Msiba wa mzee Mtei na heshima kubwa ya CHADEMA Tanganyika

Msiba wa mzee Mtei na heshima kubwa ya CHADEMA Tanganyika

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
MAMBO 7 YALIYOTAWALA HOTUBA ZA MSIBA WA MZEE MTEI NA DIVERSION STRATEGY YA MWIGULU NCHEMBA

Mwl. John Pambalu

Msiba wa Mzee Edwin Mtei haukuwa tu tukio la majonzi, bali pia jukwaa la hotuba nzito zilizobeba tafakuri ya kina juu ya historia ya taifa, hali ya siasa za sasa, na mwelekeo wa demokrasia nchini. Zifuatazo ni hoja saba kuu zilizoibuka na kutawala msiba huo.

1. Urithi wa Mtu (Legacy) dhidi ya Kifo cha Kawaida

Binadamu hufa, wanyama hufa pia. Kinachotofautisha kifo cha binadamu na kifo cha mnyama ni alama ya wema (legacy) aliyoiacha.
Mzee Mtei amefariki akiwa ameacha alama itakayokumbukwa kizazi baada ya kizazi. Wapo watu watakufa na ubaya wao utakuwa mwingi kuliko wema, vifo vyao havitatofautiana na vya wanyama.

Kauli hii nzito na ya kugusa mioyo ilitolewa kwa umahiri mkubwa na Deogratius Mahinyila, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa. Ilikuwa hotuba yenye falsafa, maadili na ukweli usio na kificho.

2. Heche: Tofauti ya Mawazo Sio Sababu ya Kuuawa

Ndogu John Heche aliwakumbusha viongozi wa dini kauli yao ya mara kwa mara kuwa “tutofautiane kwa mawazo lakini tusihasimiane.” Hata hivyo, alisisitiza kuwa katika uhalisia wa Tanzania ya leo, ukitofautiana kwa mawazo na watawala, una hatari ya kuuawa au kupotezwa.
Pamoja na mazingira hayo ya hofu na ukandamizaji, Chadema itaendelea kusimamia haki na kweli, kama alivyofanya Mzee Mtei bila kuyumba.

3. Mbowe: Maridhiano Huponya Taifa

Ndugu Freeman Mbowe alizungumza kama mtu anayetafuta tiba ya taifa lililojeruhiwa. Aliwaambia watawala kuwa wameionea Chadema kwa kiwango kikubwa hadi kufikia hatua ya kuonekana wakali na wakorofi.

Lakini alisisitiza, uchokozi huo ni matokeo ya majeraha makubwa waliyosababishiwa.
Aliweka wazi kuwa maridhiano ya kweli huponya nchi, lakini kwa sasa watawala wanaonekana kukosa dhamira na political will ya kurejesha haki na kuponya taifa. Akahitimisha kwa kusisitiza, kama dhamira ipo, Chadema si chama cha vurugu.

4. Mnyika na Zitto: Historia na Alama ya Mtei
Kwa upande wao, Mnyika na Zitto Kabwe walichagua kuizungumzia historia ya Mzee Mtei kwa kina.

Mnyika alieleza mchango wa Mtei ndani ya chama, akisisitiza jinsi alivyolinda alama na misingi ya Chadema, ikiwemo ishara ya mkono wenye vidole viwili.

Zitto, kwa upande wake, alieleza uamuzi mzito wa Mtei wa kujiudhuru kisiasa kwa kuondoka serikalini kutokana na kutofautiana kimtazamo na Mwalimu Nyerere, uamuzi unaoonyesha uadilifu na msimamo wa mtu.

5. Gavana wa Benki Kuu na Ubaguzi wa Kisiasa

Hotuba ya Gavana wa Benki Kuu Emmanuel Tutuba iliacha maswali mengi. Alitaja makundi mbalimbali yaliyoguswa na msiba, lakini akaepuka kwa makusudi au kwa “bahati mbaya” kulitaja Chadema kama mfiwa.
Hili linaonesha wazi kuwa chuki ya watawala dhidi ya Chadema imevuka mipaka ya kisiasa na sasa imehamia hata kwa watendaji wa taasisi ambazo kimsingi hazipaswi kuhusishwa na migogoro ya kisiasa.

