Msemaji wa Simba unaanza kuharibu

Msemaji wa Simba unaanza kuharibu

Uzi umevamiwa na wale wazee wanaochangia(ga) bila kusikiliza na kutumia akili timamu kuhukumu,wazee wa kudandia treni kwa mbele na Utopolo wenye hasira

Fikiria hawa ni JF je fb na insta itakuwaje. Guys use your common and other senses before you open your mouths.

Kwa wale watu makini mnaweza kumsikiliza hapo Semaji la Robo Fainali. Ila mashabiki mseto mnaweza kuendelea na mada huku motive yenu ikiwa ni ghazabu za kufungwa midomo
 
Duuh jamaa basickazingua.

Ule mwanga wa tochi ya mzee wala haukua na madhara kabisa ila kama sasa kaanza kutoa na hivyo vizawadi ni hatari kwa timu yake.

Wabongo wapenda sifa na umaarufu watakuja na vicochi vyenye madhara wakitegemea kutrend mitandaoni na umaarufu huo.

Hajafikiria mara 2, kaanza kua msemaji uchwara sasa.
Fact mkuu
 
Fact mkuu
Screenshot_20220405-154050_Chrome.jpg

Bila shaka hilo tochi aliloshika meneja limekupiga usoni huoni kabisa
 
Uto Mkijisikia aibu kwenye hili nigeukieni na mimi niliyeshika pumbu mwanzo mwisho kinyume na kanuni za soka ☹☹☹☹
 
Babu kazawadiwa Jezi kwa uzalendo sio lile tochi ambalo halikuwa na uwezo walau wa kufika mia 20 seuze uwanjani

Sema wa Tanzania tunaumia sana Team yako kufungwa kuliko ya Taifa au sijui usikie kuna Richmond sijui Epa sijui escrow…ila Mtu auze mechi team ifungwe utaona hasira zake

Hiyo ndo Tanzania
 
Hahah GENTAMYCINE hebu sema kitu hapa
Wapumbavu wataamini kuwa Mzee wa Tochi Abdallah Mzuzuri ni Mtu wa Kawaida tu ila waliokuwepo Uwanjani shuguli yake waliiona iliyoleta Ushindi na hiyo Tochi ni Zuga tu, ila hapo anapongezwa kwa 'Job Well Done' na kuna Mzigo ( Hela ) pia ya Asante ameshapewa / atapewa.

Huyu ni Version ya Mzee Mpili wa Yanga SC. Kuhusu kumjibu Mleta Mada ( Uzi ) huu ni kwamba Moja ya Kazi ya Mtu wa Mawasiliano na Mahusiano wa Klabu pia ni kufanya Fan Engagement, Kujichanganya nao na hata sometimes kufanya 'something Kiddish' ili Kumfanya Mshabiki ajione nae ni 'part and parce'l na Timu na hii husaidia katika Kuwashawishi na Kuwavutia wengine kitu ambacho huwa na Faida kwa Klabu Kiumaarufu na hata Kibiashara.

Mleta Uzi anitafute nimpe 'Elimu' zaidi!!!

Cc: malantu
 
Ulisikia wapi kuwa vitochi vinaleta madhara kwenye mpira? Vitochi vilikuwepo toka enzi hizoo za akina kaseja... na huwa vinatumiwa na mashabiki wa timu zenye malengo kama al hally, zamalek, simba..au timu za taifa zenye malengo kama senegal, misri... we unafikiri kwa mfano utopolo vs polis tz zikicheza unaweza kuona vitochi? Acha semaji liendelee kufanya mambo yake...
Uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo?

Unajua maana ya neno precedence? Huyu msemaji katengeneza precedence ya haya mambo kuendelea na kufanyika kwa ukubwa zaidi. Ndama ukimlea anakua ng'ombe mzima.
 
Amesifia uzalendo wa yule mzee, na kuongeza ya kuwa japo ile ni tochi ya kawaida ila haikuwa na madhara yoyote.

Sijaona alipohamasisha zaidi ya kuona ujasiri na umakini wa yule mzee na mapenzi kwa timu yake
 
Uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo?

Unajua maana ya neno precedence? Huyu msemaji katengeneza precedence ya haya mambo kuendelea na kufanyika kwa ukubwa zaidi. Ndama ukimlea anakua ng'ombe mzima.
Mkuu hebu nikupe heshima kidogo nikupime uwezo wako;
1. Umetazama video ya interview?
2. Umemsikiliza Ahmed maelezo yake yote?
3. Kama umemsikiliza,anasemaje?
 
