Mshangao: Wanafunzi wa shule moja ya msingi wote wamechaguliwa secondari moja

Mshangao: Wanafunzi wa shule moja ya msingi wote wamechaguliwa secondari moja

Ina maana hao vijana hawatakuwa na maarifa mapya ya kijamii maana wanafahamiana tangu utotoni. Uwezo wa kuchangamana na tamaduni zingine kwao utakuwa mdogo sana.

Huku ndio kuja kuwa na watu wanaoamini vyakula ni Ugali, wali na makande 😂 maana hawajui jambo jipya lolote.
Ukitamani kupata upeo mpya "exposure" lakini ukaona Serikali imeshindwa kukusaidia kwakuwa haiwezi kimiundombinu jisaidie wewe mwenyewe.

Kuwa mfano wa baba kwenye ndoto zako na za wanao, hakikisha wanapata Elimu bora. Serikali haina mkono mrefu wakumgusa kila mtu.
 
Leo nilikutana na bwana mdogo mmoja akaniomba nitazamie shule aliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza.

Cha ajabu nikakuta wanafunzi wote 230+ wamechaguliwa kwenda secondary moja yani ni kama kuhamisha shule nzima kwend secondary moja.

Je hii imenifanya nitafakari Sana namna selection zilivyofanyika au wote walichagua io shule.
Inatokeaga Sana kwenye shule za kata ni kama kuhamishwa darasa..
 
Ukitamani kupata upeo mpya "exposure" lakini ukaona Serikali imeshindwa kukusaidia kwakuwa haiwezi kimiundombinu jisaidie wewe mwenyewe.

Kuwa mfano wa baba kwenye ndoto zako na za wanao, hakikisha wanapata Elimu bora. Serikali haina mkono mrefu wakumgusa kila mtu.
Ni kweli nakubaliana n wewe kabisa, ila nmeshangaa kuona watunga sera hawana hata wazo la kuwapa hao vijana upeo mpya.

Robo tatu ya darasa kujikuta shule moja ni jambo la kusikitisha sana. Shule nyingi za kata ni kama vituo vya makuzi tu.
 
Umesoma primary ukafanya kitu ukawa unataniwa , ila unajip moyo nikienda sec haya yataisha mara sec ni watu wale wale eneo ndio tofauti, unaendelea kutaniwa au kuonewa.
Usinikumbushe, kuna mtu mmoja alikuwa na vipele miguuni tulipokuwa primary. Sasa sisi tulikuwa tukimuona tunasoma miguu yake tunasema gazeti. Eti vile vidone vidone tunaona km maandishi. Baati mbaya tukafaulu woote sec jamani tulimuita hivyo hivyo wala hakujali mwisho form 4 tulilimaliza lile jina. Sasa no big boss halmashauri huko.
 
Ni kweli nakubaliana n wewe kabisa, ila nmeshangaa kuona watunga sera hawana hata wazo la kuwapa hao vijana upeo mpya.

Robo tatu ya darasa kujikuta shule moja ni jambo la kusikitisha sana. Shule nyingi za kata ni kama vituo vya makuzi tu.
Wakati shule hizi mpya zinajengwa tulitakiwa kujua ndizo zitakazowachukua wadogo zetu. Jambo pekee la kuhamasisha ni kwamba zipewe huduma bora, vinginevyo sioni shida wanafunzi wa shule moja ya msingi wakisoma shule moja wakiwa Sekondari.
 
Usinikumbushe, kuna mtu mmoja alikuwa na vipele miguuni tulipokuwa primary. Sasa sisi tulikuwa tukimuona tunasoma miguu yake tunasema gazeti. Eti vile vidone vidone tunaona km maandishi. Baati mbaya tukafaulu woote sec jamani tulimuita hivyo hivyo wala hakujali mwisho form 4 tulilimaliza lile jina. Sasa no big boss halmashauri huko.
Unaona sasa. Unapiga hatua na past zako zinakufuata nyuma😂
 
Unaona sasa. Unapiga hatua na past zako zinakufuata nyuma😂
Angalau unapata muda wakuishi maisha yaliyojaa utani, vituko na vibweka. Shule ni sehemu pekee inawageuza watu na kuwaacha wainjoi kwa kipindi kifupi kabla hawajakutana na uhalisia wa maisha.
 
Unaona sasa. Unapiga hatua na past zako zinakufuata nyuma😂
Lakini mwenyewe hata hajali maana alikuwa mweusi ule wa kuteleza tulikuwa tunamwita dege ( kungulu) yaani huwezi amini hadi kesho tunamwita hivyo wala hajali.
 
Shule ya Sekondari ipo kwenye kata yao hao wanafunzi wa shule ya msingi, unataka wakasome wapi? Waanze kuijaza shule yao ya kata kwanza kabla ya wageni. Kama kijana hataridhika kubaki shule hiyo anaweza kuhama, mzazi au mzazi wake kama anajimudu apelekwe shule ya binafsi
Inamana hakuna waotot wenye ufaulu wajuu kwenda shule zingine zinazochukua ufaulu wa juu? Lakini pia psychological sio kitu kizuri kwa mtazamo wangu mtoto Anapaswa kupata changamoto mpya kukua zaidi.
 
Nilimaliza la 7 mwaka 98 hakuna kitu ambacho ningetamani kama darasa letu lote tungeenda sekondari wote kwenye shule moja. ..
 
Inamana hakuna waotot wenye ufaulu wajuu kwenda shule zingine zinazochukua ufaulu wa juu? Lakini pia psychological sio kitu kizuri kwa mtazamo wangu mtoto Anapaswa kupata changamoto mpya kukua zaidi.
Watoto waliopata ufaulu wa juu wamepangiwa shule za kiwango chao (Kipaji, Teule, au Teule Bweni), watoto wengine wamepangiwa shule wanazostahili.
 
Santa kayumba,hapo anaacha shule mmoja mmoja mnaingia form one wanafunzi 200+ kufika mwezi wa sita washabaki 100
 
Back
Top Bottom