Msiba wa mzee Mtei na heshima kubwa ya CHADEMA Tanganyika

https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/share/v/1Z1GNoNUpN/
 
CHADEMA punguzeni siasa uchwara msibani
Mumetumia mahakamani kuzuia Chadema kufanya siasa sasa kila tunapopata nafasi ya kuongea lazima tuongee siasa na kuwanyoosha nyie washenzi mlioshindwa kujibu hoja zetu na badala yake mnatumia mitutu ya bunduki. CCM imekoma kuwa chama cha siasa na kuwa genge maslahi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.
 
Kuhusu Hayo maneno ya Godbless.

Hapa hata ule "uswahili" unaosemwa, haufui dafu!

Hata ile fani ya 'sanaa 'komedi' ", haifui dafu!

Hawa ni majambazi wanaoua waTanzania halafu wanatunga hadithi za kuhalalisha maovu hayo.

Sasa, watu wa namna hii watashindwa jambo gani?

Labda nimueleweshe tu Lema kuhusu jambo dogo la umeme. Ni China ndiyo kinara wa umeme mwingi.
 
MZEE MTEI AMEZIKWA MWILI; FIKRA ZAKE ZIMEBAKI
Na Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza PhD

Jana 24/1/2025, taifa limeuzika mwili wa Mzee Edwin Mtei (94). Ana historia inayogusa sekta nyingi hapa nchini. Watu wa namna hiyo huwa ni kama moto ambao hufa/kuzimika na kuacha majivu badala ya kuacha moto. Yeye ameacha fikra. Ebu tudadavue umbeya kidogo:

1. Amewakusanya na kuwaunganisha watanzania. Hata waliohujumu fikra zake wakashika vipaza sauti kumsifia. Duh! Hata shetani anatamani kama wangekuwa wanamaanisha walichokuwa wanaongea bila kupepesa macho! Misiba ni darasa la uongozi.

2. Kanda zote za Chadema zikatoa salamu. Nikajifunza. Kama hatuko tayari kubadilika, badi tupanue mahabusu na magereza. Hakuna hela inayotosha kuwanunua wote, na hakuna risasi za kutosha kuwaua wote. Tunahitaji uongozi, siyo utawala.

3. Freeman Mbowe; Mkwe, mmoja wa waasisi, Mhanga wa maridhiano-hila, M/Kiti Mstaafu na mfungwa wa zamani, “akaiba show” kama alivyoiiba Monduli Februari 2024. Aliongea vizuri. Tunasubiri vitendo. Tomaso ni wengi sana. Ajue: Mkandamizaji wake wa jana hawezi kuwa mkombozi wake wa kweli leo. Awe moto siyo vuguvugu.

4. Madaraka makubwa hayaachani na upofu na ukiziwi. Mwenye madaraka akiona na kusikia, madaraka hupungua na usalama wake kuongezeka. Wananchi huchukua madaraka na kuyatumia kumlinda kiongozi wao. Bunduki haiongezi madaraka bali ni “Kausha madaraka”. Watawala wetu zindukeni.

5. Upofu na ukiziwi ukimpata mtawala, mahabusu na magereza hugeuka vyuo vikuu vya mabadiliko katika nchi. Uhuru wa Afrika Kusini ukiandaliwa Roben Island. Uhuru wa Kenya uliandaliwa Lokitang Prison na Lodwar Prison. Hapajawahi kutokea mfungwa wa kisiasa aliyerudi toka gerezani akamtii mtawala aliyemuweka. Nipe ushahidi!

6. Katika nchi huru “zisizo huru”, mabadiliko huandaliwa katika vyuo vinavyoitwa House Arrests, mazuio ya maandamano, sheria za uchochezi, doria mitandaoni, na Safe Houses. Mahabusu maalum (solitary confinement) huwa ni madhabahu ya kuyeyusha dhahabu iwe bora zaidi. Hakuna barua nyepesi itokayo gerezani. Tunajikaanga.

7. Uhuru ni panga likatalo kuwili. Ukimweka huru mfungwa, mnufaika wa kwanza ni Askari Jela. Alipo mfungwa, yupo Askari. Wote wananyeshewa na wote wanakesha. Mkandamizaji na mkandamizwaji, wote hunufaika na uhuru. Kuwafungulia wafungwa wa kisiasa, ni kuwaweka huru watawala wetu. Mnataka nani aseme ndipo mjue hili ni kwa faida yenu?

8. Nimetoka ibadani. Leo tumehitimisha Ufunuo. Tumekumbushwa kubadilika kwa Bwana Yesu mbele ya wanafunzi wake kule mlimani. Wakatamani kubaki huko utukufuni. Yesu akasisitiza washuke ili kuhudumia wahitaji. Tunaalikwa kushuka ili kuwahudumia watu. Hitaji kuu la watu wetu ni UHURU na THAMANI YA UTU wao. Miradi bila uhuru ni sawa na chakula kizuri kwa mfungwa.

Ngoja niende kula. Kuna Mjaluo hapa kaazima suruali la kwenda kuposea mke wa pili, anasunbua sana hapa mtaani.😅😅
 
Mtei ni jabali na muhimili wa CHADEMA; ndio maana maCCM hawampendi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…