Mshahara wa nyota mpya wa Simba, Adam Salamba ni milioni 48

Mshahara wa nyota mpya wa Simba, Adam Salamba ni milioni 48

Wadada changamkieni fulsa hii na hyo rangi sasa Mbona mtajigonga
 
Yuko vizuri ila heading yako haijakaa poa inaonekana kama kwa mwezi mmoja analipwa Mil .48
 
Milioni mbili kwa mwezi sio mbaya kwa mchezaji anayejitambua anataka nini mbeleni. tafuta signing fee ya mlipili na kichuya na mishahara yao kwa mwezi halafu angalia watakapokuja kuongeza mkataba watalipwa nini. cha msingi afanye kazi ndani ya msimu huu wa ligi aongeze thamani yake simba wenyewe watapanda dau la mshahara na ada ya usajili achilia vilabu vingine.
Ndogo mno...!
 
Duuh, sema atajifunza kwa wenzake wanaopita kuomba omba kwenye ofisi za watu hapa mjini, ukijumlisha ofa za bia na chakula ataishi tuu
 
tunaposema mshahara wa Salamba ni mdogo tunalinganisha na mshahara upi? Je tunalinganisha na ule aliokuwa analipwa stendi united kabla hajaenda lipuli, je ni ule aliokuwa analipwa lipuli? au tunalinganisha na ule uliopo kwenye mikataba ya wachezaji wa timu fulani kubwa lakini hawalipwi labda mpaka baada ya miezi mitatu?. Siku hizi mnaweza kuwa sawa kazini vyeo sawa elimu sawa lakini mishahara tofauti inategemea uwezo wako wa mazunugumzo na utendaji wako wa kazi tu. Mimi namshauri Salamba huo mshahara asiuone mdogo yeye apambane uwanjani afanye kweli kama alivyofanya Mlipili halafu msimu wa kwanza tu kwake wa ligi unapoisha viongozi lazime wamwite wenyewe mezani wajadiliane namna ya kumboreshea maslahi. Wabongo wengi huwa tunafeli hapo unapewa nafasi badala ya kupambana na kuonyesha kuwa unaweza unaanza kulalalmika kuwa mara mshahara mdogo, mara maslahi madogo. Napenda kumtumia sana Mlipili kama mfano kwa sababu yeye ndio mchezaji aliyesajiliwa kwa dau dogo sana mwaka jana na pia hakupewa nafasi kabisa ya kuwika lakini leo ni gumzo kwa kila mtu. Na yote yametokana na mapambano yake uwanjani baada ya kupewa nafasi kidogo tu hakulalamika badala yake aliacha kipaji chake kiongee zaidi na wala sio mdomo wake na kinachofutia sasa ni piochi yake ya kujaa.
 
We bwana weeh andika vizuri mill 2 unasema mshahara mill 48 ungesema usajili wake ni gharama hiyo
 
Karibu mtaa wa msimbazi kijana
Juhudi zako kama kichuya zinahitajika
 
Yupo wapi huyu?
Alipigwa misumari ya kutosha, kwa sasa hata hajulikani alipo. Simba siyo mahali salama kwa young players.

Labda kwa wachezaji wazee, walau wanaweza kuonekana kwa misimu michache! Na baada ya hapo, na wenyewe pia hupotelea kusikojulikana.
 
Back
Top Bottom