Msemaji Mkuu wa Serikali: Wachina wataiendesha reli ya TAZARA kwa miaka 30 ili kupunguza mzigo kwa serikali

Msemaji Mkuu wa Serikali: Wachina wataiendesha reli ya TAZARA kwa miaka 30 ili kupunguza mzigo kwa serikali

[/QUOTE]
Ni sawa mradi huo mkataba usiwe wa manufaa kwa upande mmoja na vile vile kipengele cha kusitisha mkataba iwapo mmoja ataenda kinyume na yaliomo.

Hofu yangu Samia hawezi kusimamia chochote. Nafikiri kwa sasa hivi hii serikali ya mchongo ingesitisha kusaini mikataba yote mikubwa hadi serikali mpya halali itakapochukua nchi.

Hawana ridhaa kusaini mikataba hii mikubwa kwa niaba ya Watanganyika sababu hawajachaguliwa na wananchi.

Kwa ukweli sina imani na waziri wa uchukuzi huyu Mzanzibari Makame Mbarawa. Nafikiri huyu ndiye aliyeuza bandari kwa DP world.
 
Wauweke wazi, halafu tuone kama una tija. Mkataba usubiri kupitiwa upya na kusainiwa serikali mpya itakayochaguliwa na wananchi.

Mfano mmoja wa mkataba mzuri ni hiyo reli ya Tazara ilipojengwa back in 1970s.
Itakuwa ajabu jipya la dunia ukiwekwa wazi, unaongelea miaka ya 70 wakati wakurugenzi na wakuu wa vitengo vya nchi walikuwa waingereza? Mkoloni mweusi tangu apate madaraka haikutokea tena, utaona tu wanavimba matumbo kwa ulafi wao
 
Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewahakikishia Watanzania kuwa mkataba wa uboreshaji wa reli ya TAZARA kati ya Tanzania, Zambia na China utaleta manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa Tanzania.

Akitoa ufafanuzi kufuatia taarifa potofu zinazosambazwa mitandaoni, Bw. Msigwa amesema reli ya TAZARA, iliyojengwa kati ya mwaka 1970 na 1975 kwa mkopo usio na riba kutoka China na kukabidhiwa kwa Tanzania na Zambia mwaka 1976, imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za uendeshaji. Changamoto hizo zilisababisha reli hiyo kukosa tija, kushindwa kujiendesha kibiashara na kulazimu Serikali kuendelea kutumia fedha zake kuiendesha.

Aidha akitolea ufafanuzi taarifa hiyo amesema kuwa ni kweli wachina wataiendesha TAZARA kwa miaka 30 ili kupunguza mzigo wa kiuendeshaji kwa serikali na kupata faida zaidi.

Pia Soma: Kampuni ya China CCECC kukabidhiwa kuendesha Reli ya TAZARA kwa miaka 30
Mabeberu bado tunawapa kazi?
 
Wewe Msigwa ama huna akili ana unatumiwa vibaya sana watu wasio na akili. Yaani unakaa na kukiri kabisa Serikali imeshindwa kuendesha Kampuni kwamba imekuwa mzigo? Ninyi yaani mmeshindwa kabisa na mawazo mbadala ndio haya kuipa Kampuni ya nje?

Haya mmeipa hiyo, tueleze makubaliano yapo ndani ya hiyo miaka 30…wanaenda kupandisha faida kwa asilimia ngapi kutoka ya sasa na wao anachukua asilimia ngapi na Serikali inapata ngapi? Wekeni Mkataba hadhari….

Unasema Serikali haichukui mkopo na China imetoa kupitia hiyo Kampuni sasa huo si ndio mkopo wenyewe…hapo si lazima warudishe hela zao maana wao ndio waendeshaji…Hivi wewe Msigwa ukiangalia Watanzania unawaona ni mapoyoyo kama wewe ulivyo?

