Msemo gani unatumia kujifariji baada ya kumaliza pesa kwa matumizi ya kijinga au starehe?

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
"SIKU MOJA MOJA SIYO MBAYA"

Leo nimekumbuka mwaka 2020 kipindi cha Pasaka, Jijini Arusha, hapo dili la ku-design michoro ya Majengo kadhaa ya Taasisi ya Kanisa limetiki na nka kabidhiwa pesa ya Advance Millioni +.

Sikukuu ya Pasaka ilipofika mwenyeji wangu akasema twende kusherekea kwenye Bar flani, yeye atasimamia show (ipo pembezoni mwa Barabara ya Moshono-Impala).

Tulivyofika eneo la tukio,Mimi,yeye na wadogo zake wawili tukaanza piga gambe.

Ghafla tukasikia tumeitwa ,kugeuka ni mshikaji wa mtaa mmoja.

Sasa hapo mjamaa wangu gambe zipo kichwani, akainuka na kwenda kucheza, alivyorudi, kaambatana na wadada wa4 (nao ni wa mtaani ) wakajumuika.

Mjamaa akantonya hela imekata, nimuokoe maana kuna mdada mmoja wapo anamuelewa.
Kwakuwa nami nipo Gambe nkasema "mwana usihofu ".

Hapo jumla tupo 9, wote wakaagiza supu nzito, wengine kiepe kuku.
Kila mtu akapata chupa zake tano za gambe, round zikarudiwa na kurudiwa, wengine Whisky...

Kuja kufika saa 9 usiku muda wa kusepa nikalipia Bili. Lipia usafiri wa kila mtu, nkampa mjamaa na hela ya kuhonga, nyingine sijui nilitupa.

Asubuhi ilivyofika, kuja kucheki nimetumia zaidi ya 400K. Hapo nikajifariji kwa kusema "SIKU MOJA MOJA SIYO MBAYA"

Je,msemo wako huwa upi?
Tupia na tukio hata moja.
 
"Kesho nitapa pia"!
 
""""HASARA ROHO PESA MAKARATASI"""
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…