Msiba wa George Kahama wamkumbusha Mhariri wa Raia Mwema, Abdulwahid Sykes

Msiba wa George Kahama wamkumbusha Mhariri wa Raia Mwema, Abdulwahid Sykes

Na hii nayo ni Pwani:

"Hapo Makao Makuu ya CCM Dodoma ziwekwe picha za Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Edward Mwangosi, Tanga zikwekwe picha za Abdallah Rashid Sembe, Bi. Mwanamwema, Hamisi Heri. Lindi picha za Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Yusuf Badi. Kilimanjaro waweke picha za Eikaeli Mbowe, Yusuf Olotu, Juma Ngoma, Mama Biti Maalim, Halima Selengia." - Mohamed Said.
Ndio bibi Tanga na Lindi ni Pwani.

Kaingiza hiyo mikoa mingine kufunika kombe tu mwana haramu apite..

Ingekua Wahindi ndio wa Kwanza kuja Pwani ya Afrika Mashariki wewe na Mzee Said mngekua mnashubalia Wahindu wawekwe kwenye Historia.
 
uho85zSY51TvwDNhukm1-qw8Ps5P-cH5vBfx_ATJWLWrgobedeL4YiMZAiCX8L7nv50KLdt9rosSoioMBMltqJYikid8b7XhmkVKx0mU2ptd5piTZivpuuSRObVQLVWAMWS3WrfrVrMc2XtRur8OuuuT97YvDCz_FLbmAfADpmxz59XfhPBkEHvoA6Pe8NW9UGXxyzPVVUsVR_B6Imj1uPwacYrBvuxyxk6YnFQLYXTiQ387YskRmlPP0aXHpbaTvnwsj3sIN2na5oDGNCm433TFEJFWZXu-dQ5234WjqER_5nthekIXNRQVEk6qbFchotMcEVXQEntwaeg2UByEtQ8ESg-MzDFzVOf2JGX_JCsgD3iM2OSAoG9-YPxk9CqjDFcvSHyIY79F0KMEanispoSpMVplT6jsk0oYvODo78bG7WbwKnxX_WRX-gE0U6-jxcHTumcRbNiILVzuaHhedx8_8MzX243L4o4_yewpvqMnlTOvpElOPGEi6q1tXQo5eW-Vum1RgBVtjfLuQs0s_h2xESUpSz5gLAPZJxPJo823xnDQ_UivReb3867uVTKsPY6mS3euGFNt9N4eMy5_qovrv8gXJhkwcRPWCeeJMOcfCXb8Nw=w299-h692-no


Mhariri wa Raia Mwema katika toleo lake la 15 - 21, Machi 2007 katika tahariri yake kwa kumuadhimisha marehemu George Kahama aliyezikwa jana ameeleza masikitiko yake kwa Tanzania kutokuwa na historia ya mashujaa wake. Mhariri kamtaja pamoja na wazalendo wengine Abdul Sykes kama mmoja wa wazalendo ambae historia ya mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika bado haujathaminiwa.

Binafsi nimefarajika kuwa kumbe si mimi peke yangu ninayoona upungufu huu katika taifa letu.

Mara ya kwanza mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events lililokuwa likichapwa London lilipochapa makala yangu, ''In Praise of Ancestors,'' na nikamtaja marehemu Abdul Sykes kwa sifa ya kuaisi chama cha TANU 1954, toleo zima lilikusanywa na kutolewa katika mzunguko.

Mambo hayakuishia hapo toleo la gazeti hilo lililofuatia ilichapwa barua kutoka CCM Makao Makuu Dodoma iliyoandikwa na kada mashuhuri wa wakati huo na aliyekuwa na cheo kikubwa katika Sekretariati ya Kuhamasisha Umma iliyokuwa na vitisho na dharau dhidi yangu. Kisa na kosa langu kumtaja Abdul Sykes na wazalendo wengine na kusema kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika haiwezi kutenganishwa na mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Alipokufa Dossa Aziz katika maziko yake Mlandizi hakuna katika viongozi wa CCM aliyekuwapo pale mazikoni aliyejua Dossa alikuwa nani kwa Mwalimu Nyerere wala kwa TANU yenyewe na kwa bahati mbaya sana Nyerere hakuhudhuria maziko yale. Labda angekuwapo angemueleza Dossa alikuwa nani kwake na kwa TANU.

