Msemaji Mkuu wa Serikali: Wachina wataiendesha reli ya TAZARA kwa miaka 30 ili kupunguza mzigo kwa serikali

Msemaji Mkuu wa Serikali: Wachina wataiendesha reli ya TAZARA kwa miaka 30 ili kupunguza mzigo kwa serikali

Hii Tazara ikisimamiwa vizuri itakuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa Tanzania kama kuongeza ajira,biashara, utalii nk. Sababu tutakuwa tunashirikiana na China inaweza kuwa na tija.

Copper, shaba,mizigo inayopitia bandari ya Dar tutapata kodi na fees zingine ukizingatia asilimia kubwa itakuwa inaenda China.

Mbao, Mazao kutoka Nyanda ya juu itakuwa rahisi kufika Dar na labda kwenda nje ya nchi. Hopefully gharama za usafirishaji zitapungua.

Vituo vyote inaposimama train, mzunguko wa pesa chakula, sehemu ya kulala utakuwa mkubwa na biashara kuchangamka hivyo kuongeza ajira.

Kama huduma zitakuwa nzuri, world class natumaini utalii utaongezeka.
Itasaidia kupunguza malori yanayopita barabarani. Tujipange kuisimamia vizuri.
Siamin kama kuna tija cz mikataba inayopitishwa ipo sirini...hujui ni % gan sis kama taifa tutapata zaid ya waliopo huko juu kuujua ukwel na mostly hela zinaishia kwao huko..imagn UDA imeshindwa kuendeshwa na serika wkt demand ni kubwa zaid ya supply...hii serkali kuna namna haiko serious trust me
 
Kusema ukweli ni vigumu kuwa na imani na hii serikali, waziri husika na serikali nzima ya sasa. Kwao Tanganyika ni shamba la bibi.

Kama wataweka mikataba wazi inaweza kuwapa watu confidence kidogo. Labda sababu serikali tatu zinahusika, inaweza kuwa vigumu kufanya figisu. Makubaliano ya pamoja kati ya Zambia, Tanzania na China kunaweza kuwa na ufanisi na uadilifu.

Rais wa Zambia Hichlema na CEO wa Tazara huyu Mzambia Bruno Tandeo Ching'andu wanaonekana wamenyooka zaidi ya upande wetu. Ching'andu alikuwa big short General Electric kabla kwahiyo ana uzoefu wa kutosha.

Tazara itakuwa inashindana na Lobito Atlantic Railways ambayo iko backed na USA. Kwahiyo TAZARA lazima wafanye kazi kwa ufanisi wakizembea wanaweza kupoteza biashara. Sidhani kama wachina watakubali huo uzembe.

I don't know full details of these agreement but I am optimistic it will massively stimulate business activities and potentially transform that part of the country. Itachochea kwa kiwango kikubwa sana biashara, ajira, mzunguko mkubwa wa pesa kwenye vituo vyote itakapopita. Kila kitu kitahitajika Nyumba za kupanga, Guesthouses, Hotels, restaurants, usafiri, taxes, car hire, bodaboda, bajaji, kilimo kitakua kwa kiasi kikubwa upande wote ule wa utanufaika hadi Dar es Salaam.

Pia itakuwa rahisi kusafirisha bidhaa kutoka Dar to Zambia, Zambia to Dar, mikoa yote itakapopita na mikoa jirani. Nafikiri baadaye inaweza hata kuunganishwa hadi DRC.
 
Hawa wachina walijenga hii reli kwa gharama kubwa na kujitolea kwa hali na mali. Kwa pesa za leo ni zaidi ya trillion tano za Tanzania. Bàadhi walifariki katika ujenzi ule, wengine kuliwa na wanyama wakali.

Walijitolea sababu Nyerere na China walikuwa washikaji sana miaka hiyo na China haikuwa nchi tajiri. Walituma zaidi ya watu 30,000 kwenye ule ujenzi. Huu ndio ulikuwa mradi wao mkubwa nje duniani. Kwa sababu za kihistoria, urafiki, umuhimu, prestige nafikiri China ingependa kuona huu mradi unafanikiwa.

Sasa hivi China ni nchi tajiri, nchi ya kibepari. Sio tena nchi iliyokuwa karibu level moja na Tanzania. Kuna maswali inabidi tujiulize.

Wametoa masharti gani?
Watatuma wafanyakazi wangapi kutoka China?
Baada ya ujenzi watarudi kwao?
Asilimia ngapi ya ajira watapewa wazawa?
Mgawanyo wa mapato utakuwaje?
Tanzania na Zambia zitakuwa na watu wao kwenye board, management kujua kila kinachoendelea?
Kama wasipofikia malengo, kuna hatua zitachukuliwa kurekebisha au kuvunja mkataba?
Itapendeza kama wataweka mkataba wote wazi?
Akili na mawazo ya hivi CCM hawataki kabisa kuyasikia!
 
