bukoba boy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 5,370
- 3,962
Ndio bibi Tanga na Lindi ni Pwani.Na hii nayo ni Pwani:
"Hapo Makao Makuu ya CCM Dodoma ziwekwe picha za Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Edward Mwangosi, Tanga zikwekwe picha za Abdallah Rashid Sembe, Bi. Mwanamwema, Hamisi Heri. Lindi picha za Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Yusuf Badi. Kilimanjaro waweke picha za Eikaeli Mbowe, Yusuf Olotu, Juma Ngoma, Mama Biti Maalim, Halima Selengia." - Mohamed Said.
Kina Germanus Pacha nadhani wako wengi! Lakini hii huenda inatokana na hulka ya Viongozi wazamani hawakupenda makubwa. Nakumbuka mama mmoja aliyefariki karibuni hata alipopewa uongozi na Mwalimu Nyerere alisema mimi sikupigania Uhuru kwa ajili ya kupata uongozi bali nilipenda nchi iwe huru baaasi. Tusitoe sana lawama Ni jukumu letu basi sisi tutafute hiyohistoria tena sio kwa kuwa biased na kuihifadhi kwa ajili ya vizavi vijavyo hata kama wao hawakutegemea haya.
Mhariri wa Raia Mwema katika toleo lake la 15 - 21, Machi 2007 katika tahariri yake kwa kumuadhimisha marehemu George Kahama aliyezikwa jana ameeleza masikitiko yake kwa Tanzania kutokuwa na historia ya mashujaa wake. Mhariri kamtaja pamoja na wazalendo wengine Abdul Sykes kama mmoja wa wazalendo ambae historia ya mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika bado haujathaminiwa.
Binafsi nimefarajika kuwa kumbe si mimi peke yangu ninayoona upungufu huu katika taifa letu.
Mara ya kwanza mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events lililokuwa likichapwa London lilipochapa makala yangu, ''In Praise of Ancestors,'' na nikamtaja marehemu Abdul Sykes kwa sifa ya kuaisi chama cha TANU 1954, toleo zima lilikusanywa na kutolewa katika mzunguko.
Mambo hayakuishia hapo toleo la gazeti hilo lililofuatia ilichapwa barua kutoka CCM Makao Makuu Dodoma iliyoandikwa na kada mashuhuri wa wakati huo na aliyekuwa na cheo kikubwa katika Sekretariati ya Kuhamasisha Umma iliyokuwa na vitisho na dharau dhidi yangu. Kisa na kosa langu kumtaja Abdul Sykes na wazalendo wengine na kusema kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika haiwezi kutenganishwa na mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Alipokufa Dossa Aziz katika maziko yake Mlandizi hakuna katika viongozi wa CCM aliyekuwapo pale mazikoni aliyejua Dossa alikuwa nani kwa Mwalimu Nyerere wala kwa TANU yenyewe na kwa bahati mbaya sana Nyerere hakuhudhuria maziko yale. Labda angekuwapo angemueleza Dossa alikuwa nani kwake na kwa TANU.
Alipokufa Paul Bomani mambo hayakuwa tofauti na yale ya maziko ya Dossa Aziz. Hakuna katika viongozi wa CCM aliyejua mchango wa Bomani.
Hawa wazalendo watatu niliowataja hapa kwa uchache wote wanaunganishwa na sifa moja adimu sana. Hawa walitajirika katika ukoloni na TANU ilipoasisiwa walikuwakuwa tayari wana na fedha zao. Hawa hawakutajirikia katika TANU. Wazalendo hawa walitoa fedha nyingi kwa TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kwa kuhitimisha ningependa kusema kuwa hakika nimefarajika sana kuwa kumbe kuna wenzagu na wao wameona upungufu wa jambo hili.
Kwa kuitika mwito wa Mhariri wa Raia Mwema itapendeza kama katika jengo jipya la CCM pale Patrice Lumumba Avenue CCM ikaanza kutafuta historia ya mashujaa wetu na kuwaenzi angalau kwa kuweka picha zao na maelezo mafupi.