Alipokufa Paul Bomani mambo hayakuwa tofauti na yale ya maziko ya Dossa Aziz. Hakuna katika viongozi wa CCM aliyejua mchango wa Bomani.

Hawa wazalendo watatu niliowataja hapa kwa uchache wote wanaunganishwa na sifa moja adimu sana. Hawa walitajirika katika ukoloni na TANU ilipoasisiwa walikuwakuwa tayari wana na fedha zao. Hawa hawakutajirikia katika TANU. Wazalendo hawa walitoa fedha nyingi kwa TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa kuhitimisha ningependa kusema kuwa hakika nimefarajika sana kuwa kumbe kuna wenzagu na wao wameona upungufu wa jambo hili.

Kwa kuitika mwito wa Mhariri wa Raia Mwema itapendeza kama katika jengo jipya la CCM pale Patrice Lumumba Avenue CCM ikaanza kutafuta historia ya mashujaa wetu na kuwaenzi angalau kwa kuweka picha zao na maelezo mafupi.

Kizazi hiki cha leo kingependa kuona picha ya Sheikh Suleiman Takadir na maelezo yake ya mchango wake katika kudai uhuru wa nchi yetu, picha ya Saadan Abdul Kandoro, Hamza Mwapachu, Bi. Titi Mohamed na Tatu biti Mzee, Iddi Faiz Mafungo, Mshume Kiyate kwa kuwataja wachache na huko mikoani na wilayani haya yafanyike.

Hapo Makao Makuu ya CCM Dodoma ziwekwe picha za Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Edward Mwangosi, Tanga zikwekwe picha za Abdallah Rashid Sembe, Bi. Mwanamwema, Hamisi Heri. Lindi picha za Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Yusuf Badi. Kilimanjaro waweke picha za Eikaeli Mbowe, Yusuf Olotu, Juma Ngoma, Mama Biti Maalim, Halima Selengia.

Bukoba waweke picha za Ali Migeyo, Suedi Kagasheiki, Abdallah Rutabanzibwa nk. nk.

Tusitishike na majina haya ya Kiislam kwani hii ndiyo historia yenyewe hatutoweza kuibadili.
Kina Germanus Pacha nadhani wako wengi! Lakini hii huenda inatokana na hulka ya Viongozi wazamani hawakupenda makubwa. Nakumbuka mama mmoja aliyefariki karibuni hata alipopewa uongozi na Mwalimu Nyerere alisema mimi sikupigania Uhuru kwa ajili ya kupata uongozi bali nilipenda nchi iwe huru baaasi. Tusitoe sana lawama Ni jukumu letu basi sisi tutafute hiyohistoria tena sio kwa kuwa biased na kuihifadhi kwa ajili ya vizavi vijavyo hata kama wao hawakutegemea haya.
 
Nini Maana ya kuwa chini ya udhamini?
Je Tanganyika ilikuwa Koloni la Uingereza?,
Je wakti ule Wajerumani wameshindwa vita na kunyanganywa Makoloni yao, sisi (Tanganyika) tungekuwa tayari tungepewa uhuru?

Hope hukunielewa nilipokwambia Tanganyika tulishakuwa huru mara baada tu ya Mjerumani kishindwa vita
Kituko...
Historia hiyo yako ni mpya.
Nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru ni Ghana 1957.

Ingekuwa tuko tayari kujitawala wala Afrika isingevamiwa
na mataifa ya nje kupitia Mkutano wa Berlin.

Lakini ikiwa wewe unapenda kuamini kuwa Tanganyika
ilikuwa nchi huru 1918 hapana neno.
 
Nini Maana ya kuwa chini ya udhamini?
Je Tanganyika ilikuwa Koloni la Uingereza?,
Je wakti ule Wajerumani wameshindwa vita na kunyanganywa Makoloni yao, sisi (Tanganyika) tungekuwa tayari tungepewa uhuru?