Wapendwa nimemuona msemaji wa Simba huko YouTube akimtembelea na kumpongeza mzee aliyekuwa na kitochi uwanjani. Hii si sawa kwani anahamasisha vitendo vya utovu wa nidhamu unaoweza kuigharimu timu.

Kesho watu wakija na vitochi zaidi tena vyenye mwanga wenye madhara atafanyaje? Nilitegemea angekemea huo upuuzi lakini ndio kwanza ana uhamasisha.

Brother, wewe ni msemaji wa club kubwa, achana na vitu vya hovyo visivyo na tija.

NB: Niko tayari kwa povu.
Pambaneni zaidi kumshauri msemaji wenu
Simba haiwahusu
 
Wapumbavu wataamini kuwa Mzee wa Tochi Abdallah Mzuzuri ni Mtu wa Kawaida tu ila waliokuwepo Uwanjani shuguli yake waliiona iliyoleta Ushindi na hiyo Tochi ni Zuga tu, ila hapo anapongezwa kwa 'Job Well Done' na kuna Mzigo ( Hela ) pia ya Asante ameshapewa / atapewa.

Huyu ni Version ya Mzee Mpili wa Yanga SC. Kuhusu kumjibu Mleta Mada ( Uzi ) huu ni kwamba Moja ya Kazi ya Mtu wa Mawasiliano na Mahusiano wa Klabu pia ni kufanya Fan Engagement, Kujichanganya nao na hata sometimes kufanya 'something Kiddish' ili Kumfanya Mshabiki ajione nae ni 'part and parce'l na Timu na hii husaidia katika Kuwashawishi na Kuwavutia wengine kitu ambacho huwa na Faida kwa Klabu Kiumaarufu na hata Kibiashara.

Mleta Uzi anitafute nimpe 'Elimu' zaidi!!!

Cc: malantu
Ukikaribia muda wa kufuturu unakuwaga na akili kumbe
 
Mkuu hebu nikupe heshima kidogo nikupime uwezo wako;
1. Umetazama video ya interview?
2. Umemsikiliza Ahmed maelezo yake yote?
3. Kama umemsikiliza,anasemaje?

Mkuu sijatazama video. Nimejibu tokana na maelezo ya mleta uzi.

Kama mleta mada kapindisha maneno basi kakosea ila kama msemaji wa Simba kafanya hivyo kweli there's no other way about it.
 
Mkuu sijatazama video. Nimejibu tokana na maelezo ya mleta uzi.

Kama mleta mada kapindisha maneno basi kakosea ila kama msemaji wa Simba kafanya hivyo kweli there's no other way about it.
unajisikiaje kutoa hukumu bila kupata ukweli angalau wa kiasi kidogo? huku kuna video zinaonyesha kilichojiri ambacho ni tofauti na anayosema mleta mada.
Why hili taifa watu wake ni rahisi sana kupotoshwa? Tena ukimsikiliza Ahmed amefuta uvumi wote kwamba tochi ilikuwa na athari,akamzawadia jezi si kwa sababu ya tochi bali kwa amsha amsha yake jukwaani maana kila mtu alikuwa na vibe lake
 
Wapendwa nimemuona msemaji wa Simba huko YouTube akimtembelea na kumpongeza mzee aliyekuwa na kitochi uwanjani. Hii si sawa kwani anahamasisha vitendo vya utovu wa nidhamu unaoweza kuigharimu timu.

Kesho watu wakija na vitochi zaidi tena vyenye mwanga wenye madhara atafanyaje? Nilitegemea angekemea huo upuuzi lakini ndio kwanza ana uhamasisha.

Brother, wewe ni msemaji wa club kubwa, achana na vitu vya hovyo visivyo na tija.

NB: Niko tayari kwa povu.
Mna mechi na Azam kesho....na wewe andaa tochi
 
unajisikiaje kutoa hukumu bila kupata ukweli angalau wa kiasi kidogo? huku kuna video zinaonyesha kilichojiri ambacho ni tofauti na anayosema mleta mada.
Why hili taifa watu wake ni rahisi sana kupotoshwa? Tena ukimsikiliza Ahmed amefuta uvumi wote kwamba tochi ilikuwa na athari,akamzawadia jezi si kwa sababu ya tochi bali kwa amsha amsha yake jukwaani maana kila mtu alikuwa na vibe lake

Sina sababu na muda wa kuhakiki Kila kitu kinachokuja hapa jukwani nadhani hizo lawama apewe mleta Uzi kwa kupindisha maneno if so. As a responsible member he should have done the due diligence kabla ya kuleta hapa.
 
Back
Top Bottom