Mshana JR amebadilisha maisha yangu, vijana wenzangu mtumieni mshana JR kabla hajaondoka duniani

Umenipa nguvu za kumalizia kusoma Kitabu fulani kihusuyo hayo mambo ili niwe mbobevu.

Barikiwa sana Mkuu 🙏🙏🙏
 
Za kwako zinakutosha mwenyewe😂😂😂
we ni mtani wangu, ukizumgumiziwa vibaya nakuzungumzia vizuri na ukizungumziwa vibaya nakuzungumzia vizuri!! umejua kuteka saikolojia za wanazengo!!🤣
mi utani na wewe sehemu yoyote hata uchukie utakoma mwenyewe but all in all how is nazjaz doin..?
 
hayo mawaidha yaweke katika uwalisia kimaisha sasa

kawaida ya wengi wakitoka semina au kupata darasa vichwa huwa vimejaa shuhuli ni katika kuyafanyia kazi kwa uwalisia ndugu, nikusii shirikiana nae bega kwa bega kwani namini bado hujaiva sawasawa ndio mana kila mwaka tunakwenda ibada na msahafu ni uleule kuteleza ndio ubinadamu kusahau ni yetu jadi kikubwa ni kuyasawazisha makosa kila kukicha
 
Mimi sikuwahi kuonana naye lakini aliwahi kunishauri vitu kadhaa ambavyo vimenisaidia kwa kiasi flani mpaka natamani siku moja nisafiri kwa ajili ya kuonana naye!
Halafu cha ajabu kuna members humu ambao hutanguliza pesa mbele Yaani kukupa ushauri au msaada wa mawazo tu unakuta mtu anatengeneza mazingira ya kukufanya uwe fursa ya kukupigia pesa ila kwa huyu jamaa ni tofauti kabisa Yaani ukimfuata Pm una jambo hakwambii mambo ya kukuomba hela wala kukuuzia dawa au mbinu flani ila jamaa anakupa idea then anakwambia ifanyike kazi basi
Kiukweli huyu mwamba angeamua kujitangaza kwamba ni mganga au nabii naamini angepiga hela sana ila Inaonekana ni mtu mwenye maarifa mengi kuhusu mambo ya kimaisha na utafutaji lakini hatumii changamoto za anaowashauri ili kujipatia pesa yeye anakupa ushauri bure basi!
Wabongo wa hivi wamebaki wachache sana cjui huyu jamaa ni kabila gani!
Mungu ampe maisha marefu huyu mwamba naamini siku moja ntakutana naye nimshukuru kwa chochote na pia nijifunze mengi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…