Hata hii nchi imeshawashinda ninyi tayari, haya mbona hamuwapi watu wengine waendeshe kuwasaidia mnang’ang’ania nini? Msituone wajinga na kisha kuja na ufafanuzi wa kipumbavu kwenye mambo ya maana.
 
Hili sio jambo baya kama mkataba upo vizuri na kutakuwa na usimamizi mzuri kujua kila kinachoendelea. China wanawekeza pesa ndefu 1.4bn USD. TAZARA itakuwa kwenye viwango vya kimataifa.

Muhimu kuangalia ajira zinaenda kwa wazawa sio China kujaza watu wao.
Kwani Wahindi wa Rites walivyopewa mkataba wa kuendesha TRC si tuliaminishwa kuwa Shirika lingeimarika?

Matokeo yake hawakuwekeza cho chote hadi wakatimuliwa!
 
Kwani Wahindi wa Rites walivyopewa mkataba wa kuendesha TRC si tuliaminishwa kuwa Shirika lingeimarika?

Matokeo yake hawakuwekeza cho chote hadi wakatimuliwa!
Hawa wachina walijenga hii reli kwa gharama kubwa na kujitolea kwa hali na mali. Kwa pesa za leo ni zaidi ya trillion tano za Tanzania. Bàadhi walifariki katika ujenzi ule, wengine kuliwa na wanyama wakali.

Walijitolea sababu Nyerere na China walikuwa washikaji sana miaka hiyo na China haikuwa nchi tajiri. Walituma zaidi ya watu 30,000 kwenye ule ujenzi. Huu ndio ulikuwa mradi wao mkubwa nje duniani. Kwa sababu za kihistoria, urafiki, umuhimu, prestige nafikiri China ingependa kuona huu mradi unafanikiwa.

Sasa hivi China ni nchi tajiri, nchi ya kibepari. Sio tena nchi iliyokuwa karibu level moja na Tanzania. Kuna maswali inabidi tujiulize.

Wametoa masharti gani?
Watatuma wafanyakazi wangapi kutoka China?
Baada ya ujenzi watarudi kwao?
Asilimia ngapi ya ajira watapewa wazawa?
Mgawanyo wa mapato utakuwaje?
Tanzania na Zambia zitakuwa na watu wao kwenye board, management kujua kila kinachoendelea?
Kama wasipofikia malengo, kuna hatua zitachukuliwa kurekebisha au kuvunja mkataba?
Itapendeza kama wataweka mkataba wote wazi?
 
changamoto!

Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu hata kiduchu itakusaidia, hivyo tu🙌🙌🙌
 
In my opinion, taasisi zote wapewe wageni hawa wamatumbi hawawezi kuendesha kitu. From airports, reli, tanesco, tanroads hadi IKULU. SGR yenyewe inawashinda kila siku safari zinasimama kwa sababu za kijinga jinga tu. Ukitaka kitu kife wape wabongo.
 
Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amewahakikishia Watanzania kuwa mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na China wa uboreshaji wa reli ya TAZARA utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania kiuchumi na kijamii.Msigwa aliyekuwa akitoa ufafanuzi kufuatia baadhi ya watumiaji wa mitandao kupotosha kwa kubeza hatua hiyo, amesema reli ya TAZARA ambayo ilijengwa kwa mkopo usio na riba kutoka China kati ya mwaka 1970 na 1975 na kisha mwaka 1976 kukabidhiwa kwa Tanzania na Zambia ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiuendeshaji hali iliyosababisha kukosa tija, kushindwa kujiendesha na kulazimu Serikali kutumia fedha zake kuiendesha.

Amefafanua kuwa kupitia mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na nchi ya China kupitia kampuni CCECC, China itawekeza kiasi cha dola za Marekani Bilioni 1.4 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 3 na Bilioni 450 ambazo zitaboresha miundombinu ya reli, kujenga vituo, kununua treni ya abiria na pia kujenga kituo kikubwa cha Kidatu Transshipment Joint ambacho kitawezesha mizigo kutoka reli ya kati ambayo ina kiwango cha MGR kuhamishiwa katika reli ya TAZARA ambayo ina kiwango Cape Gauge.

