Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

BAADHI ya wasomi nchini wamehoji uzalendo wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wa kushabikia matatizo ya nchi yake badala ya kuwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Benson Bana ameelezea kitendo cha Lissu kujitokeza mbele yalezea kwa mbwembwe suala la kuzuiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada, ni kitendo kinachozua maswali mengi juu ya uzalendo wake kwa Tanzania.

“Nilipomuona amejitokeza katika vyombo vya habari ilinishtua kwa sababu tangu mwanzo Lissu na wenzake walikuwa wanapinga ujio wa hata zile ndege mbili za mwanzo,” alieleza Profesa Bana. Alieleza kuwa mwenendo ambao Lissu ameendelea kuuonesha, unaashiria kuna walakini mkubwa katika suala la uzalendo na pia kujenga hisia kwamba inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, linalomsukuma kufanya mambo yanayoharibu maslahi ya Taifa.

Msomi huyo alisema hivi sasa kumekuwa na minong’ono mingi juu ya uzalendo wa Lissu na namna anavyosemekana kushirikiana na watu wa nje katika kuiumiza nchi. “Tuliosoma somo la Uraia tulifundishwa namna ya kuipenda nchi yako na kutumia uwezo wako kuisaidia nchi yako badala ya kuivua nguo,” alisitiza Profesa Bana huku akimfananisha mwanasiasa huyo na askari aliyoko vitani, anayeuza siri za jeshi badala ya kupambana kulisaidia jeshi lake kushinda vita.

Aidha, alieleza pia kutokufurahishwa na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACTWazalendo) cha kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kupitia akaunti ya tweeter kuhusu kutokuwasili kwa ndege ya Bombardier Q400-Dash 8, ambapo Profesa Bana ameielezea njia hiyo ya mawasiliano kama si sahihi na badala yake angeweza njia ambayo si ya kila mtu kujua.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Wakili Dk Damas Ndumbaro amemuelezea Lissu kama mtu anayetafuta umaarufu kwa njia yoyote ile hata kama njia anayoitumia itakuwa na madhara kwa maslahi ya nchi.

“Haya tunayoyaona kwa Lissu inatuonesha jinsi gani upeo wake upo kiuanaharakati zaidi kuliko uongozi na katika hili ni kama bomu linalosubiri kulipuka ambalo hata viongozi wa chama chake na hata wafuasi wake wanashindwa kuling’amua,” alieleza Dk Ndumbaro. Maneno ya Dk Ndumbaro yaliungwa mkono ya Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja ambaye alisema tatizo kubwa la Lissu ni kukosa maarifa ya uongozi.

“Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja. Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kodi ya madini, Dk Hellen Kihunsi alisema hata kama kuzuiwa kwa ndege ni suala la kisheria lakini Tundu Lissu alipaswa kutumia njia bora zaidi ya kuwasilisha kwa mamlaka husika badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

“Masuala kama haya yana maslahi kwa Taifa mbapo hata yeye (Lissu) ni sehemu ya Taifa hili, lakini kwa mwenendo ambao siku zote amekuwa akiuonesha unatilia shaka uadilifu na uzalendo wake kwa Taifa,” alieleza Dk Kihunsi. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kuchukua juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kumekuwa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wakipinga juhudi hizo, ambapo ndege mbili za awali aina ya Bombardier zilipigiwa kelele na wapinzani wakidai hazifai licha ya kwamba zimekuwa msaada mkubwa katika sekta ya usafirishaji
 
Amekwishasema wakati anachukua fomu na kupita nchi nzima kuomba kura alikuwa peke yake, hataki ushauri yeye ni sawa na dereva wa Lori hasikilizi kelele
 
Patriotism means to stand by the country. It does not mean to stand by the president or any other public official, save exactly to the degree in which he himself stands by the country. It is patriotic to support him insofar as he efficiently serves the country. It is unpatriotic not to oppose him to the exact extent that by inefficiency or otherwise he fails in his duty to stand by the country. In either event, it is unpatriotic not to tell the truth, whether about the president or anyone else.

Theodore Roosevelt
 
Huyu ndiye msaliti number moja wa mifumo kandamizi katika nchi hii, tuendelee kumuunga mkono kwa 100% wasaliti wenzie tunaotetea maslahi
179bc80083cb838f84da4cb7bf024725.jpg
ya nchi dhidi ya wale watetezi wa maslahi ya serikali, kama uzalendo wa nchi unapimwa kwa kuficha maovu ya serikali hatuna sababu ya kuwa wazalendo, tutaendelea kuwa wasaliti wa mifumo gandamizi ya serikali dhidi ya raia wa nchi hii.
#Lissu_The_Great

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hali jinsi inavyoonekana. Ninaimani katika kampain ya 2020, CCM watatupa lawama zote kwa lissu kuwa ndye aliyekwamisha uchumi wa viwanda.

Na tulivyo na akili za mipumbavu tupo tutakaopiga makofi na kushangilia.

Mark my words. 2020 sio mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Can I ask, Why?? Huoni anavyo kwamisha maendeleo yetu?? Kila kukicha anawaza namna ya kuleta ukorofi tuu ili tusiwaze hata kiwanda cha ngumi tunamuwaza yeye tu?? Akikaa nyumbani kwake itakuwaje?? Sasa, nitaishangaa hii serekali kama wakimuachia tena kesho jioni. Aende mbali kidogo labda kule Maweni Tanga akapasue mawe kwa mkono.
 
Kwa hali jinsi inavyoonekana. Ninaimani katika kampain ya 2020, CCM watatupa lawama zote kwa lissu kuwa ndye aliyekwamisha uchumi wa viwanda.

Na tulivyo na akili za mipumbavu tupo tutakaopiga makofi na kushangilia.

Mark my words. 2020 sio mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona kama washaanza vile kabla ya hata hiyo 2020.!! [emoji23][emoji28][emoji23][emoji28]
 
Can I ask, iWhy?? Huoni anavyo kwamisha maendeleo yetu?? Kila kukicha anawaza namna ya kuleta ukorofi tuu ili tusiwaze hata kiwanda cha ngumi tunamuwaza yeye tu?? Akikaa nyumbani kwake itakuwaje?? Sasa, nitaishangaa hii serekali kama wakimuachia tena kesho jioni. Aende mbali kidogo labda kule Maweni Tanga akapasue mawe kwa mkono.
Tatizo lako unadhani tupo Rwanda au North Korea ambao wananchi wana kazi moja tuu kumsifia mfalme , hata afanye ujinga al kiasi gani
Poor you
 
Can I ask, Why?? Huoni anavyo kwamisha maendeleo yetu?? Kila kukicha anawaza namna ya kuleta ukorofi tuu ili tusiwaze hata kiwanda cha ngumi tunamuwaza yeye tu?? Akikaa nyumbani kwake itakuwaje?? Sasa, nitaishangaa hii serekali kama wakimuachia tena kesho jioni. Aende mbali kidogo labda kule Maweni Tanga akapasue mawe kwa mkono.
Vipi kuhusu wale walioisababishia serikali hasara ya bilioni 90,....wafanywaje?
Ikizingatiwa serikali imeshindwa ata kuongeza mishahara kwa ajili ya ukata.
 
Viwanda vinazinduliwa kila siku nyie endeleeni kumpigia debe na kumponza LISSU.Hiyo 2020 harudi bungeni.AFE BEKI AFE KIPA.
 
Back
Top Bottom