Msemo gani unatumia kujifariji baada ya kumaliza pesa kwa matumizi ya kijinga au starehe?

Msemo gani unatumia kujifariji baada ya kumaliza pesa kwa matumizi ya kijinga au starehe?

bhana ee!, pesa hazijai
Ilikuwa around 2014 pale Escape One, nilitumia kizembe sana 300k na kama sio msela wangu mmoja nilikuwa niamke kapuku kesho yake.
 
"SIKU MOJA MOJA SIYO MBAYA"

Leo nimekumbuka mwaka 2020 kipindi cha Pasaka,Jijini Arusha,hapo dili la ku-design michoro ya Majengo kadhaa ya Taasisi ya Kanisa limetiki na nka kabidhiwa pesa ya Advance Millioni +.

Sikukuu ya Pasaka ilipofika mwenyeji wangu akasema twende kusherekea kwenye Bar flani,yeye atasimamia show (ipo pembezoni mwa Barabara ya Moshono-Impala).

Tulivyofika eneo la tukio, tukaanza shushia maji ya dhahabu mimi, mwenzangu na wadogo zake wawili.

Ghafla tukasikia tumeitwa ,kugeuka ni mshikaji wa mtaa mmoja (mtaa wa Baraa).

Sasa hapo mjamaa wangu gambe zipo kichwani,akainuka na kwenda kucheza,alivyorudi ,kaambatana na wadada wa4 (nao ni wa mtaani ) wakajumuika.

Mjamaa akantonya hela imekata,nimuokoe mana kuna mdada mmoja wapo anamuelewa.
Kwakuwa nami nipo Gambe nkasema "mwana usihofu ".

Hapo jumla tupo 9,wote wakaagiza supu nzito,wengine kiepe kuku.
Kila mtu akapata chupa zake tano za gambe ,round zikarudiwa na kurudiwa, wengine wanataka Whisky...

Kuja kufika saa 9 usiku mda wa kusepa
nkalipia Bili.Lipia usafiri wa kila mtu,Nkapitia mjamaa na hela ya kuhonga,Nyingine sijui nilitupa.

Asubuhi ilivyofika, kuja kucheki nimetumia zaidi ya 400K
Hapo nikajifariji kwa kusema "SIKU MOJA MOJA SIYO MBAYA"
Maisha ndio hayahaya..
Huko jikoni nitengenezeeni kuku sekela mzima na chips mtumio alfu na pilipili km ya siku zote..
 
Nile PESA kaburini,.
Hela yenyewe huwezi kununua Ferrari,
kujenga huwezi,hata chochote hauwezi.
Sasa ushindwe hata kunywa bia tena au kiroba,hata gongo unatwanga tu.
Mi hadi vilabuni ukinikuta utashangaa.
Napiga pombe za kienyeji ka sina akili nzuri.
Kesho bar za kueleweka
nshabadilika pedeshee tayari.
Kesho utanikuta Masaki Karambezi ndo utachoka
 
Nile PESA kaburini,.
Hela yenyewe huwezi kununua Ferrari,
kujenga huwezi,hata chochote hauwezi.
Sasa ushindwe hata kunywa bia tena au kiroba,hata gongo unatwanga tu.
Mi hadi vilabuni ukinikuta utashangaa.
Napiga pombe za kienyeji ka sina akili nzuri.
Kesho bar za kueleweka
nshabadilika pedeshee tayari.
Kesho utanikuta Masaki Karambezi ndo utachoka
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dr Remmy aliimba rafiki yangu yule tukipiga story miaka hiyo akila mchicha wake.
Kilio
" kama wote tukiwa madereva
Nani atakua abiria"
"Wote tukijenga,nani atakua mpangaji?
Wote tununue viatu vipya,fundi viatu afanye kazi gani?
 
Ilikua 2022 nilipata mchongo wa 800k afu nlikua nna jambo langu LA maana nifanye,

Shost akanipelekaa Mikocheni kuna duka LA viwalo, aseeh nlinunua nguo ambazo hata sikuwaza, kuja kutazama imebaki 260k

Hatariii tupuu.
Ikawa full kuvurugwa, alafu kanakuja kale ka msemo ka faraja, kama nilipata hizi ntapata zingine
 
Back
Top Bottom