Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

It is true.

Hilo deni wahusike nalo walilolisababisha.

Kama ni Waziri wa Ujenzi akiyekuwepo huo wakati huo wa mwaka 2010, basi alipe deni hilo kutoka mfukoni make.

Haiwezekani maamuzi ya kibabe na ya kizembe ya mtu mmoja yasabibishe tubebeshwe mzigo watanzania wote milioni 50 tulipe deni hilo la bilioni 87.

Imenenwa kwenye maandiko... Kila mtu ataubeba mzigo wake yeye mwenyewe.......
 
Baada ya kuibuliwa kwa ukurupukaji wa mh sana, naona kuna haja CCM watumie busara na uzalendo wakalipe hizo billioni 87 kutoka kwenye chama ili tuukubali uwajibikaji wao. Nawasilisha hoja wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa mkuu, waweke uwajibikaj mbele kwa maslahi ya taifa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
F


Naunga mkono hoja kwamba hilo deni walipe ccm pamoja na mwenyekiti wao,hawa ccm ndio huwa wanashangilia kila anapovunja mikataba na wankenua meno mpaka gego la mwisho

Haiwezekani tulipe madeni ya hovyo
 
Baada ya kuibuliwa kwa ukurupukaji wa mh sana, naona kuna haja CCM watumie busara na uzalendo wakalipe hizo billioni 87 kutoka kwenye chama ili tuukubali uwajibikaji wao. Nawasilisha hoja wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo TRA wanapokusanya kodi kwa ajili ya kulipa deni wakusanye kwa wana CCM tu? Au wachukuwe malipo ya wanachama wanapolipia kadi za chama ili kulipia deni? Hii ndo sababu wananchi tunashindwa kudai haki zetu kwa kufikiri serikali ya CCM ni ya wana CCM peke yao. Wote tutalipa hilo deni siyo CCM.
 
Utasikia kafukuzwa kazi kimya2
 
Mie naunga mkono hoja. Hawa MACCM wanapata ruzuku za mabilioni kila mwaka. Badala ya mzigo huu uliosababishwa na Mwenyekiti wao ulipwe na walipa kodi MACCM ndiyo walipe deni hilo na mikataba yote ambayo Taifa limepata hasara kubwa sana kama Richmond/Dowans, IPTL, Symbion ambao wahusika ni MACCM yaliyokuwa madarakani basi pesa itoke ndani ya mfuko wa MACCM badala ya hazina, labda hili likiwepo watatia akili kichwani na kuacha kukurupuka na kuingiza nchi kwenye hasara kubwa.

Wataona uchungu mkubwa kama ruzuku yao ya miaka mitano au zaidi inaenda kulipa madeni ya kukurupuka ambacho chanzo chake ni Mwenyekiti wao na hii itawafanya watie akili kichwani wa kuacha kuchagua watu ambao hawana sifa ya kuwa hata wajumbe wa nyumba kumi kumi mtaani.

Baada ya kuibuliwa kwa ukurupukaji wa mh sana, naona kuna haja CCM watumie busara na uzalendo wakalipe hizo billioni 87 kutoka kwenye chama ili tuukubali uwajibikaji wao. Nawasilisha hoja wadau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afadhali hata wamekamata hiyo ipo siku watakamata ya Rais ar kwa lift hapa!! Aibu sana tujifunze kufuata sheria......hasara kubwa kwa Taifa.......dawa deni kulipa ila sio deni la kujitakia kama hayo! Bado samaki na acacia GGM etc
Mkuu deni la meli ya samaki tunaendelea kulipa
 
F




Naunga mkono hoja kwamba hilo deni walipe ccm pamoja na mwenyekiti wao,hawa ccm ndio huwa wanashangilia kila anapovunja mikataba na wankenua meno mpaka gego la mwisho

Haiwezekani tulipe madeni ya hovyo
Tena wapambe wake wamekuwa washangiliaji wakubwa kwa kumuita Rais wetu kuwa eti ni shujaa na analinda rasilimali zetu!

Na wakati huo huo hao wapambe wanawaita wote wanaokosoa uvunjaji huo kiholela wa mikataba na usiofuata sheria kuwa wamehongwa na hao wawekezaji wa kigeni!

Ambacho wanasahau hao wapambe wa Bwana mkubwa ni kuwa sisi tunaopinga mfumo wake wa kuendesha nchi kibabe na bila kuifuata sheria tunajua madhara yake ni makubwa sana......

Lakini pia tujiulize hivi hao walioweka saini mikataba hiyo na baadaye kuivunja ni viongozi wa CCM au wa Chadema?

Sasa ni kwanini majanga yaliyosababishwa na CCM tibebeshwe mzigo huo hata wengine tusio wanaccm?

Naunga mkono hoja, zigo hili wabebeshwe wanaccm pekee........

Hili la kulipa hizi bilioni 87 ni mwanxo tu na yapo mengine mengi yanakuja......

Solution pekee ni yeye Rais atekekeze majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu na awaache wataalam na watendaji wake wahusike na mambo wanayohusika nayo badala ya yeye kuwaingilia na kutumia mtindo wake wa kufanya kazi kwa style ya ONE MAN SHOW ambao hatimaye utaliangamiza Taifa letu.
 
Of course yule madamu sijamwelewa kabisa ,yaan hajui kupanga hoja,pili kama hiyo lipoti aliandaliwa kutoka juu ina mapungufu makubwa na haipaswi kusomwa mbele ya wasomi ,hakupaswa kuingiza mambo ya kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa

Wanasahau kwamba rais hayuko juu ya sheria na katiba,sasa makampuni yanajipigia tu fidia,mtu hajajenga barabara,umemtimua,kiulaiiini analamba bilioni 87

Kimsingi rais anajitafutia migogoro kwa kutofata sheria,anavunja mikataba bila kufata taratibu,anazuia wapinzani wasifanye siasa kinyume na katiba,anakwaruzana na wawekezaji na wafanyabiashara

Anawanyima wafanyakazi increment ya mshahara kinyume na sheria

Ananyanyasa wafanyakazi kinyume na sheria

Anampa lipumba hela za CUF kinyume na sheria

Anafukuza wabunge wa CuF kinyume na sheria

Nadhani sasa mahakama ziendelee kumuandikia maandishi ukutani kwamba "utawala wake umepimwa na unaonekana hautoshi"
 
Kwani CCM inakusanya kodi...?
Nyie mmesoma somo la uraia kweli...?
Kwani waziri ni mwajiriwa wa Chama au Umma...?
Pathetic...!
Ungeniambia Katibu wa Chama Kinana kaiba hizo hapo hoja yako ingesimama....!
 
Hivi Bi Zamaradi Kawawa ameolewa!? Nampenda sana awe mke wangu.
 
Viva Lissu, wenye akili tunakuelewa sana!!
Mashetani wanaanza kukugeuzia kibao eti msaliti, wanatengeza mazingira ya kukufanyia ushetani!!

Watashindwa tu....unapambana na udhalimu Mungu yupo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii makala wapelekee Uhuru.
 


Uzi ndani ya uzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…