Msemaji wa Serikali: Ujenzi daraja la Wami wafikia 70.4%. Kukamilika Novemba 2022

Hadi November 2022(almost mwaka mzima) kwa hizo asilimia 30 zilizobaki? kwani lilianza kujengwa lini? duh
Zamani sana hata wao wamesahau ni mwaka gani, nadhani ni zaidi ya mitano. Ni karibu na pale lilipotumbukia lori la mama wa Morogoro lilipoopolewa likakutwa halina injini! Wajenzi wa daraja sijui wanatoka sayari gani kwani hawaonekani.
Huu ni mradi pekee ambao huwa hausemwi na serikali!
 
Vyovyote vile, ila tambueni makosa makubwa mnafanya, ni kukopa fedha halafu mnazipeleka kwenye ujenzi wa madarasa na vyooo!!!

Huko zinaenda kuzalisha nini ili kuurudisha mkopo huo bila maumivu?
 
Daraja hilo linajengwa na watu toka sayari gani? Kila nipitapo siwaoni wajenzi si mchana wala usiku na huwa siwasikii viongozi wakiwasema kuhusu kasi ya ujenzi wao!
Wachina ila fedha mtoa pesa ni serikali
 
SGR Dar Moro ilikuwa ikamilike November 2019
Waziri mkuu akasema trial runs zitaanza. August 2021.
. Hii Ni January 2022 hata la kutuambia hamna.
Haa
Treni Imebemendwa Haitembei Zaidi Ujanja Tu
 
Huo ni mradi ambao umesuswaa... Hata sijui kwanini. Ulianza 2017....mwisho ilikuwa 2018.. Sijui shida ni nini. Watu hawapo site .
 
Panaogopesha sana kupita pale pamalizike tu aisee
 
Hii ndio miradi ya kukopea fedha na sio kukopa na kujenga vyoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…