Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
Porojo tu.

Sijawahi shiriki biashara ya Forex wala sijawahi amini katika biashara hiyo.
mbona mnapiga watu ban za mwezi halafu baada ya hapo hamwafunguli mnasababisha wanafungua profile nyingine, kama mtu alikosea na kuweka labda link si mnafuta kisha mtu anaendelea na jamii forum kama kawaida. nahisi hilo ni tatizo kubwa sana huku. rafiki yangu mmoja ni victim tokea mwaka jana mwezi wa 9

nnnn.JPG
 
Mwambie awekeze kwanza kwenye ufahamu na maarifa ndio awekeze pesa maana bila kusoma ba kuelewa hii kitu hawezefanikiwa Mimi nimeanza akaunti ya live mbona nampiga tu na hata asubuhi ya Leo nimepiga
 
Mwambie awekeze kwanza kwenye ufahamu na maarifa ndio awekeze pesa maana bila kusoma ba kuelewa hii kitu hawezefanikiwa Mimi nimeanza akaunti ya live mbona nampiga tu na hata asubuhi ya Leo nimepiga
_20190103_094728.jpg
 
Alianza kama utani baada ya kurudi likizo ya semister ya mwisho huyu mshikaji wangu wa chuo sijui alikutana na nani huko kwao akamshauri kuhusu mambo ya forex,

Alivyorudi akanisimulia kuhusu hiyo inshu mi nilichomwambia ni kitu kimoja tu hiyo kitu ya forex mi nilishasoma sana mada zake huko Jamii forum kwa kina Ontario na kujua hasara na faida zake kuna watu wameunguza acount zao wanalia kilio cha mbwa koko hakunisikia,

Sasa bhana wale watu aliokutana nao huku wakawa wanamshauri anatoka dom to dar kwenye semina na darasa lao na kila akirudi story ni forex,forex na yeye,

Basi bhana miezi kadhaa imepita baada ya kutrade sana na ile acount ya dermal kafungua real Account kinachomkuta huko mi sijui naona tu kila siku anauza vitu,

Alianza na Laptop yake min, akafata desk top yake ,juzi kati kauza mtungi mkubwa wa gase pamoja na jiko lake, naona kabakiwa na friji pamoja na kitanda na ata hivyo naona analipigia mahesabu friji anataka kuliuza na hilo sasa sijui kimempata nini huko kwenye forex,

Daily nampa ushauri aachane na hiyo biashara yake ya forex naona hanisikii sasa mi nasubiri kuona mwisho wake.


Sent using Jamii Forums mobile app
FOREX sio sehem ya kucheza,mwambie atulize akil na aichululie ni biashara kama biashara zingne lasivyo ataendelea kula za uso tu

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom