Ndio, amegundua Watanganyika ni mazuzu kwenye kutetea maslahi yao.Huyu Rais. Tuliyenae anatumia vibaya nafasi yake kuinufaisha Zanzibar.
Lakini hata bila Samia Tanganyika bado imekuwa ikibakwa siku zote kwenye huu Muungano.
Balozi Ali Karume katika huu uamsho wake mpya wa kisiasa kasema Mu-Unguja hawezi hata kupata ardhi Pemba, anabaguliwa, lakini akienda Bara hakuna maswali, ardhi ubwete, Zanzibar kasema inafaidi Muungano. Akatahadharisha kwamba siku Watanganyika wakiamka usingizini "wakalichekecha," Zanzibar itakoma kuringa. Ally Karume huyo, wazi wazi.
Tanganyika na vichwa vyetu vizito kipi hapo bado hatukielewi kuhusu mzigo wa Muungano?