Mshamba mimi sijawahi kwenda Club/disco, washamba wenzangu tukutane hapa!

hujawahi shawishiwa kwenda hata siku 1?
 
Nimeanza kutoroka nikiwa darasa la tano kwenda disco vumbi mpaka sasa disco naenda coz napenda sana mziki na najua kuucheza hivyo nafirijika kukumatia tunanyonga juu mpaka chini mara kulia kushoto aahaa raha sana na nikisafiri moja ya maeneo muhimu ninayoenda ni clubs
za eneo husika
 
acha kabisa asee

anaenda na bi maza ako au anenda peke ake kukutana na vinguchiro vya huko?
Bi. Mkubwa alikua anaenda na faza enzi hizo lkn ameshaacha siku hizi,amemuachia mzee baba akajichekie watoto wazuri arudi zake home ku-mbonji.
 
Hizo shule zipo karibu kweli? Maana St Francis de Sales ipo kule chini maeneo ya kota za Godes,then hii St Ann ipo huku barabarani kabisa, japo zote zipo Kihonda
 
Hizo shule zipo karibu kweli? Maana St Francis de Sales ipo kule chini maeneo ya kota za Godes,then hii St Ann ipo huku barabarani kabisa, japo zote zipo Kihonda
yap st ann na st francis ukaribu wake ni wa dk 5 tu

hope wewe unazijua kweli
 
Sio tu nazijua,Bali hta asubuh hii nimepita hapo St Francis, naelekea Maghorofani
BADO NI UNAZIJUA TU

ungekua unazijua zaidi ungekua umeshaingia ndani

so ni unazijua (sawa bob)
 
Nilianza kwenda club nilivyomaliza form six anzia siku hiyo hadi leo na uzee wangu naenda💃💃💃


Shoga ww uko km mm..jaman mm disco namuachia awaye yote ataamua..two weeks ago nimeenda bwana kuna kilounge kimoja kitaamuuu...matata balaa..nikakumbushia way back..aisee nitaamua kuacha kinywaji sio kucheza muziki aisee..!i love dancing ...mwe midude ya kinaigeria namuachia nani..!😅😅..
 
BADO NI UNAZIJUA TU

ungekua unazijua zaidi ungekua umeshaingia ndani

so ni unazijua (sawa bob)
Mule ndani St Francis nimeshaingia Mara nyingi Sana, opposite na Hiyo shule Kuna nyumba ya watawa nilikua nna bill ya maziwa pale,Kuna court ya Basketball kma unakumbuka vizuri,then hao wahindi wa St Francis nilikua nasali nao kule juu kwenye kanisa lao karibu na Polyester Club
 
Mm nimeanza toka niko darasa la saba mpaka now club hizi naenda sana na nilazima nicheze tena baada ya kulewa ndo uwa nacheza


Mimi wala sihitaji booster aisee..harusini nilikua natuma ujunbe kbs dj asiniangushe🤣🤣..woga ss dingilai. Nikajitoa ufahamu .chezaaa...mama akaniambia harusi imejaa pepo wachafu🤣🤣🤣🤣
 
Washamba tumekutana mimi mwenyewe sijui hata Club panafananaje. Nakumbuka enzi hizo after class viburudisho ili kuwa ni kucheza mpira ama kushindana michano ya freestyle za Hip Hop za wakali kama kina Songa. Ma injinia wote wa Mathematics tulikuwa tunakutana hapo, Club yangu ilikuwa ni geto langu mziki mkubwa nikifungulia basi najiona kama Osama Bin Laden.
 
Silent henzi za friday facult?
Aisee mi hakuna mkoa nimeenda nisikanyage Disco...!!

Miye hiyo Ndiyo frevor yangu sbb tuu ya majukum.Nakumbuka kuna siku nilienda Dom kulikuliwa na club 84 mpya. Weee dance mpk asbh Alafu nikachukua dinga mpk Dar mkavu.
 
Mimi wala sihitaji booster aisee..harusini nilikua natuma ujunbe kbs dj asiniangushe🤣🤣..woga ss dingilai. Nikajitoa ufahamu .chezaaa...mama akaniambia harusi imejaa pepo wachafu🤣🤣🤣🤣

Miye nikisha twanga Pepsi yangu ndani maji tuuu, Keisha habari yangu.
Lakini ukiniona utafikili nimekata vichupa kadhaa za Savana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…