6. Mwigulu Nchemba na Diversion Strategy

Kwa Mwigulu Nchemba, msiba haukuwa nafasi ya kuzungumzia haki, demokrasia, wala mapambano ya marehemu. Badala yake, alichagua kuzungumzia ujenzi wa barabara na mashamba ya wawekezaji.

Wengi walishangaa, imekuwaje hotuba ya msibani iwe nje kabisa ya muktadha?. Hii ndiyo inaitwa sanaa ya diversion, kukwepa hoja nzito. Alitambua kuwa akigusa haki na demokrasia, mada ambazo Mtei alizipigania, mjadala mzito ungeibuka, hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa hakuna haki wala demokrasia ya kweli.

Kwa mantiki ya The Art of War ya Sun Tzu: “Avoid the strong, attack the weak.” Kwa Mwigulu, Haki na Demokrasia ni eneo lenye nguvu mno ambalo linge-backfire endapo angelizungumzia ukizingatia utawala uliopo madarakani kwa sasa umepatikana baada ya mauaji ya kutisha ya raia wasio na hatia.

Zaidi ya hilo, Mwigulu alijitambulisha kama kiongozi wa kile kinachoitwa maridhiano, kwamba ameteuliwa na Samia kulisimamia hilo. Hata hivyo, ukirejea hotuba zake za hivi karibuni za kuwatuhumu na kuwashambulia wasio na hatia kwa madai ya kuwa chanzo cha matukio ya Oktoba 29, 2025, ni wazi kuwa kile kinachoitwa maridhiano kimeshakwama kabla hata ya kuanza.
Kwa maoni yangu, macho yangu yameona hivyo. Muda ni mwalimu mzuri.

7. Generali Ulimwengu: “Man of the Match”

Kwa mtazamo wangu, Generali Ulimwengu ndiye aliyekuwa man of the match. Alisema kwa ujasiri kuwa nchi hii imekwama kwa sababu ya USWAHILI, akimaanisha tabia ya kuzungumza maneno matamu yasiyoambatana na vitendo.
Kwa mujibu wake, Waswahili wana ahadi nyingi lakini utekelezaji hakuna; maneno mengi yasiyo na maana; hujifanya wema ilhali kwa undani ni waovu.
Kauli hii ilikuwa pigo la moja kwa moja, hasa ikizingatiwa kuwa “Waswahili” hao hao walikuwepo msibani.

Swali la Tafakuri

1. Kwa mtazamo wako, “Waswahili” anaowazungumzia Generali Ulimwengu ni akina nani hasa?

Wasalaam,
John Pambalu
Mwalimu wa Zamu
[email protected]
 
MSIBANI NI DARASA LA UONGOZI

Na Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza PhD.

Penye msiba huwa ni darasa la uongozi. Vyuo vya uongozi viwe vinatafuta penye misiba ili kutuma wanafunzi waende “field”. Unabishi? Fikiria haya:

1. Atokee kichaa msibani, achukue kipaza sauti, atangaze na kuamuru wasimame. Kisha atangaze majina fulani na kuwaagiza wabebe mwili ili mazishi yaanze. Kabla hamjagundua ni kichaa mtajikuta mnatii kila kitu. Huo ni uongozi.

2. Mpinzani akihamia chama tawala baadaye akafa, ni msiba wa chama tawala. Mtawala akihamia upinzani akafa, ni msiba wa wote. Unahitaji kuwa kiongozi kutambua tofauti hizi.

3. Katika jamii huria, msiba ni eneo la maridhiano. Hata aliyemroga marehemu analia na kugaragara. Ukitaka kumjua mfiwa halisi, usitazame anayekaribisha wageni. Mfiwa halisi utamkuta, hakukuti. Kuijua tofauti hii ni suala la uongozi.

4. Kwenye msiba, wanaozuiwa kuongea, wakiongea hufariji wengi. Ukweli kuhusu marehemu husemwa vizuri na wanaozuiwa kuongea kuliko wanaopewa kuongea. Msiba hauna mgeni rasmi asiye marehemu. Kuyajua haya ni tasnia ya uongozi.