Hope hukunielewa nilipokwambia Tanganyika tulishakuwa huru mara baada tu ya Mjerumani kishindwa vita
Kituko...
Kama nilivyoliahidi jamvi naweka hapa link baada ya utangulizi huu
historia ya Dk. Vedasto Kyaruzi:

Katika miaka hii ya karibuni nimesoma makala kadhaa ambazo Dk.
Kyaruzi
akifanyiwa mahojiano na waandishi wa magazeti tofauti na
katika kila makala Dk. Kyaruzi hakuacha kuweka msisitizo kuwa yeye
ndiye aliyemuachia TAA Nyerere.

Hiki ni kitu ambacho mimi kama mtafiti na mwandishi wa historia
ya uhuru wa Tanganyika kilikuwa kikinitaabisha sana. Kilichokuwa
kikinipa shida ni kuwa nilikuwa nikifahamu kuwa Dk. Kyaruzi aliingia
katika uongozi wa TAA mwaka 1950 pamoja na Abdulwahid Sykes.

Nilikuwa najua kuwa waliomsaidia kuingia katika uongozi walikuwa
watu wa mjini akina Plantan na Sykes.

Vipi watu hawa hakuwa anawakumbuka?

Wakati Nyerere anachukua uongozi wa TAA mwaka 1953 Kyaruzi
hakuwa Dar es Salaam.

Hiki ni kitu kikinishughulisha sana.

Jambo hili likishighulisha sana fikra zangu kwa kujiuliza mbona Kyaruzi
anamruka Abdulwahid Sykes katika historia yao ya uongozi wa TAA
mwaka wa 1950 na kumwingiza Nyerere ilhali Nyerere wakati ule hakuwa
anafahamika na yeyote katika duru za siasa za Tanganyika?

Nikawa nashangaa nikijiuliza kwani Dk. Kyaruzi hajui kuwa Nyerere aliingia
katika uongozi wa TAA mwaka 1953?

Nilikuwa nikijifariji kwa kusema kuwa haya ndiyo matatizo ya historia ya
uhuru wa Tanganyika.

Lakini jambo linalonisikitisha sana ni kujua kuwa katika miaka ya 1970 Dk.
Kyaruzi
alipeleka mswada wa maisha yake kwa mchapaji mmoja wa vitabu
ili mswada wake uhaririwe na kuchapwa kitabu.

Mchapaji yule ambae lilikuwa shirika la umma lilikataa kuchapa kitabu kile.

Sijui kwa nini walikataa kuchapa kitabu kile ambacho kwa hali yeyote ile
ingelikuwa hazina kubwa kwa vizazi vijavyo na hii leo wakati wa umauti
wake tungelimjua bila wasiwasi Dk. Kyaruzi na mchango wake katika
uhuru wa Tanganyika na jinsi kama alivyosema mwenyewe vipi alimwachia
TAA Nyerere.

DK. VEDASTO KYARUZI DAKTARI MWANAHARAKATI WA TAA
 
Kituko...
Historia hiyo yako ni mpya.
Nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru ni Ghana 1957.

Ingekuwa tuko tayari kujitawala wala Afrika isingevamiwa
na mataifa ya nje kupitia Mkutano wa Berlin.

Lakini ikiwa wewe unapenda kuamini kuwa Tanganyika
ilikuwa nchi huru 1918 hapana neno.

Si nimekuuliza hayo maswali hapo juu, mbona huyajibu, yajibu kama nilipokuuliza
 
Al Watan,
Historia ya George Kahama naifahamu vyema ila nachelea kuiweka hapa kwani ukweli inagusa kipindi kilicholeta mtafaruku mkubwa katika TANU baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu 1958.

Nakushauri usome historia hii katika kitabu cha Abdul Sykes.
Ahali yangu hicho kitabu kipo bookshops? Bookshop gani? Vingine kama hicho ni vipi? Nikombali na nyumbani lakini naweza kuwatuma wadogo zangu wanitafutie hapo Dar wanitumie.

Nielimike zaidi.Nawe utapata royalties pia.
 
Si nimekuuliza hayo maswali hapo juu, mbona huyajibu, yajibu kama nilipokuuliza
Kituko,
Huwa maswali mengine huyaacha yapite na kisa ni kuwa
mie siko katika mabishano na yeyote awaye yule.