Mtanzania anachoweza ni kukata mauno,uwizi,uchawa basi

Ova
 
Mkataba gani ulishawahi kufanya mzuri na sisi kenge hadi leo wawe malaika wakufurahishe wewe hapo matopeni? Ishatoka hiyo wanakula Maisha hadi ya wanao! 30yrs yani wamejihakikishia ulaji wanakufa watoto wao Wanaendelea kukinga
Nchi za ki Africa ni za kimbwa sana, mikataba mirefu kama hiyo ilipaswa ipate ridhaa kutoka kwa wenye nchi ambao ndiyo raia, waambiwe lengo la mkataba, faida za mkataba na hasara zake, zen wao wapige kura kwamba wamekubali au kukataa ili huko mbeleni kusiwe na lawama iwayo yote, lkn kwakuwa viongozi wameamua kudharau wananchi kwa kuamini kwamba watanzania hawana akili basi sawa, acha wafanye wanavyotaka.
 
Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amewahakikishia Watanzania kuwa mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na China wa uboreshaji wa reli ya TAZARA utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania kiuchumi na kijamii.Msigwa aliyekuwa akitoa ufafanuzi kufuatia baadhi ya watumiaji wa mitandao kupotosha kwa kubeza hatua hiyo, amesema reli ya TAZARA ambayo ilijengwa kwa mkopo usio na riba kutoka China kati ya mwaka 1970 na 1975 na kisha mwaka 1976 kukabidhiwa kwa Tanzania na Zambia ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiuendeshaji hali iliyosababisha kukosa tija, kushindwa kujiendesha na kulazimu Serikali kutumia fedha zake kuiendesha.

Amefafanua kuwa kupitia mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na nchi ya China kupitia kampuni CCECC, China itawekeza kiasi cha dola za Marekani Bilioni 1.4 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 3 na Bilioni 450 ambazo zitaboresha miundombinu ya reli, kujenga vituo, kununua treni ya abiria na pia kujenga kituo kikubwa cha Kidatu Transshipment Joint ambacho kitawezesha mizigo kutoka reli ya kati ambayo ina kiwango cha MGR kuhamishiwa katika reli ya TAZARA ambayo ina kiwango Cape Gauge.

Amebainisha kuwa pamoja na uboreshaji huo, kampuni ya CCECC ambayo itaboresha reli kwa miaka mitatu na kuiendesha reli hiyo kwa miaka 30 itakuwa inatoa kwa Serikali dola za Marekani Milioni 30 kila mwaka (sawa na shilingi Bilioni 35) ikilinganishwa na sasa ambapo Serikali ya Tanzania pekee inalazimika kutoa shilingi zaidi ya Bilioni 28 ili kuchangia uendeshaji wa TAZARA.Kutokana na uwekezaji huo TAZARA inatarajiwa kuchochea uchumi wa Tanzania na Zambia kwa kiwango kikubwa kwa kuwa reli hiyo inaunganishwa na mtandao wa reli za kiwango cha Cape Gauge zenye urefu za zaidi ya kilometa 50 Barani Afrika.Baadhi ya manufaa ambayo Tanzania itanufaika ni pamoja na kurahisisha usafirishaji wa madini mbalimbali yakiwemo madini adimu yaliyopo Tanzania (rare earth elements, cobalt, granite, makaa ya mawe na chuma pamoja na mazao mbalimbali ya kilimo kwenda nchi za SADC na kwenda Bandari ya Dar es Salaam.

Msigwa ametoa wito kwa Watanzania kupuuza wanaobeza mafanikio ya kupata uwekezaji huo mkubwa ambao umefanikiwa baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukutana na Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kukubaliana nae kuwekeza katika uboreshaji wa TAZARA na pia Rais Samia alipokwenda kuhutubia Bunge la Zambia na kutoa wito kwa Serikali ya Zambia kukubali uboreshaji wa reli hiyo kufanyika.Tayari Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amezindua uboreshaji wa TAZARA nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji wa mradi huo.

Pia Soma: Kampuni ya China CCECC kukabidhiwa kuendesha Reli ya TAZARA kwa miaka 30
Tunapoenda inabidi sasa tuwe kama nchi za wenzetu. Mikataba ikiingiwa hayo manufaa ya kiuchumi inabidi yawafikie raia moja kwa moja.

Watu watoe account zao waingiziwe hela kila mwisho wa mwezi. Maana huu usenge wa kuambiana tutanufaika kiuchumi ilihali wanaopata hela ni kigenge cha wachache waliosaini hio mikataba ni upuuzi.
 
Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amewahakikishia Watanzania kuwa mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na China wa uboreshaji wa reli ya TAZARA utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania kiuchumi na kijamii.Msigwa aliyekuwa akitoa ufafanuzi kufuatia baadhi ya watumiaji wa mitandao kupotosha kwa kubeza hatua hiyo, amesema reli ya TAZARA ambayo ilijengwa kwa mkopo usio na riba kutoka China kati ya mwaka 1970 na 1975 na kisha mwaka 1976 kukabidhiwa kwa Tanzania na Zambia ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiuendeshaji hali iliyosababisha kukosa tija, kushindwa kujiendesha na kulazimu Serikali kutumia fedha zake kuiendesha.

