Msiba wa Mafuru wa leo Karimjee sijaona mnyonge

Msiba wa Mafuru wa leo Karimjee sijaona mnyonge

Hiyo ndio maana halisi ya neno MSIBA (FUNERAL CEREMONY)
-Vyakula mnakula kwenye mabufee
-Magari ya mazishi
-Wafiwa wamevaa full black nguo kali
-Ndugu na jamaa ni watu wazito
Wale wenzangu na mimi huwa tunaita KILIO
-Maji yakunawa yanapitishwa kikifuatiwa na Chakula ambacho unaletewa kwenye sahani wali,finyango mbili za nyama na maharagwe hawaelewi kuna watu wanaumwa madonda ya tumbo
 
Leo hayati Mafuru aliagwa rasmi na kiongozi wa kuaga alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ukigeuka huku kuna Joseph Kusaga, ukitazama kule kuna GSM, ukishangaa shangaa kuna Mawaziri, ukiinuka kidogo kuna Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, mara unamuona Jenerali Nkunda, kwa mbali unamuona CEO wa Kempinski na wengineo wa kariba hiyo.

Hakika kila mbuzi atakula urefu wa kamba yake!
MHUBIRI 2:16
Maana hakuna kumbukumbu la milele la mwenye hekima, wala la mpumbavu; kwa sababu siku zijazo wote pia watakuwa wamekwisha kusahauliwa. Na mwenye hekima, jinsi gani anavyokufa sawasawa na mpumbavu!
 
Hakuna la ajabu nashangaa kuona watu wanaongelea vibaya kama kuna maajabu. Hii mfumo wa maisha yetu hata wewe hapo ulipo kesho ukiwa millionare automatic marafiki zako watabadilika mtu anayebaki na wale wale huyo maisha yamemkwamisha hii ni kwa wote. Harusi zetu zina reflect hali zetu wanaokuja ni level yako sio misiba tu.

Watu wanaweza kuja kama wewe Millionare basi wengi watakuja matajiri wenzako, Kama wewe ulikuwa na cheo(sio ulazima utajiri) watakuja wenzako waliokuwa na maslahi na wewe, Kama wewe ulikuwa mtu maarufu kwa matendo yako mazuri watakuja wale uliowagusa. Ndio maana akifa msanii wanajaa wasanii. Sasa hapa ajabu nini? wewe hapo umekaa unafikiria nitalipaje kodi ya nyumba utegemee uje kuzikwa na kina GSM? kwa bahati nzuri asilimia kubwa sana ya watu wanazikwa na watu hata kuwajuwa huwajui. nenda misibani unaowajua utakuta wamesimama tuko story wanaofanya kazi kwenye kaburi ni mara ya kwanza kuwaona kama wewe ni ndugu unatizama.
 
Leo hayati Mafuru aliagwa rasmi na kiongozi wa kuaga alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ukigeuka huku kuna Joseph Kusaga, ukitazama kule kuna GSM, ukishangaa shangaa kuna Mawaziri, ukiinuka kidogo kuna Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, mara unamuona Jenerali Nkunda, kwa mbali unamuona CEO wa Kempinski na wengineo wa kariba hiyo.

Hakika kila mbuzi atakula urefu wa kamba yake!
Wewe pia haukuwa mnyonge kwenye shughuli hiyo ama ndiye mnyonge pekee uliyehudhuria?
 
Lukemia siyo HIV, usilete mambo ya hayati Mtikila.
Wanadhani HIV ingemuondoa kirahisi hivyo. Watu wana HIV na ni mafukara na wanadunda miaka. Achana na kansa, tena tuombe itupitie mbali. Hakuna ugonjwa unatesa kama ule. Bora yeye kaugua muda mfupi. Nimeuguza dada yangu na kansa ya ziwa, alikuwa anatamani kufa kuliko kuwa hai.
 
Kuna kiongozi mmoja kutoka ofcn kwetu baada ya kutoka kule Karimjee mshkaji mmoja akamuuliza mbona hawajasafirisha kwenda kuzika kwao, alichotuambia tu namnukuu "Jengeni kwenu, jengeni kwenu" mwisho wa kunukuu!!
Hizi ndizo pressures za kuwafanya watu waibe, halafu wakiiba mnawaita mafisadi.

Kwa Mtanzania, Tanzania nzima ni kwao. Acheni ulugaluga.
 
Wanadhani HIV ingemuondoa kirahisi hivyo. Watu wana HIV na ni mafukara na wanadunda miaka. Achana na kansa, tena tuombe itupitie mbali. Hakuna ugonjwa unatesa kama ule. Bora yeye kaugua muda mfupi. Nimeuguza dada yangu na kansa ya ziwa, alikuwa anatamani kufa kuliko kuwa hai.

Pole sana.

Kanza ya ziwa si mchezo mkuu.

Kuna mama alikuwa anapigwa morphine pale Ocean Road mpaka alipofariki unaona kapumzika.
 
Back
Top Bottom