Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Yaani makosa yafanywe na wengine halafu so mje kuwadondoshea wengine..! Oneni aibu basi kidogo jamani, angalau mkiri tu kwamba hapo mliteleza.. Lissu alichofanya ni kutusaidia tujue kwamba kumbe ndege iko bondi, kutokana na deni la fidia..
 
Kujikwamua kwenye haya maisha ya kifisadi kuna gharama zake!
 
mkuu, kama serekali inahitaji cooperation kutoka vyama vya siasa kwa nini iwanyime uhuru wao wa kikatiba?
watu (wapinzani) wamebinywa pumzi puani, sasa inabidi waitolee kule chini...wafanyeje sasa?
 
Mchakato umeingiliwa Na lissu Na umeingiliwa kisiasa. Lissu Na baadhi ya watu wa mataifa wasioipendea mema Tanzania,
Na mtatiro kaa chonjo habari tunazo
Wewe umejisajili this August kuja kutisha watu hapa? Post zako nyingi unajionyesha una mamlaka ya kuwanyima watu uhuru wao wa mawazo kinyume na JF regulations. Kaa chonjo utakula ban ya maisha, hapa sio mahali pa watu wa aina yako.
 
Tatizo haliwezi likamalizwa kwa kuwalaumu wanasiasa wanaosema ukweli na kumfumbia macho mtu aliyetufikisha mahali tulipofika,hakuna anayepinga maendeleo ya nchi yanayoletwa na Magufuli Tatizo liko kwenye mbinu anazozitumia kuleta maendeleo,kitu ambacho hakitofautiani na kuteka maji kwenye tenga ukitegemea kuwa maji yatajaa ili watu waweze kuyanywa.
 
Haya ndio tumekuwa tukiyasema kila siku....Hawa wapinzani wa nchi hii wakae wakijua hawamkomoi MAGUFULI bali wanatukomoa sisi WATANZANIA
Kigezo cha kujiunga JF kingebadiliswa na sio KUSOMA NA KUANDIKA tuu ili kulinda hadhi ya JF, hayo waachiwe kina Bashite. Sasa kama wewe hoja yako hii ina maana hata walichozungumza wengine hujakielewa?
Rudi shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…