Msemaji wa Serikali sema ukweli kuhusu wastaafu umejitetea visivyo na kusema kitu ambacho hakipo

Msemaji wa Serikali sema ukweli kuhusu wastaafu umejitetea visivyo na kusema kitu ambacho hakipo

Natamani Rais Samia asome uzi huu na atathmini kauli yake ya kulipa pensheni watumishi kila mwezi.
 
Mkuu wako kasema ilitoka tar 22 wewe unakuja na 24 jioni sasa mnufaika kaenda tar 24 saa 2.30 usiku ATM hajakuta kitu nani muuongo kati yenu na mimi niliyeenda saa 2.30 usiku
Kifupi kuna kitu sijakielewa kwenye hoja yako.

Iko hivii? Mimi ni mstaafu(hazina) na pensheni ikiingia benki hujulishwa kwa notification.

Ilipofika Trh 24 jioni iliingia notification ya benki kunitaarifu kuwa pensheni imeingia.

Sasa kwa wastaafu (wa mifuko ya kijamii) sielewi kama nao waliingiziwa kwa muda huo ama lah.

Lolote laweza kutokea na siwezi kubishi.
 
Mkuu shkamoo
 
Natamani Rais Samia asome uzi huu na atathmini kauli yake ya kulipa pensheni watumishi kila mwezi.
Mkuu haya mambo mngeyatungia sheria thabiti wakati mlipokuwa bado kwenye utumishi wa umma. Tatizo watu wanapokuwa bado kazini hasa wakiwa kwenye nafasi mara nyingi ndo wanakuwa vinara wa kukandamiza haki za wenzao, sasa inapokuja muda wa kustaafu ndo vilio vinaanza kulaumu kila mtu aliyepo kwenye nafasi. Ni bora kuwa mvumilivu maana haya mambo tumeyapalilia wenyewe................
 
Mimi nazungumzia Mafao na Pensheni. kumbe wewe ni mstaafu unapokea Pensheni ndio ukapata notification, sasa mimi ni mstaafu wa Mwaka huu mwezi wa 2 ndio nilistaafu, sasa Pensheni na Mafao vyote hakuna hata kimoja. Nadhani swala lako la tar 24 jioni ni la kwenu ambao mna Pensheni tayari na si kwa sisi tunao subiri Maafo na Pensheni sawa rafiki tumeelewana hapo. Huenda Msemaji wa serikali alizungumzia Pensheni kwenu si kwetu. Na alisisitiza nadhani anachanganya pia maana alisema hata pensheni mwezi huu wa 9 watu wamelipwa tar 22
Kifupi kuna kitu sijakielewa kwenye hoja yako.

Iko hivii? Mimi ni mstaafu(hazina) na pensheni ikiingia benki hujulishwa kwa notification.

Ilipofika Trh 24 jioni iliingia notification ya benki kunitaarifu kuwa pensheni imeingia.

Sasa kwa wastaafu (wa mifuko ya kijamii) sielewi kama nao waliingiziwa kwa muda huo ama lah.

Lolote laweza kutokea na siwezi kubishi.
 
Niliweke wazi na vizuri, uzi huu unazungumzia walio staafu kupewa PENSHENI na MAFAO yao haijazungumzia walio tayari kwenye mfumo wa pensheni, kwa maana ya kwamba watu tumekaa miezi ya kutosha tumesha staafu hakuna pensheni wala mafao na ndio swali aliloulizwa msemajiwa serikali naona labda yeye kaja na hoja ya pensheni kwa waliopewa tayari mafao yao muda mrefu.
 
Hadi muda huu saa 4 usiku hakuna mafao yaliyowekwa benki na ofisi ya PSSSF, tupo kama wastaafu 14 hivi secta mbali mbali leo tulikutana PSSSF mkoani muda wa saa 6 leo tumeambiwa tuwe wapole na wavumilivu, ebu fikiria wenzangu walistaafu mwaka jana mwezi 11 hadi sasa wanapata tabu sana halafu msemaji wa serikali anakuja anasema wamelipa tar 22 mwezi huu wa 9 kweli. WAJIFUNZE KUMUOGOPA MUNGU
 
Back
Top Bottom