuwa sawa na jana.
 
Hili sio jambo baya kama mkataba upo vizuri na kutakuwa na usimamizi mzuri kujua kila kinachoendelea. China wanawekeza pesa ndefu 1.4bn USD. TAZARA itakuwa kwenye viwango vya kimataifa.

Muhimu kuangalia ajira zinaenda kwa wazawa sio China kujaza watu wao.
Ni kipi umeona serikal imewekeza kikawa na tija wa mtazania zaid ya kufaidi wao tu huku raia wakibebeshwa gunia la msumari ...kodi+ ushuru
 
Narudia tena, ile propaganda mnayawapaga wananchi kuwa wapinzani wanataka kuchukua nchi ili wagawe raslimali kwa wageni huwa mnamaanisha nini?
Mimi ushawahi kusikia naongelea hizo mambo, naomba risiti chap
 
Ni kipi umeona serikal imewekeza kikawa na tija wa mtazania zaid ya kufaidi wao tu huku raia wakibebeshwa gunia la msumari ...kodi+ ushuru
Yapo mengi sana, tatizo tunaiona upungufu unapojitokeza hatuoni mema yakiwa kazini.

Mwendokasi jijini Dar hauna tija yoyote?. Upanuzi wa bandari kule Tanga na hii itakayojengwa hapo Bagamoyo hazitakuwa na tija yoyote?.
 
Ni kipi umeona serikal imewekeza kikawa na tija wa mtazania zaid ya kufaidi wao tu huku raia wakibebeshwa gunia la msumari ...kodi+ ushuru

Hii Tazara ikisimamiwa vizuri itakuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa Tanzania kama kuongeza ajira,biashara, utalii nk. Sababu tutakuwa tunashirikiana na China inaweza kuwa na tija.

Copper, shaba,mizigo inayopitia bandari ya Dar tutapata kodi na fees zingine ukizingatia asilimia kubwa itakuwa inaenda China.

Mbao, Mazao kutoka Nyanda ya juu itakuwa rahisi kufika Dar na labda kwenda nje ya nchi. Hopefully gharama za usafirishaji zitapungua.

Vituo vyote inaposimama train, mzunguko wa pesa chakula, sehemu ya kulala utakuwa mkubwa na biashara kuchangamka hivyo kuongeza ajira.

Kama huduma zitakuwa nzuri, world class natumaini utalii utaongezeka.
Itasaidia kupunguza malori yanayopita barabarani. Tujipange kuisimamia vizuri.
 
Hiyo reli china anataka kuipeleka Hadi Zimbabwe na Botswana

Reli itakuwa bize na bandari yetu itakuwa bize ikihudumia mizigo ya Zambia. Zimbabwe na Botswana

Alafu Marekani anabaki kuwa kama Joka la kibisa katika hizo nchi
Na ndio maana hata Zambia pia Kuna mambumbu kama nyinyi mnatumiwa kufanya vurugu tena ni kama huku na kule pia zinasababishwa na TEC ya Zambia

Hii ni kweli China yupo serious anataka kuiunganisha Dunia kupitia plan yake ya Road and Belt Initiative.
 
Hii Tazara ikisimamiwa vizuri itakuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa Tanzania kama kuongeza ajira,biashara, utalii nk. Sababu tutakuwa tunashirikiana na China inaweza kuwa na tija.
Vya kunyonga virahisi....!!! Hawataki bughudha
 
Hii reli tungeiunga kwa Lobito Corridor/ Beunguela tungeweza kupata $30Mil mpaka 50Mil kwa mwaka sema tungepiga na kazi nyingine na uendeshaji na umiliki ungekuwa juu yetu yaani kulipa wafanyakazi na ufundi. Ila pia ile ilikuwa ni program ya Marekani na tofauti yake na China ni kwamba huwa anaingilia siasa za ndani sehumu alipowekeza tofauti ni China masuala ya siasa hayamuhusu kabisa.
 
Kwamba wachina wanatupenda sana ama??Wao wanapata ninj mbona hasemi??Kitu kinakarabatiwa miaka 3, then wanatumia miaka 30...duuh..
Bora wangesema wanakarabati miaka 3, wanaendesha miaka 10,huku wakitumia wazawa kwenye kila operation, uendeshaji etc...ili kupata uzoefu, then wanaturudishia
 
Back
Top Bottom