Kizazi hiki cha leo kingependa kuona picha ya Sheikh Suleiman Takadir na maelezo yake ya mchango wake katika kudai uhuru wa nchi yetu, picha ya Saadan Abdul Kandoro, Hamza Mwapachu, Bi. Titi Mohamed na Tatu biti Mzee, Iddi Faiz Mafungo, Mshume Kiyate kwa kuwataja wachache na huko mikoani na wilayani haya yafanyike.
Hapo Makao Makuu ya CCM Dodoma ziwekwe picha za Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Edward Mwangosi, Tanga zikwekwe picha za Abdallah Rashid Sembe, Bi. Mwanamwema, Hamisi Heri. Lindi picha za Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Yusuf Badi. Kilimanjaro waweke picha za Eikaeli Mbowe, Yusuf Olotu, Juma Ngoma, Mama Biti Maalim, Halima Selengia.
Bukoba waweke picha za Ali Migeyo, Suedi Kagasheiki, Abdallah Rutabanzibwa nk. nk.
Tusitishike na majina haya ya Kiislam kwani hii ndiyo historia yenyewe hatutoweza kuibadili.
Kituko...Nini Maana ya kuwa chini ya udhamini?
Je Tanganyika ilikuwa Koloni la Uingereza?,
Je wakti ule Wajerumani wameshindwa vita na kunyanganywa Makoloni yao, sisi (Tanganyika) tungekuwa tayari tungepewa uhuru?
Hope hukunielewa nilipokwambia Tanganyika tulishakuwa huru mara baada tu ya Mjerumani kishindwa vita
Kituko...Nini Maana ya kuwa chini ya udhamini?
Je Tanganyika ilikuwa Koloni la Uingereza?,
Je wakti ule Wajerumani wameshindwa vita na kunyanganywa Makoloni yao, sisi (Tanganyika) tungekuwa tayari tungepewa uhuru?
Hope hukunielewa nilipokwambia Tanganyika tulishakuwa huru mara baada tu ya Mjerumani kishindwa vita
Kituko...
Historia hiyo yako ni mpya.
Nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru ni Ghana 1957.
Ingekuwa tuko tayari kujitawala wala Afrika isingevamiwa
na mataifa ya nje kupitia Mkutano wa Berlin.
Lakini ikiwa wewe unapenda kuamini kuwa Tanganyika
ilikuwa nchi huru 1918 hapana neno.
Ahali yangu hicho kitabu kipo bookshops? Bookshop gani? Vingine kama hicho ni vipi? Nikombali na nyumbani lakini naweza kuwatuma wadogo zangu wanitafutie hapo Dar wanitumie.Al Watan,
Historia ya George Kahama naifahamu vyema ila nachelea kuiweka hapa kwani ukweli inagusa kipindi kilicholeta mtafaruku mkubwa katika TANU baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu 1958.
Nakushauri usome historia hii katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kituko,Si nimekuuliza hayo maswali hapo juu, mbona huyajibu, yajibu kama nilipokuuliza
Kituko,
Huwa maswali mengine huyaacha yapite na kisa ni kuwa mie siko katika mabishano na yeyote awaye yule.
Nikinyanyua kalamu basi huwa kusomesha.
Al Watan,Ahali yangu hicho kitabu kipo bookshops? Bookshop gani? Vingine kama hicho ni vipi? Nikombali na nyumbani lakini naweza kuwatuma wadogo zangu wanitafutie hapo Dar wanitumie.
Nielimike zaidi.Nawe utapata royalties pia.
Cha Dr. Ghassany nilikisoma kilipotoka. Kimeanza complacent halafu kikawa na a very provocative point of view that does not get discussed often.Al Watan kitabu kipo Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema na Mtoro pia soma Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru cha Dr. Harith Ghassany na Conflict and Harmony cha Ali Muhsin kuhusu historia ya Zanzibar na Mapinduzi.
Al Watan,Cha Dr. Ghassany nilikisoma kilipotoka. Kimeanza complacent halafu kikawa na a very provocative point of view that does not get discussed often.
Hivo vingine viwili nitavitafuta.
Ndio bibi Tanga na Lindi ni Pwani.
Kaingiza hiyo mikoa mingine kufunika kombe tu mwana haramu apite..
