tunaposema mshahara wa Salamba ni mdogo tunalinganisha na mshahara upi? Je tunalinganisha na ule aliokuwa analipwa stendi united kabla hajaenda lipuli, je ni ule aliokuwa analipwa lipuli? au tunalinganisha na ule uliopo kwenye mikataba ya wachezaji wa timu fulani kubwa lakini hawalipwi labda mpaka baada ya miezi mitatu?. Siku hizi mnaweza kuwa sawa kazini vyeo sawa elimu sawa lakini mishahara tofauti inategemea uwezo wako wa mazunugumzo na utendaji wako wa kazi tu. Mimi namshauri Salamba huo mshahara asiuone mdogo yeye apambane uwanjani afanye kweli kama alivyofanya Mlipili halafu msimu wa kwanza tu kwake wa ligi unapoisha viongozi lazime wamwite wenyewe mezani wajadiliane namna ya kumboreshea maslahi. Wabongo wengi huwa tunafeli hapo unapewa nafasi badala ya kupambana na kuonyesha kuwa unaweza unaanza kulalalmika kuwa mara mshahara mdogo, mara maslahi madogo. Napenda kumtumia sana Mlipili kama mfano kwa sababu yeye ndio mchezaji aliyesajiliwa kwa dau dogo sana mwaka jana na pia hakupewa nafasi kabisa ya kuwika lakini leo ni gumzo kwa kila mtu. Na yote yametokana na mapambano yake uwanjani baada ya kupewa nafasi kidogo tu hakulalamika badala yake aliacha kipaji chake kiongee zaidi na wala sio mdomo wake na kinachofutia sasa ni piochi yake ya kujaa.