Nikinyanyua kalamu basi huwa kusomesha.

Nimeeleza kwa kirefu dhana ya Mandate Territories katika
kitabu cha Abdul Sykes.
 
Kituko,
Huwa maswali mengine huyaacha yapite na kisa ni kuwa mie siko katika mabishano na yeyote awaye yule.

Nikinyanyua kalamu basi huwa kusomesha.

Asante kwa kunielewa nilichokuwa nakimaanisha
 
Ahali yangu hicho kitabu kipo bookshops? Bookshop gani? Vingine kama hicho ni vipi? Nikombali na nyumbani lakini naweza kuwatuma wadogo zangu wanitafutie hapo Dar wanitumie.

Nielimike zaidi.Nawe utapata royalties pia.
Al Watan,
Kitabu kipo Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema
na Mtoro pia soma Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru cha
Dr. Harith Ghassany na ''Conflict and Harmony'' in
Zanzibar cha Ali Muhsin kuhusu historia ya Zanzibar
na Mapinduzi.
 
Al Watan kitabu kipo Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema na Mtoro pia soma Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru cha Dr. Harith Ghassany na Conflict and Harmony cha Ali Muhsin kuhusu historia ya Zanzibar na Mapinduzi.
Cha Dr. Ghassany nilikisoma kilipotoka. Kimeanza complacent halafu kikawa na a very provocative point of view that does not get discussed often.

Hivo vingine viwili nitavitafuta.
 
Cha Dr. Ghassany nilikisoma kilipotoka. Kimeanza complacent halafu kikawa na a very provocative point of view that does not get discussed often.

Hivo vingine viwili nitavitafuta.
Al Watan,
Ahsante kingine ni ''Propaganda za Udini Tanzania,''
cha Prof. Ibrahim Noor Sharif.
 
Ndio bibi Tanga na Lindi ni Pwani.

Kaingiza hiyo mikoa mingine kufunika kombe tu mwana haramu apite..

Ingekua Wahindi ndio wa Kwanza kuja Pwani ya Afrika Mashariki wewe na Mzee Said mngekua mnashubalia Wahindu wawekwe kwenye Historia.

Kagasheki wa Pwani?
 
Kituko,
Mimi niko katika Cambridge Journal of African History.

Niko katika Dictionary of African Biography (DAB) na utanikuta
kwingi Oxford University Press.

Makala zangu zimechapwa na magazeti makubwa kama New
African na Africa Events na nikiandika na Africa Analysis na mara
moja nimechapwa na The Economist.

Miaka mingi sana imepita wakati nafanya haya.
Unataka kunambia hawa wanachapa stori za barzani?

Na hawa hawa wote wananitambua kama mtafiti na
mwandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika na siasa
za Tanzania.
Nashukuru kwa unayo yazungumza.

kuna mzee aliye mtoa Nyerere makerere ama alisoma naye sijakumbuka vyema kwa jina nahisi Rwegasira...achana na balozi alofariki majuzi, huyu amefariki miaka kama 5 hivi...je ni akina kagasheki tu kwa Bukoba waliopigania uhuru?

secretary general to buhaya council akina rwamugila, zahoro hawakuwa na mchango?

Ntafurahi ukinijibu, binafsi nipo hapa kujifunza
 
Iceman,
George Kahama
mimi nimemweleza vizuri vipi aliingia TANU na katika
Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1958 pamoja na Chifu Abdallah Said
Fundikira, Enesmo Eliufoo, Lawi Sijaona, Paul Bomani, John Keto,
John
Mwakangale na Lawi Sijaona.

Haya yapo katika kitabu cha Abdul Sykes.

Sijaweza kuwa na ujasiri wa kuandika taazia ya George Kahama kwa
namna hao hapo juu kuja TANU baadhi yao 1958 wakiwa wamechelewa
lakini Mwalimu Nyerere akawateua kuingia katika Baraza la Kutunga
Sheria 1958 kulivyozusha ugomvi ndani ya TANU kati ya Sheikh Takadir
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na Julius Nyerere.