Amebainisha kuwa pamoja na uboreshaji huo, kampuni ya CCECC ambayo itaboresha reli kwa miaka mitatu na kuiendesha reli hiyo kwa miaka 30 itakuwa inatoa kwa Serikali dola za Marekani Milioni 30 kila mwaka (sawa na shilingi Bilioni 35) ikilinganishwa na sasa ambapo Serikali ya Tanzania pekee inalazimika kutoa shilingi zaidi ya Bilioni 28 ili kuchangia uendeshaji wa TAZARA.Kutokana na uwekezaji huo TAZARA inatarajiwa kuchochea uchumi wa Tanzania na Zambia kwa kiwango kikubwa kwa kuwa reli hiyo inaunganishwa na mtandao wa reli za kiwango cha Cape Gauge zenye urefu za zaidi ya kilometa 50 Barani Afrika.Baadhi ya manufaa ambayo Tanzania itanufaika ni pamoja na kurahisisha usafirishaji wa madini mbalimbali yakiwemo madini adimu yaliyopo Tanzania (rare earth elements, cobalt, granite, makaa ya mawe na chuma pamoja na mazao mbalimbali ya kilimo kwenda nchi za SADC na kwenda Bandari ya Dar es Salaam.

Msigwa ametoa wito kwa Watanzania kupuuza wanaobeza mafanikio ya kupata uwekezaji huo mkubwa ambao umefanikiwa baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukutana na Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kukubaliana nae kuwekeza katika uboreshaji wa TAZARA na pia Rais Samia alipokwenda kuhutubia Bunge la Zambia na kutoa wito kwa Serikali ya Zambia kukubali uboreshaji wa reli hiyo kufanyika.Tayari Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amezindua uboreshaji wa TAZARA nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji wa mradi huo.

Pia Soma: Kampuni ya China CCECC kukabidhiwa kuendesha Reli ya TAZARA kwa miaka 30
Mikopo sugu imeanzwa kulipwa kimtindo
 
Nafikiri tuwarudishe wajerumani vilevile waisimamie na kuiboresha reli ya kati kwa kuwa kumbukumbu zinaonesha ujenzi ulianza 1905 na kufikia 1914 ilikuwa imeshafika Kigoma.

Mchina alijenga TAZARA kwa malipo yasiyokuwa na riba na bado nchi mbili kwa pamoja kwa zaidi ya miaka 30 MMESHINDWA kuiboresha!
 
Aisee nchi hii imejaza madalali pimbi hawa

Sasa nyie ni mradi gani mnaweza endesha ukaleta tija?

Hapo na uhakika mmeshakula mgawo na mikataba ya ovyo na wachina!
 
Siasikiliza yote
Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amewahakikishia Watanzania kuwa mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na China wa uboreshaji wa reli ya TAZARA utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania kiuchumi na kijamii.Msigwa aliyekuwa akitoa ufafanuzi kufuatia baadhi ya watumiaji wa mitandao kupotosha kwa kubeza hatua hiyo, amesema reli ya TAZARA ambayo ilijengwa kwa mkopo usio na riba kutoka China kati ya mwaka 1970 na 1975 na kisha mwaka 1976 kukabidhiwa kwa Tanzania na Zambia ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiuendeshaji hali iliyosababisha kukosa tija, kushindwa kujiendesha na kulazimu Serikali kutumia fedha zake kuiendesha.

Amefafanua kuwa kupitia mkataba ambao Tanzania na Zambia zimeingia na nchi ya China kupitia kampuni CCECC, China itawekeza kiasi cha dola za Marekani Bilioni 1.4 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 3 na Bilioni 450 ambazo zitaboresha miundombinu ya reli, kujenga vituo, kununua treni ya abiria na pia kujenga kituo kikubwa cha Kidatu Transshipment Joint ambacho kitawezesha mizigo kutoka reli ya kati ambayo ina kiwango cha MGR kuhamishiwa katika reli ya TAZARA ambayo ina kiwango Cape Gauge.