Ingekua Wahindi ndio wa Kwanza kuja Pwani ya Afrika Mashariki wewe na Mzee Said mngekua mnashubalia Wahindu wawekwe kwenye Historia.
Si nimekuuliza hayo maswali hapo juu, mbona huyajibu, yajibu kama nilipokuuliza
Mohamed Said , keshaweka habari za Kyaruzi nenda kasome utaona ni paragraph mbili tu ndio zenye Kyaruzi, kwingine kote ni Sykes tu, mi sio mgeni na nyie Dada FaizaWewe nimekuuliza maswali mbona hukujibu ukababaisha?
Nashukuru kwa unayo yazungumza.Kituko,
Mimi niko katika Cambridge Journal of African History.
Niko katika Dictionary of African Biography (DAB) na utanikuta
kwingi Oxford University Press.
Makala zangu zimechapwa na magazeti makubwa kama New
African na Africa Events na nikiandika na Africa Analysis na mara
moja nimechapwa na The Economist.
Miaka mingi sana imepita wakati nafanya haya.
Unataka kunambia hawa wanachapa stori za barzani?
Na hawa hawa wote wananitambua kama mtafiti na
mwandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika na siasa
za Tanzania.
Nimenunua Vitabu vyako vya hiyo historia ntajitaidi nivisomeIceman,
George Kahama mimi nimemweleza vizuri vipi aliingia TANU na katika
Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1958 pamoja na Chifu Abdallah Said
Fundikira, Enesmo Eliufoo, Lawi Sijaona, Paul Bomani, John Keto,
John Mwakangale na Lawi Sijaona.
Haya yapo katika kitabu cha Abdul Sykes.
Sijaweza kuwa na ujasiri wa kuandika taazia ya George Kahama kwa
namna hao hapo juu kuja TANU baadhi yao 1958 wakiwa wamechelewa
lakini Mwalimu Nyerere akawateua kuingia katika Baraza la Kutunga
Sheria 1958 kulivyozusha ugomvi ndani ya TANU kati ya Sheikh Takadir
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na Julius Nyerere.
Hii ni historia hata Nyerere mwenyewe akiiogopa kuitaja.
Ndiyo maana hutosoma popote kisa cha Nyerere na Sheikh Suleiman
Takadir.
Imetokea kuwa mimi ndiyo matafiti wa kwanza kumtaja Sheikh Suleiman
Takadir katika historia ya TANU.
Mambo kama haya ndiyo yalinifanya nijizuie kuandika.
Hakuna apendae kusoma taazia iliyojaa mapambano.
Dr. Akanyonyi,Nimenunua Vitabu vyako vya hiyo historia ntajitaidi nivisome
Dr. Akanyonyi,Nashukuru kwa unayo yazungumza.
kuna mzee aliye mtoa Nyerere makerere ama alisoma naye sijakumbuka vyema kwa jina nahisi Rwegasira...achana na balozi alofariki majuzi, huyu amefariki miaka kama 5 hivi...je ni akina kagasheki tu kwa Bukoba waliopigania uhuru?
secretary general to buhaya council akina rwamugila, zahoro hawakuwa na mchango?
Ntafurahi ukinijibu, binafsi nipo hapa kujifunza
Economist hili tunalolijua,au zamani kulikuwa na lingine tofauti- na hasa hiyo nakala uliyoandika ilikuwa inahusu nini??Kituko,
Mimi niko katika Cambridge Journal of African History.
Niko katika Dictionary of African Biography (DAB) na utanikuta
kwingi Oxford University Press.
Makala zangu zimechapwa na magazeti makubwa kama New
African na Africa Events na nikiandika na Africa Analysis na mara
moja nimechapwa na The Economist.
Miaka mingi sana imepita wakati nafanya haya.
Unataka kunambia hawa wanachapa stori za barzani?
Na hawa hawa wote wananitambua kama mtafiti na
mwandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika na siasa
za Tanzania.
Mohamed Said , keshaweka habari za Kyaruzi nenda kasome utaona ni paragraph mbili tu ndio zenye Kyaruzi, kwingine kote ni Sykes tu, mi sio mgeni na nyie Dada Faiza