Mshahara wa Rais Magufuli wawa gumzo Kenya

Kwanza kabisa hongera kwa Rais Magufuli kwa kuanzisha uwazi huu.

Baada ya hongera hiyo nina machache.

Kuzungumzia sana mshahara wa mtu anayeweza kupiga simu Benki Kuu na kuagiza apewe mabilioni ya fedha kwa kazi za siri za "Uslama wa Taifa", na akapewa, bila kuzingatia bajeti, ni kutojua jambo la muhimu kabisa liko wapi.

Jambo la muhimu kabisa simshahara anaolipwa rais, that is peanuts.

Jambo la muhimu ni nguvu za uMungu-Mtu alizopewa rais ambazo zinaweza kutumiwa vibaya kupiga hela ndefu sana kiasi huo mshahara ukaonekana ni vijisenti vya vijisenti.
 
Hapo kweli na Dawa ni kupunguzwa nguvu..na iwepo tume ya kupanga mishahara kwa watumishi wote na kuiweka wazi kma ilivyo kwa nchi jirani yetu..
 
Maneno yake usiyaamini, rejea nitaongeza, siongezi na sitoongeza, salary slip
 
Hapo kweli na Dawa ni kupunguzwa nguvu..na iwepo tume ya kupanga mishahara kwa watumishi wote na kuiweka wazi kma ilivyo kwa nchi jirani yetu..

Kimsingi hilo ndo nimekuwa nikilipigania kwa zaidi ya miaka 10 humu JF.

Mshahara wa rais wetu si taarifa ya umma au taarifa iliyo wazi kwa umma.

Na ndo maana kiasi chake hakijulikani rasmi na matokeo yake ni kuwa huo mkanganyiko.

Huyu anadai ni kiasi hiki...yule kiasi hiki...na yeye mwenyewe kiasi hiki.

Kenya huwezi kukuta discrepancies kama hizo kwa sababu kiasi kinapangwa na tume yao ya mishahara ya watumishi wa umma na hivyo kufanya chanzo cha taarifa kuwa kimoja tu.

Marekani nako ni vivyo hivyo. Bunge lao ndo linapanga kiasi cha mshahara wa rais, makamu wa rais, na viongozi wengineo.

Huwezi kukuta figures tofauti tofauti za mshahara wa rais wa Marekani.

Lakini kwetu sisi jambo kama hilo ni hisani ya rais wakati sisi ndiyo tunamlipa huo mshahara.

Na sasa hivi tutajuaje kama ametudanganya?
 
BASI WAJE KUMCHUKUA AENDE KWAO WATUPE UHURU KAMA HAWAJAMRUDISHA NA MATATUU KESHO KUTWA

Siyo kweli, tuna/tutamshindwa Magufuli coz siyo wa type yetu - vilaza, wapenda vyupi, wavivu, waongo, wapenda majungu, wasiojitambua, wasiojiamini, wasio na misimamo, wanaojadili watu na sio mada.

Nenda Kenya hautakuta behaviour za kibongo. Huko Magufuli ataonekana mzuri kwa sababu yeye anataka kumreward mtu kutokana na kazi yake. Hapa tunaona fahari mtu anayefunga baa nzima kila siku lakini Hana kipato kinachoeleweka. Ni nchi tuliyotaka kuifanya ya wapiga dili huku tukidharau wasomi.

Kenya time is money, kwa Tanzania hata hapa DSM time ipo tu muda wote.
Mungu ametuwaishia Magufuli naona haukuwa muda wake. Pliz for the record - Magufuli ametuwahi ni sawa na mwanafunzi wa hesabu darasa la II kufundishwa na mwalimu wa hisabati darasa la VII lazima mtashindwa kuelewa tu somo hata ajikunje kiasi gani kuelezea maana vichwa vyenu bado.
 
Huu uzi bana, hehe. Watanzania mna maneno! 😀 Eti hizo ni akili za kupewa, ongeza na zako.
 
Nakubaliana na wewe mkuu
 
Atoe salary sleep yake kama ni kweli
Hapo kwa 'salary sleep' ndo umenikanganya kidogo jombaa. Ongeza karoyco kiasi tukuelewe basi. Ndo ule usingizi mnono unaompata mtu akishalipwa mshahara au?
 
Reactions: Oii
Ni nini kilitokea baada ya kuapishwa ? la pili kibaki ni kiongozi mwenye hadhi usimfananishe na yule shamba boy.
Kwa sbu anatoka Central na alikuwa mkikuyu, kule abakubalika atokaye Rift na Central tu, na awe mkalenjini au mkikuyu, Odinga angekuwa na hizo sifa angekuwa Rais tangu 98 ila urais atausikia tu....
 
Mkuu, umemaliza na umeua. Naona tinga tinga limekuja mapema sana, limekuta watu bado wamelala.
Na bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…