Sielewi unachozungumzia hapa, maanake umeweka kijumla jumla tu.
Lakini ninachojua, kwa uhakika ni kwamba mmekwisha ondolewa kwenye lile vugu vugu mlilo wahi kuwa nalo, la kuiondoa CCM madarakani.
Mlisha fanya kazi kubwa sana chini ya mazingira magumu sana, na dalili zilikwisha anza kujionyesha kwamba adhma yenu inaelekea kwenye lengo hilo.
Hayo yalikuwa ni ya wakati huo.
Ya wakati huu, ni dhahri kuna sumu iliyo mwagwa miongoni mwenu, iwatafune taratibu, na kuvuruga mipango ya kuiongoza nchi hii.
Matokeo yake tunayaona, hata kama mtayaficha na kuyakana kuwa hayapo.
Wakati ambapo mlikuwa mmefikia hatua ya kumsukuma mlevi (CCM) aishie korongoni, imegeuka na kuwa kama mlevi huyo huyo ndiye anaye waamurisha mfuate maagizo yake!
Mlevi anajiandaa na mbinu zile zile alizotumia miaka yote kumbakisha madarakani, lakini kwenu ni kama hamuoni wala kuelewa kinachofanyika, na hamjibidishi kujipanga kuzuia uhalifu huo.
Haya ni matokeo ya sumu mliyo nyweshwa. Mnabaki tu sasa mkituonyesha picha za viongozi wakifurahia maisha, badala ya kupambania maslahi ya nchi hii.
Inasikitisha.