SI KWELI Mshahara wa Rais wa Kenya ni mara 3 zaidi ya Marais wa Misri na Nigeria na mara 4 zaidi ya Rais wa Tanzania

SI KWELI Mshahara wa Rais wa Kenya ni mara 3 zaidi ya Marais wa Misri na Nigeria na mara 4 zaidi ya Rais wa Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mshahara wa Rais wa Kenya ni mara 3 zaidi ya Marais wa Misri na Nigeria na mara 4 zaidi ya Rais wa Tanzania.

Kuna ukweli hapa?

1660375184472.png
 
Tunachokijua
Mishahara ya marais wa Nchi mbalimbali imekuwa ni ajenda inayozungumzwa mara kwa mara. Baadhi ya nchi zimejaribu kuweka waazi mishahara ya marais wao huku wengine wakiifanya kuwa siri kubwa isiyoweza kufikiwa na umma.

Kwa muktadha huo huo, Madai ya kuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anapokea mshahara unaofikia mara 4 ya ule wa Rais wa Tanzania yameibuka.

Madai haya yanafafanua zaidia kuwa mshahara wa Rais kenyatta unafikia mara 3 ya ule wanaopokea marais wa Nchi za Misri na Nigeria.

Mishahara ya Marais
Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, Mshahara wa Rais wa Kenya Uhuru Keyatta ni Dola za Marekani 14,000 kwa mwezi.

Aidha Rais wa Misri mshahara wake ni dola 63,000 kwa mwaka, sawa na Dola 5,250 kwa mwezi. Rais wa Nigeria hupokea Dola za Kimarekani 70,000 kwa mwaka, ambazo ni wastani wa Dola 5833 kwa mwezi.

Kwa upande wa Tanzania, baada ya kuingia madarakani, Rais John Magufuli alianza mchakato wa kupunguza mishahara ya viongozi wa taasisi za umma na kuamua kupunguza mshahara wake hadi kufikia Dola za Marekani 4000, ambayo inakadiriwa kufikia Milioni 9.

Rekodi za mishahara hii ni kwa kurejea takwimu za kabla ya mwaka 2020 na inaweza kubadilika kadri muda unavyozidi kwenda.

Ulinganisho wa ukubwa wa Mishahara
Kwa kurejea kiasi cha mishahara iliyoainishwa hapo juu, madai yanayotajwa na mdau yatakuwa sahihi.

Mathalani, kiwango cha Dola 4000 anachopata Rais Magufuli kinaingia mara 3 kwenye kiwango cha Dola 14,000 anachopokea Rais wa Kenya na kubaki dola zingine 2000.

Vivyo hivyo, mishahara ya marais wa Misri na Nigeria kikizidishwa mara 3 kinazidi kile anachopokea Rais Kenyatta.

Aidha, mishahara hii haijazingatia marupurupu mengine wanayopokea marais hao.
Back
Top Bottom