Amefafanua kuwa kupitia mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na nchi ya China kupitia kampuni CCECC, China itawekeza kiasi cha dola za Marekani Bilioni 1.4 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 3 na Bilioni 450 ambazo zitaboresha miundombinu ya reli, kujenga vituo, kununua treni ya abiria na pia kujenga kituo kikubwa cha Kidatu Transshipment Joint ambacho kitawezesha mizigo kutoka reli ya kati ambayo ina kiwango cha MGR kuhamishiwa katika reli ya TAZARA ambayo ina kiwango Cape Gauge.

Amebainisha kuwa pamoja na uboreshaji huo, kampuni ya CCECC ambayo itaboresha reli kwa miaka mitatu na kuiendesha reli hiyo kwa miaka 30 itakuwa inatoa kwa Serikali dola za Marekani Milioni 30 kila mwaka (sawa na shilingi Bilioni 35) ikilinganishwa na sasa ambapo Serikali ya Tanzania pekee inalazimika kutoa shilingi zaidi ya Bilioni 28 ili kuchangia uendeshaji wa TAZARA.Kutokana na uwekezaji huo TAZARA inatarajiwa kuchochea uchumi wa Tanzania na Zambia kwa kiwango kikubwa kwa kuwa reli hiyo inaunganishwa na mtandao wa reli za kiwango cha Cape Gauge zenye urefu za zaidi ya kilometa 50 Barani Afrika.Baadhi ya manufaa ambayo Tanzania itanufaika ni pamoja na kurahisisha usafirishaji wa madini mbalimbali yakiwemo madini adimu yaliyopo Tanzania (rare earth elements, cobalt, granite, makaa ya mawe na chuma pamoja na mazao mbalimbali ya kilimo kwenda nchi za SADC na kwenda Bandari ya Dar es Salaam.

Msigwa ametoa wito kwa Watanzania kupuuza wanaobeza mafanikio ya kupata uwekezaji huo mkubwa ambao umefanikiwa baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukutana na Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kukubaliana nae kuwekeza katika uboreshaji wa TAZARA na pia Rais Samia alipokwenda kuhutubia Bunge la Zambia na kutoa wito kwa Serikali ya Zambia kukubali uboreshaji wa reli hiyo kufanyika.Tayari Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amezindua uboreshaji wa TAZARA nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji wa mradi huo.

Pia Soma: Kampuni ya China CCECC kukabidhiwa kuendesha Reli ya TAZARA kwa miaka 30
Aliyeturoga Waafrika angefufuka tu ili atuondolee hii laana. Hii treni nimeipanda kwa miaka mingi sana. Ujinga,wizi, uvivu, uzembe, ubadhirifu, upumbavu, upunguani, na kila aina uwendawazimu uliokuwa unafanywa na baadhi ya Watanzania na wapumbavu wenzao Wazambia; hakika unahuzunisha sana.

Yaani treni ya kisasa mnapewa bure ikiwa ina miundo mbinu yake bora kabisa! Mnashindwa kuiendesha, na mwisho wa siku wale waliowajengea wanarudi tena kuja kuiendesha kwa sheria zao! Huu ni upungasese wa hali ya juu sana.

Binafsi sitokoja kushangaa nikija kusikia siku zijazo hao wawekezaji wa Kichina wamewacharaza viboko au kuwatwanga ngumi na mateke baadhi ya wafanyakazi wenye ngozi nyeusi kutoka tu na makosa ya uzembe, uvivu, wizi, nk.
 
Kwanini tusiwarudishe na wakoloni ili kuwapunguzia mzigo?
Kwa hali hii watarudi tu. Maana Afrika imebarikiwa raslimali za kila aina. Ila kwa bahati mbaya imepewa viongozi vilaza, wabinafsi, na wasio na chembe ya uzalendo kwa nchi zao.
 
Us*ng* tu ndio umebakia huko serikalini k*manina.
 
huu muungano hautufai watanganyika tuna hujumiwa

nyerere nakulaumu sana wazanzibar wamemwagwa uku kama mchanga wanajimegea tu wanafanya watakavyo tukisema tunambiwa tunaleta udini
 
Naipongeza serikali kwa kufufua reli hii.

Hapo sasa kwakuwa lengo kuu la mwekezaji ni kubeba mizigo itakuwa faida kubwa kwa mwekezaji na serikali zote za Zambia na Tanzania.
 
Kwa hali hii watarudi tu. Maana Afrika imebarikiwa raslimali za kila aina. Ila kwa bahati mbaya imepewa viongozi vilaza, wabinafsi, na wasio na chembe ya uzalendo kwa nchi zao.
Walisharudi kwa ubia wa kuchuma tu rasilimali kuendesha serikali hawataki maana ni mzigo
 
Back
Top Bottom