Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Mlaleo,Alifutwa kwa kuwa hakuwa na adabu hivyo upuuzi wake wa kuleta udini ndio sababu kuu.... hata wewe utafutika kwasababu ya udini udini wako kwanza unachosha tu
Hapana haja ya kutukana.
Tunaweza tukafanya mnakasha wa ustaarabu watu wakatusoma na faida na tija vikapatikana.
Najua ni kwa kiasi gani wengi mfano wa wewe wanavyochomwa na historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika kama nilivyoiandika.
Lakini huu ndiyo ukweli.
Ikiwa nachosha hujalazimishwa na mtu kunisoma ungeweza kunipita wima tu ukasoma hayo yasiyokuchosha.
Hii ni historia wala hakuna dini popote unajitisha pasi na sababu.
Ama kuwa nitafutika si rahisi.
Madhali nimeandika In Shaa Allah watakaokuja baada yetu watanisoma.
Wewe ndugu yangu ndiyo ushafutika hata kabla hujaandoka duniani.
Angalia mimi nikiingia kwenye uzi mnavyojazana kunisoma.
Nani leo ajae kukusoma wewe?