Hii ni historia hata Nyerere mwenyewe akiiogopa kuitaja.

Ndiyo maana hutosoma popote kisa cha Nyerere na Sheikh Suleiman
Takadir
.

Imetokea kuwa mimi ndiyo matafiti wa kwanza kumtaja Sheikh Suleiman
Takadir
katika historia ya TANU.

Mambo kama haya ndiyo yalinifanya nijizuie kuandika.
Hakuna apendae kusoma taazia iliyojaa mapambano.
Nimenunua Vitabu vyako vya hiyo historia ntajitaidi nivisome
 
Nashukuru kwa unayo yazungumza.

kuna mzee aliye mtoa Nyerere makerere ama alisoma naye sijakumbuka vyema kwa jina nahisi Rwegasira...achana na balozi alofariki majuzi, huyu amefariki miaka kama 5 hivi...je ni akina kagasheki tu kwa Bukoba waliopigania uhuru?

secretary general to buhaya council akina rwamugila, zahoro hawakuwa na mchango?

Ntafurahi ukinijibu, binafsi nipo hapa kujifunza
Dr. Akanyonyi,
Watu wengi wamechangia katika jitihada za kupigania uhuru
wa Tanganyika lakini bahati mbaya michango yao haitambuliwi.

Endapo nisingeliandika kitabu hcho cha Abdul Sykes historia
kubwa ingepotea.

Binafsi sina taarifa za Rwamugila au Zahoro katika TANU.

Kwa kuwa wewe unayo hayo majina jaribu kufanya utafiti tuwajue
watu hawa.
 
Kituko,
Mimi niko katika Cambridge Journal of African History.

Niko katika Dictionary of African Biography (DAB) na utanikuta
kwingi Oxford University Press.

Makala zangu zimechapwa na magazeti makubwa kama New
African na Africa Events na nikiandika na Africa Analysis na mara
moja nimechapwa na The Economist.

Miaka mingi sana imepita wakati nafanya haya.
Unataka kunambia hawa wanachapa stori za barzani?

Na hawa hawa wote wananitambua kama mtafiti na
mwandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika na siasa
za Tanzania.
Economist hili tunalolijua,au zamani kulikuwa na lingine tofauti- na hasa hiyo nakala uliyoandika ilikuwa inahusu nini??
 
Mohamed Said , keshaweka habari za Kyaruzi nenda kasome utaona ni paragraph mbili tu ndio zenye Kyaruzi, kwingine kote ni Sykes tu, mi sio mgeni na nyie Dada Faiza

