Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu

Kama Mimi ndo wewe nisingesimulia maana ni aibu!! Kama hujatunga story basi huna aibu mzee. Mwanamke unamuombaje msamaha na hayupo kwako Bali na yote akamtukana mzee wako Bado unaimba msamaha?

Miaka 35 Bado hujawa mwanaume na anafanya hayo yte anajua udhaifu wako 100% kwamba huna maamzi na ulikuwa una mtegemea yeye kukuamlia hata hapo kwako!!

Manyanza
 
RULIWAAMBIA MSIOE WANAWAKE WENYE AJIRA NI VIBURI NA JEURI HAMSIKII, eti mnatafuta wa kusaidiana maisha haya kula chuma hiyo.

Hivi kweli mwanaume mwenye timamu kichwani unaenda kuoa lifeminist unategemea nini, hivi unadhani ungeoa mama wa nyumbani angekupelekeaha mpaka mahakamani, mapolisi, madawati ya jinsia nk ?!!!
 
Pole sana ndugu... huyo mwanamke hakufai na si mkeo tena huyo!!! Pili achana na dhana ya shiriki ktk hili unless kama we ni mkali na muumini wa hayo mambo ila kiuhalisia ni kupoteza mda na pesa zako bure.... mwanamke umezaa nae watoto wanne, mwache aende na mpe talaka yake!!! Usimuzuie mtu anayetaka kwenda na kuhusu polisi, tafuta msaada wa kisheria ili kuepukana na usumbufu na kero ya kupotezewa mda wako!!! Mwisho kabisa, kuwa jasiri na weka msimamo... umekosea sana pale ulipoanza kuomba radhi na pale ulipokiri kumchapa kama kosa!!!
 
Waafrika na ujinga ni kama kopo na funiko,
Mtu unasema amefanya makosa ya kutokuwa mwaminifu dhidi yako,ukampiga ametaka muachane bado unamngangania wa nini sasa.unacho ogopa ki loose ni nini nyumba ua gari??
Huyo mwanamke amisha kuwa adui kwako,mpe talaka yake kila moja achukue njia yake.Sio kila moja anabalikiwa kuwa na ndoa nzuri hapa Duniani.

Wewe ukipewa kitu fulani mwenzio naye atapungukiwa kitu fulani,tujifunze ku accept mambo mengine.
 
Ukishaharibikiwa kabisa ndo utajua jamaa kaona mbali,Huyo mkeo atakumaliza beba Kila silaha kummaliza.
 
Bonge la ushauri wifi, afate huu ushauri wala asijichoshe na huyo mwali kigego..!!

Huyo akili zinafyatukia ukubwani, mume mwenyewe mpole km ana hasira sana si angemrudishia hata na mwiko wa ugoko..!! 😹😹😹
 
35 mwanaume bado mdogo kabisa...mpe anachotaka..talaka..mali...watoto..najua kwa watoto patauma sana ila do that..alaf ondoka maishani mwao kaa kimya kama hau exist duniani wakati huo pambana na maisha na mafanikio yako...
Ukimya wako utamuumiza sana sana...akili ikija kumkaa sawa mbona atarud kwa magoti!!! Anadhani kulea watoto wanne bila baba yao mchezo?? Ata kama yuko financially capable trust me hiyo shughuli sio ndogo.
 
Kama unasema wewe unaamini katika Yesu basi ingia kwa maombi
 
Huyo “rafiki” yako sio mzuri na pengine yeye ndio mharibifu wa mambo yako. Ogopa sana mshirikina yeyote na yule anayejifanya kujali mambo yako kuliko wewe mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…