Amebainisha kuwa pamoja na uboreshaji huo, kampuni ya CCECC ambayo itaboresha reli kwa miaka mitatu na kuiendesha reli hiyo kwa miaka 30 itakuwa inatoa kwa Serikali dola za Marekani Milioni 30 kila mwaka (sawa na shilingi Bilioni 35) ikilinganishwa na sasa ambapo Serikali ya Tanzania pekee inalazimika kutoa shilingi zaidi ya Bilioni 28 ili kuchangia uendeshaji wa TAZARA.Kutokana na uwekezaji huo TAZARA inatarajiwa kuchochea uchumi wa Tanzania na Zambia kwa kiwango kikubwa kwa kuwa reli hiyo inaunganishwa na mtandao wa reli za kiwango cha Cape Gauge zenye urefu za zaidi ya kilometa 50 Barani Afrika.Baadhi ya manufaa ambayo Tanzania itanufaika ni pamoja na kurahisisha usafirishaji wa madini mbalimbali yakiwemo madini adimu yaliyopo Tanzania (rare earth elements, cobalt, granite, makaa ya mawe na chuma pamoja na mazao mbalimbali ya kilimo kwenda nchi za SADC na kwenda Bandari ya Dar es Salaam.

Msigwa ametoa wito kwa Watanzania kupuuza wanaobeza mafanikio ya kupata uwekezaji huo mkubwa ambao umefanikiwa baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukutana na Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kukubaliana nae kuwekeza katika uboreshaji wa TAZARA na pia Rais Samia alipokwenda kuhutubia Bunge la Zambia na kutoa wito kwa Serikali ya Zambia kukubali uboreshaji wa reli hiyo kufanyika.Tayari Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amezindua uboreshaji wa TAZARA nchini Zambia ikiwa ni utekelezaji wa mradi huo.

Pia Soma: Kampuni ya China CCECC kukabidhiwa kuendesha Reli ya TAZARA kwa miaka 30
Lakini swali kwa msigwa, wachina ndio wapo tayari kuendeha huu mradi kwa hasara?
 
Nawaambia ule upuuzi wenu mnaowambia wananchi kuwa wapinzani wanatumika na wazungu ili wagawe raslimali za nchi. Sasa unafiki wenu huo hapo hadharani.
Kuna tofauti kati ya kumleta muingereza ukamkabidhi ikulu na kuingia ubia wa kibiashara ili pande zote zipate chochote.

Heche anaongea kusalimisha utendaji mzima wa serikali kwa Muingereza yaani kunakuwa hakuna tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya 1961.

Huo ni ubia wa kibiashara kuna mikataba itaandikwa kabla hawajaanza kuendesha hiyo treni hao wachina.
 
Ndugu yangu kwahiyo wewe hupendi Tazara iboreshwe?

Kama mkataba ni mzuri na sio wa kinyonyaji ni jambo zuri sana,kama tunalipa 28bl kwa uendeshaji halafu anakuja mtu anaendesha yeye halafu anatupa 30bl je shida iko wapi?
Narudia tena, ile propaganda mnayawapaga wananchi kuwa wapinzani wanataka kuchukua nchi ili wagawe raslimali kwa wageni huwa mnamaanisha nini?
 
Kuna tofauti kati ya kumleta muingereza ukamkabidhi ikulu na kuingia ubia wa kibiashara ili pande zote zipate chochote.

Heche anaongea kusalimisha utendaji mzima wa serikali kwa Muingereza yaani kunakuwa hakuna tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya 1961.

Huo ni ubia wa kibiashara kuna mikataba itaandikwa kabla hawajaanza kuendesha hiyo treni hao wachina.
Peleka utoto mbali.
 
Back
Top Bottom