Kituko,
Hebu msome hapo chini Dr. Vedasto Kyaruzi kama nilivyomueleza katika kitabu kizima cha Abdul Sykes bila kutia niliyoweka katika ''footnotes'':
  1. Lakini pamoja na yote hayo, wazee hawakutaka kuachilia madaraka. Jambo hili lilizusha mvutano baina ya wazee na wanasiasa vijana waliosomeshwa na himaya ya Waingereza. Vijana hawa walikuwa akina Abdulwahid na Ally Sykes, Tewa Said Tewa, Stephen Mhando, Dossa Aziz, James Mkande, na wale madaktari watano - Joseph Mutahangarwa, Luciano Tsere, Michael Lugazia, Vedasto Kyaruzi na wengineo. Haya yalikuwa ni mapambano baina ya kizazi kipya na kile cha kale.
  2. Mwezi Machi mwaka 1950, katika Ukumbi wa Arnatouglo, kijana wa Kihaya, Dr Vedasto Kyaruzi alichaguliwa kuwa rais na Abdulwahid Sykes katibu wake. [1]Walipokichukua uongozi, TAA ilikuwa na shilingi themanini na saba pekee katika Barclays Bank. Huu ndiyo ulikuwa mwisho wa wazee, kuongoza TAA. Vilevile mwanzo wa uzalendo nchini Tanganyika.
  3. Baadhi ya wanasiasa wakongwe wengine washirika wa marehemu baba yake kama Schneider, Mashado Plantan na Clement Mtamila walimuunga mkono yeye na Kyaruzi katika kuipa TAA uhai mpya.
  4. Jambo la kwanza alilofanya Abdulwahid mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA) [1] iliyomjumuisha yeye mwenyewe, Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika na Zanzibar; Dr Kyaruzi, Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwa liwali wa mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando. Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika.
  5. Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam chini ya Dr Kyaruzi na Abdulwahid ikiungwa mkono na kamati ya siasa sasa ilikuwa ikiamka kutoka kwenye usingizi mzito.
  6. Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo.[1] Katika taarifa yake ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika: ''Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria. Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi. Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba.''
  7. Kufuatia mwamko huu wa chama, serikali ilishtuka na ikaanza kuingia hofu, ikaamua kumpa uhamisho Dr Kyaruzi, rais wa TAA, kutoka Dar es Salaam kwenda Hospitali ya Gereza la Kingolwira karibu na Morogoro. Serikali ya kikoloni iliamini kwa kufanya hivyo itaweza kupunguza kasi ya TAA katika uwanja wa siasa.
  8. Serikali ilidhani kwa kumtoa Dr Kyaruzi Dar es Salaam, jambo hilo lingedhoofisha uongozi wa TAA pale makao makuu. Lakini Dr Kyaruzi hakuzuiliwa na huo uhamisho. Kila mwisho wa juma alisafiri Dar es Salaam kushauriana na Abdulwahid. Serikali ilipotambua kuwa uhamisho huo haukuathiri chochote katika mchango wa Dr Kyaruzi kwenye uongozi wa TAA, alihamishwa tena kutoka Kingolwira hadi Nzega mbali kabisa na Dar es Salaam. Hapo ikawa Dr Kyaruzi amepatikana.
  9. Baada ya Dr Kyaruzi kuhamishiwa Nzega nafasi ya rais ikawa wazi. Abdulwahid akakaimu nafasi hiyo sasa akiwa katibu na kaimu rais wa TAA.
  10. Watu wengine mashuhuri walioshauriwa na kuombwa kuunga mkono chama hiki walikuwa: Dr Joseph Mutahangarwa, Chifu Abdeli Shangali wa Machame, Chifu Mkuu Thomas Marealle wa Marangu, Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Haruna Msabila Lugusha, Dr William Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dr Vedasto Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K. Viran, Stephen Mhando, Ally Sykes na Dossa Aziz.
  11. Hili linaweza kueleweka ikifikirika kuwa ilikuwa ni miaka mitatu tu huko nyuma wakati Abdulwahid na Dr Kyaru
  12. zi walikifufua baada ya kupoteza mwelekeo baada ya Vita Kuu ya Pili. Iliamuliwa kuwa wazee Waislam wa mjini Dar es Salaam waombwe kumuunga mkono Nyerere.
  13. Kuanzia mwaka wa 1950 wakati Abdulwahid na Dr Kyaruzi walipochukua uongozi makao makuu walianza kutumia manungíuniko ya wananchi ili kujijengea uhalali wa kuwapo kama chama chenye kushughulikia maslahi ya watu wa Tanganyika.
  14. Ajenda ya kwanza kujadiliwa chini ya TANU tarehe 9 Julai ilikuwa lile suala la uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria. Katika mwaka 1950 itakumbukwa kuwa TAA, chini ya uongozi wa Abdulwahid na Dr Kyaruzi iliwakilisha memorandum kwa Gavana Twining kueleza mapendekezo yake juu ya mabadiliko ya katiba.
  15. Ally angefanywa kama vile Dr Kyaruzi mwaka wa 1951, alipokuwa rais wa TAA. Aliondolewa Dar es Salaam na kutupwa kwanza Kiongolwira na baadaye Nzega.
  16. Kufuatia majibishano haya kati ya TAGSA na serikali, Dr Mwanjisi kama Dr Kyaruzi kabla yake, alihamishwa kutoka hospitali ya Sewa Haji mjini Dar es Salaam hadi Kingolwira Prison Hospital karibu na Morogoro. Kawawa alipewa uhamisho kwenda Bukoba na Ally Sykes kwenda Mtwara. Ilikuwa wazi kwa uongozi wa TAA pamoja na TAGSA kuwa Uingereza ilikuwa bado haiko tayari kuwasikiliza Waafrika.
 
Back
Top Bottom