Msemaji wa HAMAS: Hatamu za udhibiti wa mapigano na adui mzayuni ziko mikononi mwa wanajihadi
Magharibi mwa Ei Rose ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuzilenga kwa makombora zana za kivita za jeshi la utawala wa Kizayuni.
Baada ya hapo, al Qassam ilitangaza kuwa wapiganaji wake wamewaangamiza askari kadhaa wa Israel waliokuwemo ndani ya zana hizo. Baada ya kukamilishwa operesheni hiyo na kuwasili vikosi vya usaidizi vya utawala wa Kizayuni karibu na Ei Rose, yalizuka mapigano makali kati ya vikosi vya wazayuni na Mujahidina wa al Qassam.
Mwandishi wa habari wa Russia al-yaum ameripoti kuwa: tukio hilo lilianza kwa operesheni ya vikosi vya al Qassam ya kujipenyeza nyuma ya safu za wanajeshi wa Israel, na vikosi hivyo vya Hamas vikashambulia magari ya kivita ya Israel kwa makombora ya kuteketezea magari ya kivita.