Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
Alianza kama utani baada ya kurudi likizo ya semister ya mwisho huyu mshikaji wangu wa chuo sijui alikutana na nani huko kwao akamshauri kuhusu mambo ya forex,

Alivyorudi akanisimulia kuhusu hiyo inshu mi nilichomwambia ni kitu kimoja tu hiyo kitu ya forex mi nilishasoma sana mada zake huko Jamii forum kwa kina Ontario na kujua hasara na faida zake kuna watu wameunguza acount zao wanalia kilio cha mbwa koko hakunisikia,

Sasa bhana wale watu aliokutana nao huku wakawa wanamshauri anatoka dom to dar kwenye semina na darasa lao na kila akirudi story ni forex,forex na yeye,

Basi bhana miezi kadhaa imepita baada ya kutrade sana na ile acount ya dermal kafungua real Account kinachomkuta huko mi sijui naona tu kila siku anauza vitu,

Alianza na Laptop yake min, akafata desk top yake ,juzi kati kauza mtungi mkubwa wa gase pamoja na jiko lake, naona kabakiwa na friji pamoja na kitanda na ata hivyo naona analipigia mahesabu friji anataka kuliuza na hilo sasa sijui kimempata nini huko kwenye forex,

Daily nampa ushauri aachane na hiyo biashara yake ya forex naona hanisikii sasa mi nasubiri kuona mwisho wake.


Sent using Jamii Forums mobile app

mkuu huyo jamaa hana usimamizi mwambie ajiunge hapa na telegram group BRIGHT FOREX TANZANIA INSTITUTE au anicheki ni msaidie bure maana wengi wana unguza bila kujua misingi imara. mpe pole sana
 
Mkuu mbona ni yaleyale tena...mi nikajua unanipa madini kwa ufupi hapa kuhusu pesa inaenda wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unapata tabu tupu..ukitaka kujua uhalisia wa mtu usipate tabu jaribu kurudi nyuma kwenye nyuzi zake.

Huyo dogo anaekulisha vitango pori hapa kuna uzi analalamika hana ajira..baadae kuna uzi mwingine anasema anauza kuku..

Jana akanipostia vile vi random internet pictures za dolla akisema zake..nilivoinua nyuzi zake za nyuma akakimbia mazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FOREX sio ya Kujiingizia pesa kwa Kuotea...

FOREX ni hatari mara 100 ya Betting...

FOREX inahitaji usomee hasa na uelewe nini Unafanyaa...

FOREX haiwezi kuwa kimbilio la kijana maskini wa kitanzania hata Siku moja!

FOREX SIO MCHEZO SITAKI KABISA KUJARIBU

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaa

Man,play that game maybe can be your chance to be the youngest billioner in Tanzania
 
Kabla ya kufanya biashara ya Forex huu ujumbe unapatikana kwa kila broker awapatie trader wake.. Sasa sijui kama nyie huwa mnaelewa kinachoandikwa hapo.


Yaani mtu mzima unafananisha Ujinga ujinga na upuuzi wa Qnet na Forex ?? Biashara ambayo ni halali kwenye nchi ya dunia za kwanza miaka na miaka. Hiyo Qnet ni pyramid scheme bussines ambayo katika nchi kama marekani ni kosa la jinai kufanya Ponzi bussines na ukikamatwa ni kifungo.



Ninachojifunza hapa, watanzania ni wavivu wa kutafuta maarifa kabisa. Hufanya maamuzi kwa kusikia watu wanasema nini. Mtu akisikia Deci anaenda. Akisikia D9 anaenda . Akisikia Forex anaenda ila hana sababu zake za kiutafiti kwanini kafanya hayo maamuzi.


Amini nakwambia ukifanya utafiti wako kuhusu biashara ya forex bila kuwa bias utakuja kunitafuta siku moja. Kama una king'amuzi cha Dstv weka channel namba 411 (Bloomberg Tv) naamini utaelewa Forex ni nini.




Sasa Kama MTU anasema forex ni utapeli hivi ukisikia biashara ya stocks, commodities, indices na shares si ndio mtasema ni ujambazi. Hebu nikusaidie tafuta gazeti la either The citizen au Daily News nenda kwenye ukurasa wa bussines utakuta FOREX,INDICES,SHARES & commodities zinachambuliwa vyema kabisa.

Maarifa Maarifa Maarifa .... Tafuteni maarifa. Inauma sana mwaka 2019 bado kuna kiumbe duniani anasema FINANCIAL MARKETS ni utapeli . Bado kuna mtu anashidwa tofautisha Marketing Network na Financial Markets.




View attachment 982938

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndio daudEURUSD????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaa

Man,play that game maybe can be your chance to be the youngest billioner in Tanzania
Hapana mkuu... Siwezi kabisaa!! Nilijaribu kusoma mara 2 lakini kila nkisoma sielewi.. Mara pip sijui nkasema niombe nipigwe pindi jamaa akatala laki na nusuu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hapo ndo nkajisemea mchezo usiuchezee kabisaaa huu... Yani nitoe pesa nijifunze namna ya kupoteza pesaa tenaa bora nibet tu mkuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MBONA MAMBO YANA ONEKANA TU NA NI SIMPLE. SIJUI HAO WATU WANA CHOMAJE WAKATI UKIWA UNATUMIA RISK MANAGEMENT NI SAFI SANA

GBPUSDH4.png


EURGBPH4.png
 
Sio lazima forex hata kutrade stock kuna faida tena kwa waoga wa kutrade forex you can do stock...tumia volume analysis yaan ni mtelezo tu hivi ugumu ni nin jamn na mbona complications...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom