Nguruvi3 ,
Mzee Mwanakijiji Pascal Mayalla na wajumbe wengine wa JF. Karibuni.
Kumradhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Kuna mengi, unaliliona ni sehemu tu. Tatizo ni kizazi kilichopo. Huko nyuma yalitokea haya:
Zanzibar wakata Bara watumie passport. Bara wakasema waje na passport, tangu siku hiyo hakuna tena hoja
A.H Mwinyi akawa anachota mapesa na kuyapeleka Zanzibar, akina Jenerali na G55 wakataka Tanganyika
Historia inajirudia. Kuna masuala yasiyo ya muungano sasa yanafanywa ya muungano.
Mfano, Utunzaji wa nyaraka si suala la muungano kila upande una mamlaka zake.
Mwaka jana Rais Samia kasema mkutano ufanyike Zanzibar, na umefanyika. Lengo ni kupeleka watu zaidi ya 400 kukuza uchumi. Ikiwa ni lazima, ni rahisi kuleta Wazaz 20 . Ndivyo mikutano inavyofanyika siku hizi .
Historia ya Mwinyi inajirudia lakini Samia kapania zaidi, yaani Zanzibar inapewa rasilimali kuliko Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Dar, Mbeya n.k.
Kero za muungano zinamalizwa na Wazanzibar wenyewe Rais Samia na Mwinyi.
Hakuna anayesimamia masilahi ya Tanganyika. Mpango ni rubber stamp tu
Philipo na Maja hawana kauli wanavizia kama zamu yao itafika.Wanapenda masilahi yao kuliko ya Tanganyika.
Ndivyo waziri Makamba anasamehe deni la umeme Zanzibar ili tozo alipe Mtanganyika.
Zanzibar ina watu 1.5 Milioni, na zaidi ya nusu wanaishi bara wakitumia resource za bara kama Elimu.
Bajeti ya muungano inahudumia Wazanzibar walioko Bara bila kubagua.
Mkoa wa Dar es Salaam una watu 6 Milioni , bajeti yake ya elimu ni ndogo kuliko ile ya Zanzibar
Mkoa wa Mwanza una DGP kubwa nchini kwa mujibu wa BoTresorce inazopata ni ndogo kuliko Zanzibar
Mkoa wa Kigoma una watu zaidi ya Zanzibar, bajeti yake ya elimu haifiki hata nusu
Wizara ya ulinzi ina bajeti ya 2.7 T na Bajeti ya Zanzibar ni 2.7 T.
Ikiwa Zanzibar wanaweza kuwa na bajeti ya elimu ya 457B wanashindwaje kuhudumia Wabunge Dodoma?
SMZ inasema hekta 6000 za Makurunge Bagamoyo ni za Wazanzibar. Ali Karume katihibitisha Baba yake aliomba eneo. Kwa historia Makurunge walipewa wafuge ng'ombe. Kauli ya SMZ haikutoka bila msaada wa Rais wa JMT!
Orodha inaendelea, hivyo kusema bajeti yao ya elimu ni kubwa kuna walakini. Ni sawa kabisa kwasababu Wazanzibar hawana bajeti ya Ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje, na Taasisi zote na wanapata 4.5% ya GDP ya Tanganyika kwa jina la muungano. Ile mikopo wanayopewa anayelipa ni Mtanganyika
Kasome katiba ya 1977, Tanganyika ndiyo Tanzania bara, halafu kuna Tanzania visiwani na Tanzania Zanzibar. Kinachoshindwa kuainishwa ni mambo ya Tanganyika kwa uwazi. Kuna Wapuuzi wa Zanzibar wakiongozwa na OM wanasema Tanganyika haipo! ipo lakini mambo yake yameporwa na neno muungano
Kinachotakiwa kwa Watanganyika si kulalamika au kutegemea viongozi au Wabunge.
Watanganyika chukueni hatua za kutoridhika kama nilivoonyesha vizazi vya miaka hiyo.
Bila kuwa na Tanganyika hakuna atakayesimamia masilahi yenu, na itafika mahali watu wa kule wanalipwa kwa kulala kwa kodi za Tanganyika. Hata sasa hivi kufanya kazi si lazima, bili kama za umeme zinalipwa huko Bara. Kwasasa wazee wanalipwa pensheni? Kwa uchumi upi ?
Kama kuna ulazima wa muungano lazima iwepo Tanganyika na mambo yake yawe wazi na kuwa na viongozi wanaosimamia masilahi ya Tanganyika. Warioba aliona, akaandika draft ya katiba! turudi kule
Mchambuzi JokaKuu Mag3