Msiache kuiomba mizimu yenu, hii ndo njia rahisi ya kufanikisha mambo


Tatizo la waafrika hasa watanzania, Kitu ambacho hawakifahamu au maarifa ambayo hawayafahamu, Wana hitimisha kuita uchawi.

Ukiwauliza uchawi ni nini?

Na wanathibitisha vipi ni uchawi?

Hawajui.
Kutokujua jambo sio kutokuwepo kwajambo hilo
 
Ukoo wako ni wa yesu umeshajitanabahi hivyo bwege wewe huwezi ukawatumikia mabwana wawili nyau wewe
Ila sioni kama njia ya kutukanana ni nzuri katika kujifunza , kupishana na mtu kuwa na mtazamo tofauti hiyo ni kawaida na sio lazima kila mtu aunge mkono wazo lako🙏
 
Kila Kabila au Ukoo zinataratibu zake za kuombea mizimu,wewe muumini wa hizo mambo nenda kawaone wazee wako wa Ukoo.
 
Kutokujua jambo sio kutokuwepo kwajambo hilo
Jambo linaweza kuwepo ila watu wakawa hawana uelewa nalo na namna lilivyo wakaishia kuamini ni uchawi tu , wenzetu wangekuwa wanatoa conclusion za namna hiyo ungekuta hakuna ugunduzi wowote .
 
Hata sasa Bwana amefanya....
Wote tuseme Haleluyaaa
 
Naunga mkono hoja, mimi ni Kuhani Mkuu wa mizimu yote ya milima ya Uluguru, karibuni kwa ibada na utakaso.
 
Vijijini wanaomba mizimu kila siku na wanazidi kuwa maskini
Umasikini ni relative term mkuu.

Unatumia vigezo vya wazungu kujua huyu masikini na huyu tajiri.

We mtu akila mihogo na mboga za majani za kuchemsha chuku chuku unamuona masikini kulinganisha na anaekula baga sio?

Mtu akikaa kijijini na familia yake ya watoto 6 nyumba ya kawaida very natural analima anakula vitu fresh kabisa anavuta hewa safiiii unamuona masikini compared na mtu anaishi mjini kapanga chumba ghorofani anakaa na mkewe na katoto kamoja wanaamka saa 11 kila siku kukimbizana na foleni barabarani wako busy hatari wanarudi nyimbani saa 2 hoi! wanalala saa nne miili haifai mchana wanaishia take away za chips, kwako wewe huyu ndio tajiri sio?
 

Wewe unamuomba mzimu wa aina gani? Unamuomba kwa kutumia utaratibu gani? Unaweza kuandika mtitiriko wa ibada ya kuomba mizimu ikoje, ili watu waelewe?
Na mwisho, sadaka unayoitoa ni ya aina gani?
 
mi najua mizimu ni majini yanajivika taswira ya marehemu na kujifanya roho ya marehemu
lengo ni kudanganya na kujinyakulia waumini wa shetani
Ok. Mimi kwa upana zaidi naona MIZIMU ni mikataba (maagano) waliyoingia mababu na majini. Na kwa kuwa mababu wenyewe washakufa na mkataba unaendelea kusoma. Majini yanaexecute yale ambayo yanatakiwa kufanyika. Mfano binaadam wasipotoa sadaka waliyokubaliana, wanapata madhara stahiki (penalty). So Mizimu ni mambo ya kujitakia yaliyosababishwa na tamaa na ujinga wa mababu.
Na ndio maana unakuta sio kila jamii ina hayo mambo ya mizimu. Kuna wengine hawakuingia hayo maagano. Ila kwa wale ambao waliingia ndio shida haziishi.
 
naona tunakubaliana ni majini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…