Mshituko: Rais Magufuli, agoma kumsalimia kwa mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar ndugu Paul Makonda

Binafsi naona serikali ishajua akili za wananchi wake kwahyo tukio kama hili nadhani lilikua planned yaan magufuli na makonda wote walipanga ili kuchek upepo wetu au makonda hakujua hili ila Mzee alijua na akaamua kufanya ili kuchek upepo wetu na kweli kila kona pamechafuka na hii ishu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ipo nimeona huko twita. Inaonesha amemruka maalim Seif halafu kampa warioba na viongozi wengine na alipofika kwa makonda amempa mwengine na hakumpa makonda.
Maalim Seif hajamruka angalia vizuri video, au tafuta video iliyokamilika..
 
Kahakikisha Lemutuz kampost saa anapeana mkono na baba yake kipindi anaenda kupanda gari aondoke. Bashite imembidi akimbilie mbele ili apate ya kupost. Poor him binadamu wa mtandaoni wanamuendesha sana.
 
Taharuki kila upande yaani ukimuangalia katika hii video baba swalehe alikuwa anajiandaa kuushika ule mkono kwa ile heshima ya kupunguza kimo kidogo lakini jamaa akapindisha, nadhan ni vile baba swalehe alivyompeleka Idrissa muigizaji kituo cha polisi
 
Je alishafanyiwa uchunguzi wa kina kubaini kama sumu bado ipo mwilini ama la??
 
kuna mimtu mingine kama michawi vile! Walishasalimiana hapo kabla na sasa alikuwa anasalimiana na wale aliokuwa bado kusalimiana nao!
 
Well said
 
Mfano Yusuph angekuwa Hai angefanya kitendo kama chake cha kwenda Dodoma na kina nyaulingo heri kisanduku cyprian Musiba na kikundi chake kumpiga Risasi Tundu Lisu?
Hivi Makonda anajisikiaje anapohusishwa kwa uwazi namna hii na kushambuliwa kwa Lissu?
Hivi anajipangaje maana anaye mbeba uwezekano wa kuiacha ofisi mwakani upo, na kama nguvu ya Gamboshi inaweza kutuliza mambo 2025 mwisho nayo haiko mbali!
Huwezi kutajwa kwa nguvu namna hiyo na ukawa unasingiziwa, we nani hadi usingiziwe?
 
Swali zuri. Naamini Bashite huwa anaiingia humu ukumbini, itakuwa vema akatujibu huo u Yusuf wake.
Wako watu wa kulinganishwa na Yusuf siyo Bashite, ni ukosefu wa kuijua Biblia. Bashite analinganishwa na Isaac Maliyamungu yule mshirika na Iddi Amin Dada wa Uganda 1971-1979, ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kuua na kutesa wakosoaji wa Iddi Amin. Soma hapa:
 
pantheraleo,
Hili tukio ni la kupangwa kabisa, maana hata Makonda mwenyewe anaonekana wazi kuwa alijiandaa kwa hilo maana hata yeye hakuuinua mkono wakati rais akielekea uelekeo wake.
Kwa jinsi picha likivyo basi hata kama rais angeinua mkono basi Makonda asingeuinua. Hilo picha limetengenezwa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…