5. Sijasahau Monduli kumzika rafiki yangu Edward. Waliolazimisha kuongea walitufariji sana kuliko walioongea kiitifaki. Edward alituzodoa sote. Wote tulimwita fisadi; wote tukageuka tukamwita mtakatifu. Aibu yetu wote. Namwona Edward mwingine anatusuta. Tumeteka watu, sasa tunateka misiba. Kutambua HILA misibani unahitaji tasnia ya uongozi.

Kwa haya, hata Wajaluo chotara wananiunga mkono.
 
1769268902609.jpg
 
Hii ilikuwa kwenye msiba wa Bob Makan ambae na yeye alikuwa mmoja wa Waasisi wa Chadema na yeye alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Jeneza la Bob Makani lilifunikwa bendera ya Chama mwanzo, mwisho.

Hata Kikwete akiwa Rais alitoa heshima za mwisho jeneza likiwa limefunikwa bendera ya Chama na alisaidia kubeba Jeneza likiwa liefunikwa bendera ya Chadema.

Bendera ilitolewa wakati mwili unashushwa kwenye kaburi, kiukweli leo sijaelewa Logic ya kuondoa Bendera ya CHADEMA kwenye Jeneza la Mzee wetu Mtei.😤
1769300938359.jpg
1769300941952.jpg
1769300946523.jpg
1769300950585.jpg
 
Lakini alisisitiza, uchokozi huo ni matokeo ya majeraha makubwa waliyosababishiwa.
Aliweka wazi kuwa maridhiano ya kweli huponya nchi, lakini kwa sasa watawala wanaonekana kukosa dhamira na political will ya kurejesha haki na kuponya taifa. Akahitimisha kwa kusisitiza, kama dhamira ipo, Chadema si chama cha vurugu.
Mbowe kwa kweli ni mtu wa kumsikitikia.
Utazungumziaje "maridhiano" na watu unaojuwa wazi, tena kwa uzoefu kuwa hawana dhamira safi?

Anataka alaghaiwe upya ndipo ajue kuwa hakuna watu wa kuridhiana nao katika hawa waliopo?

Hii lugha maana yake ni nini; kwamba bado anaamini dhamira ya waovu hawa inaweza kubadilika na kuwafanya wawe watu wa kuridhiana nao?

Haipendezi kuendelea kumpondaponda mtu huyu aliyewahi kuonyesha alama nzuri katika uongozi wake; lakini kuendelea kung'ang'ania na hawa watu waovu inalazimisha aonekane kuwa ni mtu ambaye kavurugwa sana akili na hawa mashetani.

Anachotakiwa akifanye Mbowe, kwa heshima yake, ni kuwaondoa kabisa akilini mwake hawa Samia na Genge lake; hasa hasa kupitia kwa Kikwete. Vinginevyo, atadumu na sifa mbaya, na hiyo 'legacy' yake mwenyewe itamwonysha hivyo.

Kata mahusiano na watu waovu; hayakujengi kwa vyovyote.
 
Dah!
'Sermons' za namna hii, unasikiliza na kuekewa kinachozungumzwa, halafu usiguswe kabisa; wewe ni binaadam wa namna gani!

Sasa tatizo ni kuwa na ujasiri wa kuyatekeleza hayo uliyosikia; hapo ndipo palipo na mtihani mkuu.

Haijalishi wewe ni mtu wa imani au dini gani, huwezi kukosa kuguswa na mahubiri ya namna hii.
Vimepigwa vitasa vya maana sana
 
Hii ilikuwa kwenye msiba wa Bob Makan ambae na yeye alikuwa mmoja wa Waasisi wa Chadema na yeye alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Jeneza la Bob Makani lilifunikwa bendera ya Chama mwanzo, mwisho.

Hata Kikwete akiwa Rais alitoa heshima za mwisho jeneza likiwa limefunikwa bendera ya Chama na alisaidia kubeba Jeneza likiwa liefunikwa bendera ya Chadema.

Bendera ilitolewa wakati mwili unashushwa kwenye kaburi, kiukweli leo sijaelewa Logic ya kuondoa Bendera ya CHADEMA kwenye Jeneza la Mzee wetu Mtei.😤View attachment 3534068View attachment 3534069View attachment 3534070View attachment 3534071
Hakuna mwenye maelezo kuhusu uamzi huo umetokea wapi?.
Ni serikali FEKI walioagiza iwe hivyo? Kwa sababu zipi?
 
Back
Top Bottom